Uthibitisho wangu kwamba Ben Saanane/Mamuya ni watu hatari ndani ya chama

Mtela Mwampamba

JF-Expert Member
Dec 19, 2012
537
347
Habari wana JF mimi ndiye Mtela Mwampamba ambaye nilikuwa mgombea ubunge mbozi mashariki na pia nilikuwa mgombea uenyekiti bavicha taifa,

Nimekuwa nikifuatilia kwa makini sana mijadala inayoendelea humu JF na nimekuwa nikihusishwa na tuhuma mbalimbali na nimekuwa nikitajwa jina langu kwa kuhusishwa na majina mbalimbali ambayo kwa kweli mimi siyafahamu,

Kwanza naomba kukiri kwamba namfahamu vizuri sana Ben Saanane na Exaud Mamuya uso kwa uso, kufahamiana na hawa jamaa ilikuwa ni katikati ya mwaka 2011 katika uchaguzi wa BAVICHA Ben Saanane akiwa mgombea wa nafasi yangu na Exaud Mamuya akiwa mpiga kura kutoka Arusha.

siku ya kwanza kuanza mawasiliano mimi na Ben Saanane ni siku ambayo mgombea wa nafasi yangu ndugu Habibu Mchange alienguliwa katika kinyang'anyiro na kamati kuu ya chama, Ben Saanane alinipigia simu nakunijuza kwamba kamati kuu umemuengua Mchange ili bwana Heche ashinde katika uchaguzi huo na mimi nikiri wazi kabisa bwana Mchange ndiye aliekuwa anaonekana mwenye nguvu kutuzidi sisi wagombea wengine kwa hio Ben Saanane alitumia mwanya huo wa kuenguliwa bwana Mchange kama ni lengo la kamati kuu kumpitisha bwana Heche kirahisi na pia Ben Saanane aliniambia kwa habari za kiintelijensia ni kwa Mwampamba, Nyakarungu na yeye mwenyewe tuko mbioni kuenguliwa katika kinyang'anyiro kile.

Ben Saanane akaniomba tuonane nae mimi nikamkubalia tukaonana nae maeneo ya Hill Park akanishauri kwamba yeye na ndugu Nyakalungu wako tayari kujitoa katika uchaguzi ule nawataniunga mkono mimi ili tuweze kushinda nguvu ya heche ya kubebwa na vigogo wa chama na nikiri kweli kwa mazingira ya uchaguzi ule bwana Heche alibebwa moja kwa moja kwa ushahidi wa mazingira yaliowekwa katika uchaguzi ule.

Ndugu wana JF, nakiri siku ya kwanza sikujua kwamba huu ni mkakati wa wanamkakati wa kutaka kunimaliza kisiasa na kuendeleza siasa zao za kibaguzi kwa mtu yeyote anaeonekana ni mwiba katika ulaji wao, kwa sababu nilikuwaa na imani kubwa sana na nyakalungu kwa hio sikuwa na shaka katika hilo,siku ya uchaguzi nikasomewa mashtaka nane ya bila ushahidi na nyakalungu akasomewa mashtaka bila ushahidi halikadhalika nab en akasomewa mashtaka bila ushahidi na tukaenguliwa katika kinyang'anyiro hicho kisha heche akapita na akawa mwenyekiti wa bavicha taifa.

Kwa kuwa nilijiunga CHADEMA ili nifanye harakati za ukombozi wa pili wa Mtanzania na wala sio kupata cheo basi nikaendelea na ujenzi wa chama katika jimbo langu la uchaguzi na maeneo mbalimbali nchini kwa kueneza sera za chama.

Nikiwa katika harakati zangu hizo za chama na maisha binafsi nikaanza kupigiwa simu mara kwa mara na Ben Saanane kwa lengo la kutaka tuonane pia nikagundua kwamba akiwasiliana na mimi huwa anawasiliana pia na Mchange, Nyakalungu na Juliana Shonza kwa lengo kuu la kutaka kuonana,tukawa tunaonane na anatushauri kutomuunga mkono heche na kutushawishi kutowaunga mkono katibu mkuu na mwenyekiti kwa sababu walimbeba Heche na pia alitumia muda wake mwingi kunishawishi mimi nimkutanishe na Zitto ili aweze kumsaidia ni jinsi gani atamsaidia katika kufanikisha mpango wake wa kutowaunga mkono Mbowe na Dr. Slaa,

Kwa kweli nikawa na shaka sana kwa huyu jamaa kwa nini anataka kuongea na Zitto maswala ya BAVICHA wakati Zitto sio BAVICHA nikajaribu kumuuliza Mchange kuhusu swala hilo bwana Mchange alikataa kata-kata kumkutanisha Zitto na ndugu Ben Saanane.

Ben Saanane amekuwa akija mpaka nyumbani kwangu akinishawishi nimukutanishe na Zitto lakini nikawa namzungusha kwa sababu tayari Mchange alinidokeza kwamba Ben Saanane anakazi maalum ya kufanya juu ya Zitto na kwetu anatumia kama njia ya kutaka kuonane na Zitto na kisha kumdhuru na nikiri ya kwamba mara ya kwanza sikumwelewa Mchange lakini baadaye nikamwelewa kwa sababu Ben Saanane aliongeza juhudi za kunipeleleza kuhusu maisha ya Zitto na jinsi ya kumpata Zitto ili waongee. Ben Saanane alijitahidi sana kutushawishi kwamba tuwe na kikundi cha kuwapinga viongozi wa chama(ushahidi ninao) lakini hakuweza kufanikiwa maana lengo lake lilikuwa ni kumuua Zitto kwa sumu kitendo ambacho tulimshikukia na tukaanza kumkwepa(ushahidi upo).

Ben alitumia pesa nyingi sana katika kila vikao ambavyo tulikuwa tunafanya na mara nyingi alikuwa anaanzisha mijadala na kuwaponda Mbowe na Dr. Slaa ili sisi tumuunge mkono na aturecord na sio siri Ben Saanane kanirecord sana mimi mpaka siku Mchange aliponiambia kwamba ben huwa anakurecord kwa kupitia saa yake ya mkononi na simu yake baada ya kugundua hilo nikaanza kumfatilia Ben Saanane na nikagundua kweli ananirecord nikamwambia ukweli na siku hio tuliweka tego hilo nikiwa na ndugu Gwakisa, pia Gwakisa akamwambia ukweli maana nae alikuwa anarecodiwa mara kadha wa kadha akiwa na Ben.

Baada ya kushtukiwa mpango wake wa kumuua Zitto na kutuharibia sisi kisiasa ndipo Ben Saanane alipo amua kutafuta Id fake na kuanza kututaja kwa majina kwamba Mwampamba,Juliana,Gwakisa,Mchange na Nyakalungu ni wakina Tuntemeke wanaomchafua Slaa na Mbowe na ameanza kufanya hayo baada ya sisi kumshtukia kwamba Ben Saanane anaishi mjini kwa kutengeneza migogoro mfano amenikosanisha mimi na katibu mkuu Slaa(ushahidi ninao).

Kama kuna mtu aliewahi muona Ben Saanane kwenye ujenzi wa chama mahara popote alete ushahidi humu JF mimi ninavyomfahamu Ben Saanane ni kwamba hajawahi husika sehemu yeyote katika ujenzi wa chama zaidi ya kutengeneza migogoro ndani ya chama na kisha kujifanya kama yeye ndie mwenye uwezo wa kutatua migogoro hio ili aweze kujipatia kipato kama alivyofanya sasa kwa kumtumia mtu asiye jitambua exaud mamuya. Ben saanane anatengeneza migogoro ili alipwe posho na vigogo ndani ya chama na vigogo hao ni mabingwa wa kupika na kusikiliza majungu na wamekuwa wakimtuhumu mtu yeyote wanaehisi anawakosoa na wanamwita mfuasi wa Zitto, ninamambo mengi sana lakini kwa sababu ben amesema atapeleka mashtaka kwa katibu mkuu huko ntafunguka kisawasawa.

Mimi nakiri kwamba nafahamiana na Zitto, Zitto ndiye role model wangu kisiasa na nitafurahi sana Zitto akiwa rais wangu ajae maana ni mtu mwadilifu,mwenye uwezo na mwajibikaji pia Zitto sio mpika majungu,msikiliza majungu,mfitini halikadhalika zitto sio mkabila,mdini na mtu wa ukanda kama walivyo wengine.

Namshukuru mwenyezi mungu kwa kutuepushia wakina IDDI AMINI katika taifa letu la Tanzania maana ni bora vita ya kifisadi tunayopigana sasa kuliko vita na ukabila na udini inayotengenezwa ndani ya taasisi zetu huku watanzania wakifumbia macho na kuitana makamanda. Wale tuliojitolea kujenga chama kwa kwa moyo wote na nguvu zote kwa uaminifu ndio tunaoitwa wasaliti kwa sababu tunawakosoa! Wale wanaoishi kwa kutumia kodi zetu(ruzuku ya chama),wenye kadi mbili, wanaolipwa mishahara minono, wale wanaowatumia mahawara wao kuzunguka mikoani na kutafuta wagombea ubunge kwa kutumia kodi zetu, wale wanaopewa pesa na wanachama wa CCM(Sabodo), wale wanaofadhiliwa na CCM katika maisha yao ndio wanaoitwa makamanda kwa sababu ya ushabiki na ulimbukeni wa kisiasa tulionao baadhi ya vijana tuliojiunga ndani ya vyama baada ya uchaguzi mkuu na wanadhani kwamba viongozi ni mwingu watu na kuna watu wanaotakiwa kukosolewa na watu wanatakiwa kuabudiwa!

Wana JF ,Naomba mnielewe kwamba kutomuunga mkono Mchungaji au Padre mnafiki, mpika majungu, mfitini, anaendesha kanisa kwa maono ya hawara yake, mkabila, ndumilakuwili haimanishi kwamba nimelihasi kanisa, kanisa huendeshwa kwa maono ya biblia na mchungaji au padre anaweza anaweza potosha kondoo wake kama alivyofanya mchungaji Kibwetere kwa kuwaangamiza kondoo wake waliokuwa wanamwaminia kuliko Biblia.

Mimi ninaamini katika taasisi imara ambayo ni CHADEMA niliyoijenga na ninayoijenga kwa kushirikiana na wenzangu kwa nguvu na moyo wote kikamilifu.sijapenda sana kumuelezea Exaud Mamuya maana namfahamu ni kijana asiye jitambua na muda wote yeye hufanya kazi ya ukuadi hata wanaBAVICHA huwa wanampuuza ndio maana kuna kipindi alichukua form ya kugombea uongozi BAVICHA(unaibu katibu) akaambulia kura sifuri maana kila mtu humpuuza kwa kuwa wanamfahamu akili yake.

R.I.P CHACHA ZAKAYO WANGWE, PHILLIP MAGADULA SHELEMBI.
Bado tunaendeleza harakati mlizoziacha na wala hatutakata tamaa hata wakitumaliza wote wapo watakao zaliwa wenye maono kame yenu na ni malize kwa kusema mimi sio kitoweo cha wajinga ndio waliwao.

CHADEMA HURU KWA MASLAHI YA KITAIFA
MAJIBU YA BEN:
5266907]Sikupenda kuingia tena katika majadiliano haya zaidi ya kusubiri vikao vya Chama. Kwa kuwa kundi hili linaendeleza mjadala na upotoshaji wa pale alipoishia kiongozi wa kundi nimeona si vyema kukaa kimya. Mchange anasema hakuwa wa kwanza kunitafuta mimi as if hii ni hoja ya Msingi sana. Hata Zitto sikuanza kumtafuta mimi ila yeye hasa baaada ya kuenguliwa uchaguzi wa BAVICHA. Nitaweka baadhi ya mawasiliano yake ya kwanza yakiwemo ya tarehe 29/05/2011 siku iliyofuata baada ya kuenguliwa BAVICHA.

Kwanza NI KWELI kundi hili la PM7 lilikuwepo. Ni kweli tulishirikana kaktika mpango huu.Kwanza jina PM7 ni miongoni mwa majina yaliyopendekezwa miongoni mwa majina mengine. E-Mail aliyotuma Mchange hapo juu ni e-mail ambayo nilimtumia Zitto Kabwe na tulikubakliana mimi na yeye isajiliwe taasisi ambayo tutakua tukiendesha harakati bila kujipambanua waziwazi na malengo ya taasisi hiyo. Lengo kuu la Taasisi hii lilikua ni kuanzisha vuguvugu la vijana na kulitumia kama platform ya kisiasa na kijamii ambayo ingekuwa non-partisan baada ya taasisi ya ADO kutokuwa active. Pia ingekuwa taasisi ambayo ingefanya harakati za baraza huru la vijana. Zitto alipokea wazo hili kwa furaha.Hata hivyo lengo la Taasisi lilibadilika na kuwa na malengo ya kisiasa ndani ya chama na wakati huo huo tukitafuta njia ya kubeba kundi la masalia kisiasa. Zitto alikuwa ameshaanza kuzunguika na kundi hili kwenye mikutano ya hadhara mikoani. Mimi ndiye niliye-draft contents zote ambazo hata hivyo Mchange hajathubutu kuziweka zote hapa.Tulitohoa jina la PM kutoka katika taasisi hiyo niliyoipa jina la Youths Patriotic Movement

Ninayo mawasiliano yangu na Zitto kuhusu kundi hili na alinihimiza wakati huo akiwa Songea kwenye kampeni za udiwani kwenye chaguzi ndogo za udiwani akiwa na akina mwampamba na Shonza.Tulikubaliana kwamba hii taasisi isajiliwe haraka sana iwezekanavyo namnukuuu YPM MUST BE REGISTERED SOON AND GO COUNTRYWIDE mwisho wa kunukuu. Ndugu Zitto, bila shaka anaweza kuthibitisha hili

Nikiwa Geita wanachama wa kundi la Masalia walikua wakinipigia simu mara kwa mara na hata Message za kunitaka nirudi Dar haraka hata kwa muda mfupi tu tuweke mipango ya kuanzisha kundi hili pamoja na kufungua bank account. Tarehe 01/05/2012 nilifika Dar es Salaam kikazi. Siku hiyo hiyo tulikutana na Habib mchange, Mtela Mwampamba, Juliana Shonza na Festo Sanga pale Lunch time hotel. Siku hii ndiyo niliyotambulishwa kwa Festo Sanga. Wote walikua na shauku ya kupata mawazo yangu kwa kuwa zitto alishawadokeza juu ya mkakati huu hasa baada ya kikao cha kamati kuu.Nadhani ilikua ni matokeo ya kikao cha kamati kuu na mambo yaliyotokea humo ambayo sitaki kuyaandika hapa kwa sababu ni siri za vikao.

Tulikubaliana katika kundi hili tuwe na mkakati wa siri na tukusanye fedha nje na ndani ya chama.suala la kukusanya fedha nje ya chama nililipinga sana.Nakumbuka Mchange ndiye aliyeleta wazo la kukusanya fedha nje ya chama.miongoni mwa walengwa walikua
-David Kafulila
-Mwigulu Nchemba
-Deo Filikunjombe
na baadhi ya wafanyabiashara

Draft niliyoandika ilionekana kuwa na ushawishi mkubwa kwa wale ambao walikua potential donors.

Pia Habibu Mchange alileta taarifa kwenye kikao kwamba Zitto amemwambia tuandae bajeti ya kundi hili. Zitto alisafiri siku hiyo bila kutuambia na tulilalmika sana sana. Baada ya hapo alikua akiwasiliana na mtu mmoja mmoja. Hata hivyo kwa kuwa ulikua mpango wa siri nilipendekeza tutumie code names au namba zilizochanganywa na herufi kama mbinu mojawapo ya kijasusi. Mwishowe kila mmoja alikubaliana tutumie tu majina kwa kuwa walihofia kusahau code names.tulibatizana majina na jina langu likawa COBRA, Mchange-Mdude, Shonza-Benazir, Mwampamba-Kony na code name ambayo tuliitumia kwa Zitto ni Prezzo au Dogo

Role yangu mimi ilikua katika fedha baada ya majadiliano kwa kuwa kila mjumbe alisema Ben ndiye tunayemuamini pekee katika usimaizi wa fedha na kubuni vyanzo vya fedha. Nilipewa kazi ya kuandaa bajeti.Lakini nilikataa kwa kuwa nilisema bado siridhishwi na mwenendo wa kukusanya fedha nje ya chama.

Shonza Alikuwa Mwenyekiti wa PM7 strategically ili awe na wajibu mkubwa kwa kuwa alikua kiongozi wa juu wa BAVICHA. Mchange alijichagulia kuwa makamu Mwenyekiti, Mwampamba Katibu, Festo Sanga alipewa kazi ya kuandika kwenye mitandao kwa kutumia ID ya TUNTEMEKE akisaidiana na mchange na Mwampamba. Tulikubaliana iwe taasisi kwa kundi lote la Masalia ili itumike panapolazimika. Sikuwahi kuitumia kwa kuwa niliwaambia nitaendelea kutumia ID yangu kwa kuwa siatamtukana mtu au kuzusha kitu hata kama michango yangu ingeniweka matatani

Hata hivyo baadae nilikubali na niliandaa bajeti ya Sh. 25,000,000 kwa awamu ya kwanza na tukachora ramani ya jinsi tutakavyogawana mikoa.

Lengo lilikua kuingia mikoani hata kwa lazima na kufanya mikutano ya hadhara na kujenga mtandao. PM7 ilikuja kubadilika na malengo yakawa too narrow kwa kuwa yalilenga kuimarisha kundi ndani ya chama. Badala ya Patriotic Movement ilikuja kuwa PINDUA MBOWE-7. Lengo hapa lilikua kumtenganisha mwenyekiti na Katibu mkuu ili kundi liweze kuimarika na kupenya kati kati. Hapa ndipo kazi ambayo ilikua imekwisha anza mwezi wa 4 katika kampeni za Arumeru Mashariki ya kumchafua Mbowe na Katibu mkuu kwa kutumia ID ya TUNTEMEKE iliposhamiri

Actually, niliona hatari ya kukichafua chama hasa tuhuma zilizokuwa ziktumika zilikua tuhuma za uongo na uzushi.Wakati tunafanya maandalizi ya kufungua akaunti benki, nilikutana na Dr. Kitila kwa haraka na kumweleza kama zitto au yeyote amemweleza kuhusu kundi hili. Alinijibu kwamba hana taarifa hizo.Hata hivyo tulikubaliana tukutane haraka na Zitto tuweke mikakati mipya kwa kuwa alishangaa ni kwa nini amewahusisha akina Mchange na Mwampamba huku akijua siyo watu makini katika strateggy na ni waropokaji. Aliniomba nifanye mpango wa kulivuruga kundi hili na Pm-7 ife taratibu. Baadae alinieleza kwamba tutapanga siku tutoke nje ya Dar mimi, yeye na zitto tuweke mikakati upya kwa kuwa hapa dar tulikua tunafuatiliwa sana sana. Nilifanikiwa katika mipango hii ya kuiua Pm-7 taratibu na hata wakati mwingine tuligombana sana na baadae kwenye kiakao karibu na Pacific hotel pale Manzese, Mchange na Mwampamba waliibuka na hoja kwamba kuna haja ya kwenda kula viapo kwa mganga ili tusisalitiane katika kazi hii pm-&. Kwa bahati nzuri shonza, Mimi naMwakajila tulipinga vikali upuuzi huu. Shonza hili unalijua na unajua ni kiasi gani nilikasirika siku hiyo. Uliniandikia Message na kunisihi tuendeleze kundi hili

Baada ya hapo wakati kikao cha bajeti kinaendelea Shonza na Mwampamba walinipigia simu kuhusu kikao cha dgharura na David Kafulila. Ilikuwa Tarehe 4/07/2012. Tulikutana Tamal Hotel. Kafulila alitudokeza juu ya kusajiliwa kwa chama cha CHAUMMA, tulijadili mambo mengi.Nilishirikishwa juu ya kujiunga na CHAUMMA na kuhakikisha kinasajiliwa rasmi kwa usajili wa kudumu. Kafulila alinisihi sana na kuniambia ndani ya CHADEMA yatanikuta yaliyomkuta yeye kwa hiyo tuungane. Nilimwambia nitafikiria. Hussein Bashe alikuja dakika za mwisho kwenye kiako kile. Yeye ni miongoni mwa mashuhuda. Kafulila aliniambia mzee Hashim Rungwe pia atajiunga na anafanya mawasiliano na Zitto. Tulipanga kukutana siku iliyofuata. Mwampamba alipewa kazi ya kuandika kwenye mitandao pamoja na Shonza. Siku hii mchange hakuwepo

Tarehe 7/07/2012 nilikuwa ndani ya Ofisi ya CHAUMMA. Nilitambulishwa kwa viongozi wote tukaweka mikakati. Mingine sitaiandika hapa kwa sasa. Walinipa kazi ya kuandika sera ya Vijana na sera ya mambo ya nje huku Kafulila akisema kwenye uchumi sera ya gesi atashirikiana na Zitto kwa kuwa wote wana utaalamu kutoka holand na Norway. Niliwakubalia kimkakati hasa nilipogundua wanapanga kupunguza kura za CHADEMA mwaka 2015 huku akiniahidi kwamba kundi kubwa litatoka CCM na CHADEMA baada ya chaguzi za ndani mwaka huu na mwaka ujao respectively. Aliniambia hata akina Hashim Rungwe wapo nyuma ya kundi hilo na vigogo wa CCM. Mliniambia CHAUMMA kitakua chama darasa. Kafulila anaweza kuthibitisha hili.

Katibu Mwenezi wa CHAUMMA ndg.Mawazo Athanas kutoka kigoma alinisihi sana nimsaidie na Zitto akiwa nje amemuhakikishia kwamba sisi tutamsaidia yaani masalia group au PM-7. Hapa Dr. Kitila mkumbo hakuhusika.Ikumbukwe Mawazo athanas alikua Mgombea Ubunge kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi huko kigoma na baada ya kuhama alitaka kujiunga na CHADEMA. Nilimshawishi sana ajiunge na CHADEMA lakini baadae nilimsikia yupo CHAUMMA. Nilikuwa nikifahamiana naye hapo kabla. Tuliendelea kuwasiliana nae kwa karibu na pia nikamuahidi Kafulila na uongozi wa juu wa CHAUMMA kwamba nitatoa ushirikiano ila waandae vitendea kazi. Nitaweka baadhi ya mawasiliano yetu hapa. Hata ID ya CHAUMMA hapa JF niliifungua mimi nikiwa ndani ya Ofisi za CHAUMMA na tulipeana Password. Kafulila alitaka nimpe paswd yeye, Katibu Mwenezi na katibu mkuu huku akiahidi kwamba atampa zitto itakapobidi. Alinisihi nisiwape akina Mchange na wengine kwa kuwa wanaweza kuharibu na kuonyesha wazi kwamba lengo la CHAUMMA ni kuigawa CHADEMA. Alitaka tuende kimya kimya. Akina Mchange na Mwampamba waliendelea kutumia ID Fake na ID ya TUNTEMEKE. Hii ni sehemu ndogo tu,sitaki kuharibu mambo mengi hapa hasa nyeti kwa kwa chama.

Nitaendelea....Nikihitajika nitakuja tena

attachment.php

attachment.php

 
Hahahhaaa hivi kumbe na wewe ulikuwa mgombea, kiswahili chenyewe ndio hiki?

Huwezi kujenga hoja mkuu wangu, mie sio mshabiki wa upande wowote but at least wenzako wanaelekea elekea, sijaelewa kabisa content ya thread yako, suala sio ugeni wako jamvini ila naona hata uelewa wako ni mdogo kidogo....

Nawashauri haya mambo kama mlivyokaa huko kwenye hizo hotel zenu basi itaneni mmalizane huko huko hapa mnatujazia server bure bhana
 
in your topic there is no any credible evidence or what so ever as claimed ... all the contents are null and void

rubish and childish post

you have wasted a batch of my brain memory space by reeding this literature full of cosmetics
 
Huu sasa ni utoto, yani uroho wa madaraka ya urais ndo ulete yote haya? Zito umepotoka na umekwisha kisiasa ,finaly mungu amewaumbua wanafiki ndan ya cdm
unasema utoto?Ukubwa ni kutumwa kumuua zitto
 
Wana jf ,Naomba mnielewe kwamba kutomuunga mkono mchungaji au padre mnafiki,mpika majungu,mfitini,anaendesha kanisa kwa maono ya hawara yake,mkabila,ndumilakuwili haimanishi kwamba nimelihasi kanisa,kanisa huendeshwa kwa maono ya biblia na mchungaji au padre anaweza anaweza potosha kondoo wake kama alivyofanya mchungaji kibwetele kwa kuwaangamiza kondoo wake waliokuwa wanamwaminia kuliko biblia

Hilo nalo neno!
 
Angalia hapo
"pia alitumia muda wake mwingi kunishawishi mimi nimkutanishe na zitto ili aweze kumsaidia ni jinsi gani atamsaidia katika kufanikisha mpango wake wa kutowaunga mkono mbowe na slaa".

SWALI
Kwa hiyo mpango wa ZZK wa kutowaunga mkono viongozi wengine nyie nyote mnaujua?.
Ili swala la Kuuwa kwa ZZK mbona controversial,mwenzenu ZZK amesema ameaga kwao na yeyote atakayethubutu hata panya hatabaki?, je mlitoa taarifa hata polisi,kwa viongozi kuwa mwenzenu anataka kuuwa.
Nikwambie tu ushauri wa bure na kundi lako ,sayansi ya vita hata mgambo wa aina mafunzo ya siku tatu anawashinda,Mko tu poor in every aspect of organization and determination.
Utetezi wako ndio unaweka mambo ya ZZK nje nje zaidi kweupe usaliti wake wa kulea na kufuga mamluki.
 
Nishawahi kusema siku moja kuwa…most of the young politicians have inner political torture.

Mamuya, Zitto, Ben Saanane, Mchange and the like saga is one of the evidences. The agony has reached a point where the patients cannot resist inner political healing. In other words the conflict is at the climax where both sides would opt for a round table.

Taking the patients to disgrace might not be a proper approache, though it can cause conflict resolution experts (like Prof, Baregu) to intervene.
Chadema kama taasisi inayojiandaa kuchukua dora kutoka kwa watu ambao wasingependa kuiachia lazima ipitie haya yote. Usaliti ulikuwepo hata wakati wa Yesu na aliwafahamu.

Bahati mbaya wao (wasaliti) hawakujifahamu. Wote walijiona wako sawa. Mamuya, Zitto, Ben Saanane, Mchange, Dkt. Kitila Mkumbo na wenzao, wote ni wanachadema.

Ni wakati wa chadema kama shina la mti ikusanye matawi yake pamoja, na matawi yakusanye vijitawi vyake wakae pamoja na kujitambua kuwa wao ni mti mmoja.
 
Mfyuuu! Naona umepanga maneno bila mtiririko wa kueleweka,usitoche na miparagraph isiyokuwa na mantiki yoyote'wanafiki wakubwa nyie na Mungu kawaumbua.
 
tumechoka! this is not a right place now>>> nenden kwenye vikao vya chama jamani!!!!
Yani imekuwa kama Hadija kopa na Nasma Kadogoo R>I>P.
Siasa haiendi hivi Nyie Vijana.
Dr Slaa na Mw Kit. Please hawa Vijana waiteni muwaonye, Huu upuuzi wa maneno ya khanga hatutaki humu jamiii.
hapa wasira na Nape wanachekelea tu, wanapata vyakuongea majukwaani.
 
Back
Top Bottom