Utulivu bungeni

Kwa wanaofuatilia Mijadala ya Bunge watakubaliana na mimi kwamba tangu Wabunge wapenda vurugu waliposimamishwa kushiriki Vikao vya Bunge,hali ya utulivu imerejea Bungeni.Hivi ndivyo Bunge letu linavyotakiwa kuendeshwa kwa Wabunge kujenga hoja zenye manufaa kwa Wananchi na siyo kila siku kuomba miongozo isiyo na tija.

Mheshmiwa Naibu Spika,
pamoja na kuileta mada hii huku JF bado hukuridhika ukaamua kuhitimisha nayo kikao cha leo jioni??
 
Naibu Spika wa bunge Job Ndugai amesema kwa siku hizi nne bunge limekuwa tulivu watu wanachangia hoja kwa utulivu na maelewano makubwa.

Huku akizungumza kwa kejeli na dharau kubwa amesema kwamba ameombwa na wananchi waliompigia simu aongeze adhabu aliyokuwa ametoa kwa wabunge wa Chadema ili utulivu huu uendelee bungeni.

Hata hivyo amesema kwamba amekataa maoni hayo ya wananchi na badala yake adhabu ya siku 5 aliyokuwa ametoa ikiisha atawaruhusu warudi bungeni.

Amesema adhabu aliyotoa kwa wabunge wa Chadema sio kuwakomoa bali ni kuwanyoosha na kuwafundisha adabu na taratibu za kibunge.

Wakati akizungumza alikuwa akishangiliwa kwa mayowe na wabunge wa CCM.
 
Hao wabunge waliobaki wanalalamikia serikali lakini baada ya hapo wanaunga mkono hoja na kutusababishia umasikini
 
Kwani bunge tulivu la miaka ya 2002 limetusaidia nini? bora bunge hili linawafanya angalau mawaziri wahusishe ubongo
 
Ukiambiwa umetumwa unalalamika uzi wako na hitimisho la ndugai havitofautian

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Mbogo, unaanzisha thread nyingine ya nini? alafu kama umepanga na naibu speaka maana muda fupi sasa naye katoa kejeli ya adhabu aliyoitoa kwa wabunge wa cdm bila kujari athari zilizowapata magamba nje ya bunge.
 
Kwa wanaofuatilia Mijadala ya Bunge watakubaliana na mimi kwamba tangu Wabunge wapenda vurugu waliposimamishwa kushiriki Vikao vya Bunge,hali ya utulivu imerejea Bungeni.Hivi ndivyo Bunge letu linavyotakiwa kuendeshwa kwa Wabunge kujenga hoja zenye manufaa kwa Wananchi na siyo kila siku kuomba miongozo isiyo na tija.
Duuuuuh...! Anyway huo ni mtazamo wako tu.
 
Ni kwa "utulivu" huo tumeshuhudia bilioni 29 zikipelekwa kwenye PDU na milioni 300 zikiidhinishwa kununua magari mawili ya serikali... Utulivu my foot
 
umeacha hizi

serikali ni maha...ni..th.......mbunge chadema
....waziri mpumbavu.....mbunge chadema
rais ni mdini.........mbunge chadema


umeacha hizi

maha...ni..th.......mbunge chadema


Kwanza impotent sio sahihi kusema ------- ni uzushi kwa maana nyingine wewe na ccm wenzio ni wafa maji ........

Impotent means non productive

Serikali ya ccm ni non productive in every aspect, Elimu, afya, kilimo, miundombinu, maji nk sasa kuna kosagani

kusema serikali hii ni impotent- non productive.


....waziri mpumbavu.....mbunge chadema

Ni kweli kabisa mawaziri wa serikali ya ccm niwapumbavu, nitathibitisha hoja na dhana hii

1. Elimu kuanzia kwa takribani miaka saba mfurulizo graph ya elimu inashuka na cha ajabu mwaka matokeo 2012 zaid ya

90% form four ni falure. Huu ni upumbavu ulivuka mipaka hawa mwaziri wa elimu wanaliangamiza Taifa.

2. Afya mpaka sasa wenye uwezo wote wakiwemo wabunge mawaziri nk, wamegeuza India ndiyo kimbilio je na sisi maskini tuende wapi? zahanati na hopitali za erikali zimebaki majina hakuna lolote zaidi ya majengo na upuuzi mwingine-tiba hakuna, huu sio upumbavu wewe unakimbilia ujerumani kutibiwa raia wako wanateketea tena unaafukuza kazi madakitari!!!!!!!!!!!!

3. Kilimo mpaka sasa mkulima yule wa kijijini ndiye anayebeba gharama zote za kipuuzi, mfumko wa bei, bei ya ovyo kwa mazao yake, kuibiwa mazao yao mfano korosho, pamba na tumbaku, hata mafuta ya taa kwa faida ya mafisadi waakulima wanauziwa bei mbaya kisa matajiri wasichakachuwe petrol huu sio upumbavu????

4. Usafiri wa anga mpaka sasa Rwanda hapo mjini Kigali wanandege zaidi ya Tano, tanzania pamoja na utajiri wote tunandege ngapi??? huu sio upumbavu???

5. Usafiri wa reli mpaka sasa tunasuasua na huu ndiyo usafiri wenye gharama ndogo na bora duniani hususan kwa mizingo, katika hili huko kenya wanaplani treni za umeme kwa abilia, sisi hata hizi line mbili kati na TAZARA tuko hooi bin tabani huu sio upumbvu???

7. Maji safi na salama, mfano ni bungeni leo jion, maji yamezua mjadala mpana, miaka 50 tuko huru pamoja na rasmalimali nyingi tulizonazo watu wanalialia, pamoja na vyanzo kibao hali ni mbaya kabisa kwanini?? huu siyo upumbavu????

8. Umeme, tunaibiwa kila siku kwa mipango mibovu, mikataba ya ovyo IPTL, RICHMOND, nk umeme wa uhakika miaka 50 tuko huru hakuna sababu nini, huu sio upumbavu???


rais ni mdini.........mbunge chadema

Mwenyekiti wa ccm taifa ni kikwete - ndani ya ilani ya ccm imeandikwa nini na katiba inasema nini??

Kama Rais, kwanini katika utawala wake kuna matukio zaid ya 70 kuchomwa au kuhalibiwa nyumba za ibada amekamata na kufunga wangapi? kama bado amewachukulia hatuagani maafisa polisi waloshindwa kuwakamata wahalifu kama hapana yupo upandegani? tusaidie jibu!

Ni vipi baadhi ya wahubiri kuachwa wakifanya uchochezi kwa vibali vya serikali yake nchi nzima wakihamasisha mauwaji bila kuchukuliwa hatua. Baada ya miezi sita mbegu kumea, watu wanauwana watu wanagombania kuchinja ndiyo rais na serikali yake anakurupuka huu sioyo udini? alikuwa anangoja watu wachinjane au yeye ni sehem ya mkakati siasa udini!!


Mawaziri ni wapumbavu na huu ni ukweli, unaweza kukanusha kwa kupinga kila hoja niliyoiweka hapo juu????
 
Mkuu Mbogo-1 angalia kauli hizi kama mfano tu.

Siongei na mbwa (mbunge) naogea na mwenye mbwa (kiti cha spika) - mbunge ccm

wagunge wanamimba zisizotarajiwa - mbunge ccm

Camooon ---- you - mbunge ccm

Slaa anafanya mikutano na viongozi wa kidin na cdm ni wapuuzi sana - mbunge ccm

bajeti ya wapinzani kutupiliwa chini - mbunge ccm

Ni baadhi tu ya kauli hatarishi za kuudhi na kupelekea vurugu bungeni, tafakali angalia chanzo (source) sio matokeo

(outcomes) be smart in your presantation.
Mwambie huyo,coz anakurupuka tu na kutufanya wengine hatufuatilii mijadala ya bunge..WABUNGE WALIOTOLEWA BUNGENI NI WAPIGANIA HAKI ZA WATANZANIA WOTE BILA KUJALI MASLAHI YA VYAMA.
 
Kwa wanaofuatilia Mijadala ya Bunge watakubaliana na mimi kwamba tangu Wabunge wapenda vurugu waliposimamishwa kushiriki Vikao vya Bunge,hali ya utulivu imerejea Bungeni.Hivi ndivyo Bunge letu linavyotakiwa kuendeshwa kwa Wabunge kujenga hoja zenye manufaa kwa Wananchi na siyo kila siku kuomba miongozo isiyo na tija.
Kachukue posho wewe kilaza, wabunge wanaojua kazi yao ya kuisimamia serikali unasema wenye vurugu kweli tumekwisha kama ndio mawazo ya watanzania hayo.
 
Kwa wanaofuatilia Mijadala ya Bunge watakubaliana na mimi kwamba tangu Wabunge wapenda vurugu waliposimamishwa kushiriki Vikao vya Bunge,hali ya utulivu imerejea Bungeni.Hivi ndivyo Bunge letu linavyotakiwa kuendeshwa kwa Wabunge kujenga hoja zenye manufaa kwa Wananchi na siyo kila siku kuomba miongozo isiyo na tija.

Haya ni mavi ya kuku, na hapa si mahali pake. Yapeleke kwingine na si kwenye mtandao wa watu makini kama JF.
 
Kujaa kwa wabunge wa Ndio mzee! Ndio utulivu bungeni? Basi nchi hii ni aibu tupu na ndio maana pamoja na rasilimali zote sie tunaongoza kwa umasikini.
 
Hakusema hivyo bali alitumia neno la Kiingereza impotent akimaanisha dhaifu. Tuangalie context ndipo tutajua alimaanisha nini. Kwa hiyo Mhe. Wenje hajatukana.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums

Unajua mtu asiejua lugha ni kazi kumuelewesha...ukisema govt (ni combination ya all gender) sasa is impotent kuitafsiri kama "mwanaume asiejiweza kiume" ni tafsiri ambayo ni illogical kwa kweli!
 
Back
Top Bottom