SoC03 Uthubutu wako ndio Chachu ya mabadiliko

Stories of Change - 2023 Competition

desmond3076

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
278
182
Naitwa Desmond sio jina halisi,nilimaliza Elimu ya msingi miaka kadhaa iliopita ,japokuwa sikuweza kuchaguliwa,kujiunga na Elimu ya upili, ilinilazimu kurudia tena mwaka mwingine na hatimae kuweza kufanikiwa kujiunga na shule ya upili huko wilayani tarime mkoa wa Mara.

Maisha ya Elimu ya upili yalikuwa magumu sana ikiwemo kutembea zaidi ya kilomita 12 kuifikia shule hii ya upili niliochaguliwa. ilinilazimu kuamka saa 11 Ili kuanza safari, maana " niliamini ule usemi wa mtaka Cha uvunguni sharti ainame" nilipata tabu sana wakati wa mvua, ukizingatia ni vijijini na barabara lenye tope Kuna wakati ilitulazimu kubeba hata viatu.

Nilifanikiwa kumaliza na kujiunga kidato Cha Tano mkoani mwanza pamoja na vurugu za makondakta maana wanafunzi kwenye daradara tulikuwa kero kwao. Baada ya Safari ndefu ya Elimu ya kidato Cha Tano na Cha sita , nilifanikiwa kufaulu vizuri ,badala ya kwenda chuo kikuu enzi hizo Kwa kukosa pesa ,niliona ni bora kujiunga na Elimu ya ualimu yaan stashahada na hatimae kumaliza chuo Cha ualimu Bunda na hatimae kuajiliwa.

Maisha ya ualimu yalikuwa na changamoto kubwa Mshahara MDOGO, mazingira sio rafiki, maana nilipangiwa vijijini, katika shule ya sekondari kama mwalimu wa historia na jiografia. Pamoja na hayo yote nilifanya KAZI Kwa bidii na badae nilipata pesa Kwa kujishughulisha na kilimo na hatimae kupata ada maana nilitamani kufika chuo kikuu, kwani mshahara wangu kama mwalimu ulikuwa MDOGO Kwa ngazi ya diploma . Ada niliopata ilinipa msukumo wa kujiunga na chuo kikuu hivo kuhitimu shahada ya Sanaa na ualimu.

Nilipoludi kutoka masomoni nilikuta uongozi umebadilika, Mkuu wa Shule alikuwa mbabe Hana utu na hajali walimu, hii ilipelekea walimu wengi kila kukicha waliwaza kuhama Mimi pia nilikuwa mmoja wao, yeye alikuwa hanipendi Kwa sababu kwanza nilikuwa na Elimu kumzidi hivo aliniona kama mwana harakati Fulani. Nilitamani kuhama lakini sikufanikiwa.hivyo nilikuwa nikifindisha Kwa shingo upande sana.

Mwaka 2018 sitousahau nilipokea barua kuwa nilitakiwa kuhamia primary, jambo hili liliniuzunisha nilijiuliza " nilitawezaje kukabiliana na MABADILIKO haya katika maisha yangu, na nilijua kuwa yote yalisababishwa na mkuu wa Shule kisa tulikuwa hatuelewani na ni kweli ni yeye aliyekuwa kisababishi. Niliandika barua kukubali nililipwa pesa ya usumbufu na nikaanza maisha mapya kama mwalimu wa Shule ya msingi.

Maisha ya shule msingi kama mwalimu kiukweli yalikuwa mageni. Fikiria kuanza kufundishia watoto Kwa kiswahili Mimi nimezoea kingereza, hapa nilijihisi nimepotea, nilikuwa mtu wa HUZUNI sana, nashukuru nilijipa moyo, nikaanza kufundishia Somo la kingereza, ambalo niliona ni changamoto kubwa katika shule nilioamishiwa, ebwaana ee nilitokea kupendwa na watoto na wao kulipenda Somo la kingereza, hatimae katika mtihani wa kuhitimu Elimu ya msingi wanafunzi walifanya vizuri, ikawa gumzo Kwa shule ya serikari kuzishinda shule za mtaala wa kingereza katika wilaya na mkoa wangu.

Kila nilipokuwa nabadilishiwa Somo ,lazima Somo Hilo liongoze , maana nilifuta tabia iliokuwa inasema wale walimu wa Shule za sekondari walioshushwa kufundisha Elimu msingi hatuwezi kufundisha masomo ya shule za msingi, nilianza kuyakubali MABADILIKO, nilianza kutamani kufundisha Madarasa ya awali Ili kuweza kutatua changamoto ya K.K.K.(kusoma kuandika na kuhesabu) nashukuru uongozi ulinikubalia, nilianza kufundisha darasa la kwanza , niliamini katika matumizi ya zana , nilikuwa mbunifu, na hatimae kulipamba darasa Kwa zana.

Darasa la kwanza katika shule yangu likawa sio tu linazingumza , likawa linaimba , walimu walipoona KAZI niliofanya walinipongeza,taarifa zikafika juu, viongozi wakaja kutizama na kujifunza jinsi ya utengenezaji wa zana za kufundishia, darasa lile likawa la mfano, Kila nikiwaeleza nimetokea sekondari hawakuamini.

Madhumuni makubwa ilikuwa nikufuta dhana ya kuwa hatuwezi kubadilika na kuendana na Elimu msingi, lakini kwangu Mimi nimeweza. Hasa pale walipokuja kufahamu watoto 71 kati ya 71 waliweza kusoma kuandika na kuhesabu ndani ya miezi mitatu.

Hivyo kupitia hadithi hii ambayo ni ya kweli sio ya kubuni ambayo imeyahusu maisha yangu kama Mwalimu unaweza kubadilisha maisha Yako, kulingana na mazingira unayoenda na hivo ukawa mfano na kuleta MABADILIKO na kupitia wewe watu wakajifunza. Hadi Sasa shule yangu ni moja ya shule zinazofanya vizuri kitaaluma.

Imeandikwa na Desmond 3076.
 
Fanya mpango ujiajiri naamini hilo linawezekana na uttafurahi mno kikubwa uthubutu kama ulivyokubali kubadili mtazamo wa uliporudishwa primary
 
Back
Top Bottom