SoC03 Uthubutu na kuiweka hofu kando, kila kitu kinawezekana

Stories of Change - 2023 Competition

Njile bushokero

New Member
Jul 3, 2023
2
1
Haujambo mwafrika, haujambo mtanzania?

Katika jukwaa la stori za mabadiliko, ninayo furaha kubwa kuwasalimu kwa jina la mtanzania na muwe na amani hata milele Amina.

Niko na wazo langu, ambalo kupitia jukwaa hili, huenda likaleta mabadiliko kwenye jamii yetu ijapo hata kidogo tu.

Nina uliza, je tunaweza kuifanya miili yetu iwe kama jukumu la kupata uzoefu katika kila jambo maadamu tungalipo hai?

Nime fikiria ya nyuma hadi nyakati za ukoloni, kwamba jamaa zetu hawa wa ng'ambo, walikuja na elimu, wakaja na dini, wakaja na teknolojia, wakaja na uboreshaji wa aina mbalimbali uhusianao na maisha ya binadamu.

Dhana mbalimbali za matumizi ya kila siku ya binadamu, wakaboresha kutokana na ugunduzi wao.

Hadi sasa jamaa zetu hawa, bado wanaendelea kufanya hivyo, bado wanaendelea kuboresha maisha ya binadamu duniani kutokana na uvumbuzi wanaovumbua kila kuchao.

Ikiwa kila ninachokitumia, kinatokana na ugunduzi wao, je mimi nimefanya nini sasa katika dunia hii? Au jukumu langu ni nini katika dunia hii?

Ninazungumzia uhalisia na ukweli uliopo, tumefanya nini kama Waafrika? Tumefanya nini kama Watanzania? Au jukumu letu hapa duniani ni nini?

Je, mmoja anaweza niambia jukumu la kuwa binadamu ni nini? Hakuna hata mmoja atakuwa na jibu sahihi, maana tunayoyafanya hata viumbe wengine wanafanya.

Kama ni kuzaliana je, viumbe wengine hawafanyi hivyo? Kama ni riziki je, viumbe wengine hawafanyi hivyo? Maana riziki ni kwa ajili ya kula wala siyo vinginevyo.

Lakini swali hili ukimuuliza Mzungu, atakujibu kirahisi tu, na zaidi sana atakuambia jukumu la yeye kama Mzungu, swali hili ukimuuliza Mchina atakujibu kirahisi tu, na zaidi sana atakuambia jukumu la yeye kama Mchina kwa sababu wao wanajua jukumu la kuwa binadamu ni nini.

Je, mwafrika unajua jukumu la kuwa binadamu? Je, mtanzania unajua wajibu wa kuwa mtanzania? Kama unajua jukumu la kuwa binadamu, je, ni lini utatumia mwili wako na hakili zako kikamilifu? Maana hakuna dunia nyingine ila ni hii tu, na jukumu la binadamu, ni kuwa na suluhisho kwa kila kitu maadamu yu hai.

Kama unajua wajibu wako kama Mtanzania, je, hadi lini utajiona mudhaifu na mnyonge, juu ya taifa lako kana kwamba haustahili kuwa mtanzania? Maana kuna Tanzania moja tu, na wajibu wa mtanzania ni kuwa na bidii ya kuiboresha Tanzania, je, hadi lini utakuwa mzembe katika wajibu wako?

Je, hauoni kwamba watu wa mataifa mengine wao siyo wanyonge wala siyo wazembe, maana wanaitumia miili yao kikamilifu kama binadamu, kwa kuboresha mataifa yao.

Kwa hiyo, najaribu kuuliza kwamba, je tunaweza kuifanya miili yetu iwe uwezekano wa ushuhuda wa kile tunacho kifanya hapa duniani?

Sisi kama watanzania au sisi kama waafrika, tekinolojia tunayoitumia siyo yetu, elimu tunayoitumia siyo yetu, dhana mbalimbali za matumizi ya kila siku, siyo zetu.

Pamoja na kuwa kwamba hayo yote siyo yetu, bali tumejifunza kutoka kwa jamaa zetu wa ng'ambo, lakini tumeyaona kwamba yanafaa, elimu inafaa, dini zinafaa, teknolojia inafaa, dhana mbalimbali za matumizi ya kila siku zinafaa, ndiyo maana tunajifunza na bado tunaendelea kujifunza namna ya kuzitumia au namna gani ya kuzitengeneza.

Jambo ambalo napenda kuuliza, je, tutakuwa wanafunzi hadi lini? Tutajifunza vitu vilivyogunduliwa kwamba vipo hapa duniani hadi lini? Je hili ndilo jukumu letu? Kwamba ni kujifunza tu, wanagundua watu wengine sisi tunaenda kujifunza, wanaboresha watu wengine sisi tunaenda kujifunza, hili ndilo jukumu letu kama watanzania?.

Hili siyo jukumu letu, maana na sisi ni binadamu kama wengine, hili siyo jukumu la mtanzania maana yeye naye ni binadamu kama wengine, hili siyo jukumu la mwafrika maana yeye naye ni binadamu kama wengine.

Hivyo nauliza, je, tunaweza kuifanya miili yetu iwe ushuhuda wa kile tunacho kifanya hapa duniani? Je, tunaweza kubeba jukumu letu kama binadamu, Na tuijenge Tanzania ya kushangaza? Tuijenge Afrika ya kushangaza? Je, tunaweza kubeba jukumu hilo?

Ndiyo tunaweza, tunaweza kuiondoa hofu na kuwa na uthubutu, ndiyo tunaweza kuwa na uthubutu zaidi ya hofu, kwa sababu hofu ndiyo inayoendelea kutubakisha hapa na kutufanya tuendelee kuwa wanafunzi, ikiwa tutaiweka kando hii hofu na hatimaye tuwe na uthubutu, tutaenda mbele tena kwa kasi ya ajabu.

Cha kuambiwa changanya na chako, ikiwa tutakuwa na uthubutu na kuwa tayari kwa kuitumia miili yetu kikamilifu, yale tuliyojifunza na yale ya ndani mwetu, tukiyaweka pamoja, pia sisi tutakuwa walimu badala ya kuwa wanafunzi.

Niaminini, maana elimu haikushuka kama mvua, bali ni akili ya binadamu katika uthubutu, tunaishi kwa mara moja tu, na tupo hapa duniani kujishughulisha, na tunaweza kuifanya Tanzania ya kupendeza maadamu tungalipo hai, ikiwa tutakuwa na uthubutu huo kila kitu kinawezekana maana hakuna jukumu baada ya kifo, bali jukumu ni sasa, kuifanya Tanzania ya kupendeza kuifanya Afrika ya kupendeza na dunia kwa ujumla.

Kama ni mbinguni utaingia baada ya kufariki, lakini maadamu ungalipo u hai bado, jukumu lako ni kuushughulisha mwili, maadamu unaweza.

Sasa hivi tumekuwa na uthubutu, hivyo hakuna jema mbele yetu wala hakuna baya mbele yetu, maana ubaya ukizidi sana ni jema, na jema likizidi sana ni baya, kwa sababu hiyo, sisi tunajua kuwa binadamu, katika yote hayo, na kila kitu kilicho mbele yetu tutakifanya kuwa uwezekano wetu wa kupendeza, kwa sababu sisi ni binadamu.

Twendeni tukalifanye kila jambo linawezekana kwa sababu hii ndiyo sifa ya binadamu na ndiyo jukumu lake, twendeni tukaifanye Tanzania uwezekano wa kupendeza, maana hili ndilo jukumu letu kama watanzania, tuwe mwenye uthubutu, na kuuruhusu ubongo ufanye kazi yake bila shinikizo lolote, maana mafikirio ni kioo cha kukuonyesha kitu ambacho hauwezi kukipata, lakini ukiwa na uthubutu utakipata.

Twendeni tukawe na uthubutu katika kila jambo, lakini huku tukiuheshimu muda na kufahamu ya kwamba kila kitu kina wakati wake. Asanteni 🙏!

(Wasalaam)
 
Back
Top Bottom