Utekelezaji wa kutangaza mali za viongozi wa umma

nataka muelewe kuwa watanzania wengi esp viongozi pesa wanazo lakini wanaogopa kuwekeza kwa sababu ya vidole...na hizi ni pesa zetu ...tusipowaruhusu watazitawanya ...angalia hili ujue kuwa tanzania watu wana pesa ...mwaka juzi kulikuja mfuko wa UMOJA TRUST huu mfuko wa uwekezaji uliweza kuingiza shilingi BILLION 100 ndani ya miezi miwili ,,,just kutoka kwa wananchi,,,NICO walipatA BILIONI22 ..TCCIA WALIKUSANYA BILIONI 9....TWIGA CEMENT bilioni 75...ZOTE HIZI ZIMETOKA KWA WANANCHI WENYE kiu ya kuwekeza ,,,but you know what ..kiuchumi ina maana watanzania wengi hasa hawa mabosi wanazo pesa nyigi hawajui wafanyie nini...sio ufahari kuwa na milioni 600 kwenye akauti ya akiba wakati ,kuna mtu mjasiriamali akipata milioni anajikwamua na anakuwa miliomia baada ya mwaka...mimi binafsi nilishuhudia mzee mmoja aliyekuwa na nafasi zamani akinunua hisa za umoja za milioni 300 peke yake...hii pia ina maana watanzania wangehamasishwa na hawa viongozi kama si kuogopa wana uwezo wa kununua makampuni mengi tu yaliyouzwa na tusingehitaji wazungu ,,,we could just hire there management to run our industries wich could be whole owned by wazawa....so tuache unafiki ...kama kuna kiongozi ana pesa ameficha azitoe tu aingize kwenye uchumi...na PALE anapozitoa tusianze kelele...nchi yoyote inayotoka kwenye uchumi wa kijamaa inaweza kuopata wazawa kumiliki uchumi kutoka kwa WAZAWA MAFISADI.. sasa mkiaza kuwauliza walipata wapi itabidi mkubali kuwa na wawekezaji wa NJE..hapa nitawapa mfano wa russia namana ilivyopata mamilionia wazawa kwa kuwauzia wazawa waliokuwa na nafasi au channel makampuni yao hasa ya mafuta ili tu wasimilikiwe na wageni...
nyerere alisema ni "BORA KABURU MWEUSI"
 
Mzee Lunyungu hakuna sheria yoyote ya kuwabana, kwa sababu walikuwa wakibanwa na Azimio La Arusha tu, lilipokufa tu basi, leo ni mpaka kiongozi akamatwe kama Mahalu , na ushahidi at hand otherwise ni waste of time kutangaza mali!

Kwa mfano inafahamika wazi kuwa BM alipoingia madarakani yaaani urais hakuwa na mali kama aliyokuwa nayo mwishoni, yes hapo unaweza kupitsha uchunguzi maana kuna rais mpya na record zitakuwepo tu, maana hata za Mahalu Muuugwana alizikuta Ikulu kwa bahati mbaya alizisahau aliyeondoka!
 
Phillemon Mikael,
Ndugu yangu, ndugu yangu. Kusema kweli nimeshindwa kabisa kukuelewa!

Kila naposoma mchango wako huu (nimerudia mara tatu) inaonyesha wazi kwamba umekubali kuwepo kwa rushwa isipokuwa tatizo ni ktk matumizi ya fedha zilizoibiwa.

sasa na kuruhusu wizi na uuzaji unga ikiwa kuna malengo mazuri ya ku-invest ndani. Moi na viongozi wote wakiafrika ni majambazi wakubwa sana sawa kabisa na Alex Massawe isipokuwa tofauti ni vifaa wanavyotumia.

Tumekuzwa ktk mazingira ya KUOGOPA mwenye fedha na KIONGOZI. Hofu ambayo ilimpa Mkoloni nguvu ya kututawala kwa zaidi ya karne nzima, still leo bado wapo watu wanaopendelea utawala ule...

Bianfsi nakubaliana na wenzangu hapo juu kwamba kutangaza mali za viongozi ni sawa na mwanamke wa uswahilini mvaa baibui... danganya macho kwa wananchi kwa sababu viongozi wetu wanaruhusiwa kuendesha biashara zao tena wakati mbaya wa mageuzi ya kiuchumi.

Kama alivyosema Mzee ES, sii rahisi kufahamu mali za kiongozi ikiwa kiongozi huyo ameshiriki kuiuza kampuni na share yake inakwenda moja kwa moja ktk ununuzi wa hisa na other investment.

Leo hii JK na Mkapa wakiwa na share za ndani ya Barrick ama Tanzania Royalty exploration hakuna kati yetu anayeweza kufahamu utajiri wa watu hawa zaidi ya kuhesabu nyumba alizojenga pia wake wangapi wa nje. Huu ndio Utajiri wa mwafrika unaohesabiika kutokana na dhana ya Kijamaa, kumbe kiongozi anaweza kuwa tajiri mkubwa nje na ndani bila kuwa na mali chini ya jina lake. Na hakuna sheria inayotaka viongozi kuorodhesha majina ya makampuni zote ndani na nje ili tume inayoshughulika na ukaguzi wa report hizo waweza ku verify kilichokuwa claimed...

Zoezi hili ni upotezaji wa fedha za umma kwa sababu sielewi kabisa nini lengo lake!..Haiingii akilini kabisa!...
 
Mswahili

Tufafanulie hili wengine hatulijui. Mwaga vitu manaake wanaobeba pesa nyumbani in those terms in London kutoka Africa ni Nigerians.
 
Sumaye alipoona anaondoka aka team up na nigerians wakaunda NGO inaitwa regional africa lakini ni pesa za sumaye katumia ujanja kuzificha.

Na juzi wameenda Dubai na hao wa-Nigeria.
 
Last edited by a moderator:
Ili kuthibiti viongozi ku-abuse madaraka yao kwa kujinufaisha binafsi, ni lazima wataje mali zao kabla ya kuingia madarakani na baada ya kuondoka madarakani. Marekani ambayo ndiyo baba wa ubepari wanafanya hivyo iweje sisi tusifanye wakati tuna ubepari uchwara tu. Mkapa aliingia madarakani na kutuambia kuwa ana magari mawili, moja alilipata kutokana na nafasi yake ya ubunge na jingine la familia yake, nyumba moja Masasi na nyumba nyingine nadhani Kiluvya au Mbezi. Alipoondoka hakusema alijirundikia mali kiasi gani. Siri hiyo ndyo inasababisha watu wawe na wasiwasi na ushiriki wake katika mikataba ambayo baadaye imeonekana kuwa mzigo mkubwa kwa Taifa. Kama angetaja mali zake hadharani bila kuficha chochote, inawezakana watu wasingekuwa wanamnyooshea vidole kama ilivyo sasa hivi. Ingekuwa inasiadia pia kwa wananchi kuwa na imani na viongozi wao.
 
Jamani Serikali ya CCM hatab sijui tuseme nini . Huwa nachoka sana wakati mwingine kwa maneno , tabia zao hawa jamaa then tunaambiwa Chama kina sera nzuri za kuvutia watu wakuhamia huko ?
 
Jamani Serikali ya CCM hatab sijui tuseme nini . Huwa nachoka sana wakati mwingine kwa maneno , tabia zao hawa jamaa then tunaambiwa Chama kina sera nzuri za kuvutia watu wakuhamia huko ?


Yup...kama chama ni sera ccm wana sera nzuri kuliko vyama vyote....Tatizo WATU wenye UZALENDO hawapo tena CCM na pengine hawamo kwenye vyama kabisa.
 
Tabia ya viongozi kujilimbikizia mali inaangamiza taifa!
Na Profesa Leonard K. Shayo

WAAFRIKA, kwa vizazi na vizazi, tutawakumbuka viongozi waadilifu, kama Nelson Mandela na hayati baba wa taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ambao hawakujilimbikizia mali za kukifu wakati wa utumishi wao kwa umma! Tabia ya kujilimbikizia mali halali, ni sehemu ya maumbile ya binadamu, na ni kichocheo kikubwa cha maendeleo!

Tunahoji kwamba, hata maarifa ni mali, na kwa maana hiyo, yale maagizo, kwenye vitabu vitakatifu, kwa mwanadamu kutafuta maarifa, kwa nguvu zake zote, ni amri ya kujilimbikizia mali! Ndiyo maana hatupingi utajiri uliopatikana kihalali, lakini tunapinga kujilimbikizia mali za kukifu! Hakuna njia halali za kumlimbikizia kiongozi mali za kukifu!

Jamii za nchi maskini, kama Tanzania, haziwezi kukwepa lawama ya kushiriki katika kukuza tabia ya viongozi wao kujilimbikizia mali za kukifu! Jamii zinashiriki kwa namna nyingi, zikiwemo zifuatazo nne! Kwanza ni kwa kutoa ulinzi nusu kwa viongozi wao! Badala ya kulinda mwili na akili ya kiongozi, kama inavyotakiwa, zinalinda mwili peke yake! Kwa mfano, kiongozi anayeshutumiwa kwa ufisadi, hata baada ya kuachia madaraka, anaumia akili! Je, ni kwa nini vyombo vya usalama visilinde pia akili ya kiongozi huyo kwa kufungua mashtaka dhidi ya waliotoa shutuma? Kwa kuzingatia kwamba, madhara ya akili ni hatari kuliko madhara ya mwili, ni unafiki kuulinda mwili wa kiongozi bila kulinda pia akili yake! Ni unafiki pia kwa ulinzi wa viongozi kudharau haki za watoa shutuma, na haki za umma kupata majibu ya shutuma dhidi ya viongozi wao!

Njia ya pili ya jamii kushiriki katika ufisadi wa viongozi, ni kwa kurubuniwa na mchanganyiko wa umaskini na ujinga! Maskini asiye mjinga hawezi kuuza kura yake kwa gharama yoyote! Je, ni mara ngapi tumesikia malalamiko ya kura kuuzwa kwa gharama ya chakula cha siku moja, ama nguo ya mvao mmoja, katika nchi kadhaa za kiafrika? Yaani jamii inawachagua viongozi wafisadi baada ya kupewa rushwa ya kukashifu utu!

Umaskini na ujinga vinachangia pia katika ujenzi wa tabia ya kusahau majeraha makubwa, ya muda mrefu, katika kipindi kifupi! Vinachangia katika ujenzi wa falsafa ya “hatutakuwepo watajiju”! Vinachangia katika ujenzi wa tabaka la wananchi wanaoishi kwa kujali leo, yaani bila kuongozwa na historia ya jana, na bila kuchukua tahadhari ya kuzuia dhoruba ya kesho! Je, nyimbo za amani na utulivu, katika nchi zenye utajiri unaoporwa kila kukicha na wageni, sambamba na ufisadi uliokidhiri miongoni mwa viongozi, na sambamba na umaskini wa kutupa miongoni mwa wananchi wengi, zinaweza kuashiria kuwepo kwa wajanja wengi?

Njia ya tatu ya jamii kushiriki katika ufisadi wa viongozi ni kwa kuwashawishi! Kama ilivyo kwa rushwa, kiongozi anaweza kuingia madarakani akiwa safi, lakini akashawishiwa na jamii, inayonuka rushwa, kujilimbikizia mali haram! Siyo siri kwamba, katika jamii inayonuka rushwa, mteja anaweza kutoa rushwa bila kuombwa! Wateja jeuri wanaweza pia kumweka kiongozi njia panda, yenye maamuzi mawili, moja ya kupokea rushwa, na nyingine ya kupata madhara makali!

Ipo hadithi ya kiongozi wa mkoa, katika nchi moja, aliyeingia madarakani na kiapo binafsi cha kupiga vita biashara haram za magendo, lakini akaingia kilaini katika mtego wa walanguzi! Kama ilivyo kwa wafanyakazi waadilifu wa nchi maskini, kiongozi huyo alianza kazi akiwa anaishi maisha ya kawaida, na aliipenda sana familia yake! Siku moja walanguzi wakafika nyumbani kwake, baada ya yeye kwenda kazini, wakiwa na lori lililojaa bidhaa nyingi za matumizi ya nyumbani! Walimwambia mke wa kiongozi huyo kwamba, baba mwenye nyumba amewaagiza walete bidhaa zile nyumbani, na kwa furaha kubwa, zilipokelewa na kupangwa katika kila chumba! Kwa kweli nyumba ile ilibadilika, na kiongozi huyo aliporudi nyumbani, alipokelewa kama mfalme! Alishikwa na butwaa, kiasi cha kutaka kuzitupa bidhaa zile, lakini alipigwa “stop” na mapokezi aliyopewa na mke wake, pamoja na furaha iliyotanda kwenye nyuso za watoto wake! Msumari wa mwisho ulikuwa ni simu kutoka kwa walanguzi, wakimuuliza “mzee umepata mzigo wako? Mbele ya familia yake, ilibidi ajibu “ndiyo, ahsante”! Huu ukawa ndiyo mwisho wa kupambana na walanguzi kwa ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya, kwa mwelekeo wa ushindi! Tuliwahi kunena kwamba, viongozi katika nchi zote, huingia madarakani na ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya! Tofauti kati ya kiongozi mmoja na mwingine, ni mwelekeo wa upya huo!

Njia ya nne ya jamii kushiriki katika ufisadi wa viongozi, ni kwa viongozi wapya kulinda ufisadi wa viongozi wa zamani, katika kuheshimu falsafa ya ``uwenzetu”! Pamoja na ukweli kwamba, zinaweza kujengwa hoja za kufumbia macho ufisadi wa viongozi, ni vema hoja hizo zikazingatia madhara ya kufanya hivyo, hasa kwa vizazi vijavyo! Kwa mfano, ufisadi unaotokana na rushwa ama wizi wa ndani kwa ndani, una madhara yanayoweza kufumbiwa macho! Lakini madhara ya ufisadi unaotokana na rushwa za kimataifa, ni makubwa, na ya hatari kwa usalama wa taifa! Siyo busara kufumbia macho ufisadi wa aina hiyo, maana ni wa kuuza nchi!

Dunia imekuwa ndogo, kiasi cha kuyalazimisha mataifa tajiri, kama Marekani, kutumia fedha nyingi kusafiri anga za juu, kwa ajili ya kutafuta sayari inayofaa kwa maisha ya binadamu! Je, ni kwa nini tunakuwa na vichwa vigumu kuelewa kwamba, iwapo tutayapa mataifa hayo nafasi, yatavamia nchi zetu kisayansi? Mbona vita vya mafuta vimeshaonyesha jinsi sayansi inavyoweza kutumiwa vibaya? Je, umaskini na ujinga vinaweza kuwa vimechangia katika ukimya wa nchi maskini kukemea matumizi mabaya ya sayansi? Kwa kuzingatia hali halisi ya siasa za ulaghai duniani, tunatoa wito kwa viongozi wa nchi maskini, na hasa viongozi wa Tanzania, kutumia hekima katika maamuzi ya kufumbia macho ufisadi, na hasa ule wa kimataifa!

Ufisadi wa ndani unaonuka ulafi, ni hatari pia kama wa kimataifa! Tunasema hivyo kwa sababu, kama ukifumbiwa macho, utafunga mikono ya viongozi wa leo na wa kesho! Utatoa baraka ya wenye hulka ya ulafi kuwania uongozi na kupokea rushwa za kimataifa! Falsafa ya maamuzi ya kesi jana, kutumika kama utetezi wa kesi kesho, ni moja ya nguzo muhimu katika sheria na mahakama! Kwa maana hiyo, hatua ya viongozi wa leo kufumbia macho ufisadi wa viongozi wa jana, na hasa wa ulafi, ni hatua ya kuruhusu ufisadi wa leo, na ufisadi wa kesho! Kwa upande wa Tanzania, kwa mfano, tumesoma na kusikia shutuma nyingi za ufisadi wa ulafi! Je, akili za watuhumiwa zitalindwa kwa kesi kufunguliwa mahakamani ili waliotoa shutuma wapate haki ya kuzitetea? Je, kesi zitafunguliwa mahakamani ili watuhumiwa wapate haki ya kuishi kwa amani na utulivu? Je, kesi zitafunguliwa mahakamani ili kutoa fundisho kwa viongozi watarajiwa?

Wananchi wa nchi yoyote, wana haki ya kutilia mashaka maamuzi yote yenye utata, yaliyofanywa na kiongozi mkuu wa nchi, baada ya shutuma nzito za ufisadi dhidi yake kuwekwa hadharani! Kwa upande wa Tanzania, kumekuwepo malalamiko mengi ya kupinga utekelezaji wa sera ya ubinafsishaji na ugenishaji wa rasilimali zetu! Je, ni kwa nini usifanyike utafiti, wa kina, wa kubaini wamiliki halali wa mashirika mapya, na mashirika yaliyobinafsishwa, yakiwemo maduka, mahoteli, mashamba, mabenki, viwanda na migodi? Utafiti huu ni muhimu kwa ajili ya kujenga hazina ya viongozi wa kesho! Nchi itadidimia katika dimbwi la ufisadi, na umaskini wa kutupa, kama tutafanya makosa ya kuchagua viongozi walafi! Ni vema tutambue kwamba, licha ya utajiri wa kukifu, nchi kubwa kama Marekani zina utaratibu wa kuwapiga “stop” wananchi, wenye hulka ya ufisadi, kuwania nafasi za uongozi! Kwa mfano, kosa la kukwepa kodi ya mwezi mmoja linatosha kumnyima muhusika haki ya kuwania urais wa nchi hiyo!

Tunawaasa viongozi wasikie vilio vya wananchi na kuvifanyia kazi! Tunasema hivyo kwa sababu, vilio hivi ni matokeo ya maono ya macho mengi! Kwa mfano, wananchi wengi tulilia wakati wa ugenishaji wa shirika la umeme (TANESCO), na tulilia wakati wa ubinafsishaji wa Benki ya taifa ya Biashara (NBC)! Hivi karibuni kulikuwa pia na vilio wakati wa kukaribisha wawekezaji katika uzalishaji wa umeme, kutumia majenereta! Je, viongozi wa leo hawajapata fundisho?

Macho ya wananchi ni kioo cha viongozi! Kwa maana hiyo, ni udhaifu wa aina yake kwa kiongozi kukemea tuhuma, badala ya kutafuta haki mahakamani! Je, ni hekima kukemea hata matokeo ya tafiti za wataalam?

Mobile: 0754 288 179 E-mail: shayolk@yahoo.co.uk.
 
Je, kuna mali mpya za viongozi zilizoripotiwa baada ya matukio ya hivi karibuni yaliyohusisha mabilioni ya fedha za wananchi/
 
Jamani, naona hapa mada ni nzuri lakini maneno maneno yamekua mengi na hakuna anayetaja mali. KWa wale wanaosema uhalali wa kumiliki mali wa viongozi, wana haki yakusema yaho na ni sahihi kabisa wanayoyasema, ila kwa kuanika hapa, inatoa nafasi kwa watu kujadili na kuona kama kweli mali hizo ni halali? Je, zinalingana na nyadhifa zao? Je, Baba wa Taifa Mwalimu J.K. Nyerere alikua na mali kama hizo, je, watoto wake wana maisha gani hadi leo? TUSISITE KUWEKA HAPA MALI then ndio tuzijadili na kuwapa nafasi waandishi kufuatilia
 
Jamani tunaomba kutajwa mali za hawa Watawala maneno yasiwe mengi wakubwa.Haya shime!
 
wanaJF kampeni hii ya kuweka picha kwa kutumia CAMERA-SIMU kwa mali za vigogo ili tujuwe viongozi wetu wanamiliki mali za aina gani bila kuwazushia, topick hii itakuwa sehemu ya kuorozesha mali zote za vigogo wakiwa wale waliyo chuma BoT, Mikataba Mibovu- RADA, NDEGE YA RAIS,MADINI,RICHMOND,TRA, Halimashauri za wilaya, Vijiji, Misaada, Serikali Kuu,Mashule,NGO'S na sehemu nyingine,
 
Dar es Salaama kuna hospitali moja inaitwa Tumaini. Siku hizi mgonjwa akienda Muhimbili, madaktari humwambia akachukue vipimo huko Tumaini. Bei ya kipimo kimoja kinaanzia laki moja na nusu hadi milioni moja na nusu. Watu wengi waliotumwa kwenda kuchukuliwa vipimo vyao huko Tumaini wamekuwa wanakutana na waganga wale wale waliowatuma kwenda hapo kutoka Muhimbili ndio wakiwachukua vipimo hivyo hivyo kwa vifaa kama vilivyoko muhimbili. Kulikoni Muhimbili na Tumaini?

Naona kama hapa nchi inaingia kwenye crisis fulani kuhusu huduma za afya endapo hosptiali ya rufaa inatumiwa kama chambo cha kupata wateja kwenda huko Tumaini Hospital kwa nguvu za madaktari. Je serikali imeanza kuitelekza Muhimbili kusudi baadaye nayo ije ibinafsishwe?
 
Hii ni kashfa,uchafu kama huu upo kwenye hospitali kibao za serikali,lakini nani wa kulaumiwa,serikali au madaktari?Fikiria hawa madaktari wanapiga msuli miaka 5 hadi saba kupata hizo fani zao,halafu wanaambulia kulipwa laki mbili,sasa kwa nini wasianzishe hospitali binafsi ili wawakamue walala hoi,tena hizo hospitali binafsi zina huduma nzuri maana ni biashara.
 
Hii ni kashfa,uchafu kama huu upo kwenye hospitali kibao za serikali,lakini nani wa kulaumiwa,serikali au madaktari?Fikiria hawa madaktari wanapiga msuli miaka 5 hadi saba kupata hizo fani zao,halafu wanaambulia kulipwa laki mbili,sasa kwa nini wasianzishe hospitali binafsi ili wawakamue walala hoi,tena hizo hospitali binafsi zina huduma nzuri maana ni biashara.

Ninaelewa unaloongea, lakini si ni afadhali wakaondoka kwenda kufanya bishara zao huko Tumaini kuliko kukaa pale Muhimbili kama waganga kumbe siyo. Inasababisha hospitali ineokane ina waganya kumbe ni wao ni mawakala wa Tumaini.
 
Tumaini hospital ina uhusiano wowote na chuo cha tumaini moro ? if so, kile chuo cha tumaini ni cha kikristo kwa ufahamu wangu !
 
Back
Top Bottom