UTEUZI: Rais Samia amteua Jenerali Venance Mabeyo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro

In less than 24 tokea amestaafu kashapewa ajira nyingine, kwa style hii vijana watasubiri sana, chifu kaamua kutumia mjeshi kuzima sakata la loliondo
 
Tatizo la ajira linahusishwa katika uteuzi kwann? Mtu anaandika vijana hawatapata ajira........
Hata Mabeyo kuna siku aliingia jeshini kama kijana aliyepata ajira mpya.

Mabeyo alipotoka ameshika Mkunda, naye aliingia hapo bila kuwa na cheo chochote, kazi yoyote na bila uzoefu wowote na leo kaachiwa nafasi.

Sasa hiyo nafasi alitakiwa apewe graduate au nini kilitakiwa ili kusiwe na malalamiko ya ajira? Huwezi kumpa mtu asiye na uzoefu na haaminiki nafasi nyeti. HAIWEZEKANI. Yaani kijana umetoka chuo cha misitu huko puuu wewe ni mkurugenzi mpya bodi ya utalii?

Kuna siku Mabeyo atampisha mwingine hiyo nafasi mpya aliyopewa, na huyo mwingine huenda sasa hivi anapata uzoefu wa kazi sehemu fulani baada ya kuajiriwa huko nyuma akiwa fresh bila uzoefu.

Kila wakati kuna vijana wapya wanaingia jeshini. Hao ni Macdf wajao, wakuu wa vikosi wajao na kuna siku watapewa nafasi za ukurugenzi, ubalozi n.k

HAKUNA UHUSIANO WA UKOSEFU WA AJIRA NA NAFASI ZA UTEUZI SABABU KILA CHEO KIPYA NI FURSA MPYA KWA MWINGINE KUPATA NAFASI ILIYOACHWA NA ALIYEPEWA CHEO KIPYA.
 
Lazima amshukuru. Mwaka 2020 jeshi lilihusika kikamilifu kwenye wizi wa kura. CCM oyee.
 
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania mstaafu, Jenerali Venance Mabeyo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA).

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais- Ikulu imesema kuwa uteuzi huo umeanzia leo Alhamisi Juni 30, 2022.

Uteuzi huo umekuja muda mfupi baada ya Mkuu huyo wa nchi kumuapisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) mpya, Jenerali Jacob Mkunda.

Wakati wa uapisho huo uliofanyika Ikulu ya Dar es Salaam, Rais Samia ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu alimshukuru huku akiahidi kumpangia majukumu mengine Mabeyo.

“Namshukuru Mungu kwa kumjalia Jenerali Mabeyo kumaliza kazi leo akiwa smart na bado ana nguvu. Nikushukuru Jenerali Mabeyo kwa kazi nzuri uliyofanya katika utumishi wako wa zaidi ya miaka 40 jeshini.
“Umefanya kazi yako kwa uadilifu mkubwa, umetumikia cheo chako kwa jitihada kubwa na umemaliza na kukabidhi kwa wengine.

Tunakushukuru sana na tunakupongeza sana kwa sababu siyo kazi rahisi,” amesema Rais Samia.

Mkuu huyo wa nchi aliahidi kuwa wataendelea kumteua katika majukumu mengine huku akisisitiza kwamba tayari Katibu Mkuu Kiongozi, Hussein Kattanga ameshampangia majukumu mengine.

“Unaacha ukiwa na nguvu, ukiwa bado kijana na kwa hiyo tutaendelea kukuteua, tutaendelea kukupa majukumu, uendelee kutusaidia.

“Nadhani jioni ya leo Katibu Mkuu Kiongozi atasikia kwenye bomba, tayari ameshakupangia kazi ya kufanya. Kwa hiyo tunakushukuru sana na tunakupongeza na tunakuomba bado uendelee kulitumikia taifa lako,” amesema Rais Samia.

Source: Mwananchi
 
Mwenye nacho ndiye huwa anaongezewa!
Shida iko kwenye process ya kufikia kuwa nacho.Kapitia magumu mengi hadi kufika hapo kuwa nacho

Hiyo process maskini wengi huishia tu kupiga yowe ohh mwenye nacho ataongezewa
 
OK kwa hiyo ulisema Ngorongoro wanyama wamepigwa risasi au vipi! Au hukusema ?

FWhbtBlXkAAzWto.jpeg
 
Back
Top Bottom