Utekelezaji wa kutangaza mali za viongozi wa umma

kwa ufahamu wangu, Tumaini Hospital inamilikiwa na umoja wa madaktari, wengi wao wako muhimbili.
 
Tumaini hospital haina uhusiano wowote na tumaini university, madaktari wajasiliamali walikuna na kuanzisha hospitali hiyo, na kumbuka wakati wa kuanzishwa kulikuwa na zogo kweli kweli kuhusu confilict of interest lakini wajasiliamali wakashinda,hata upatikanaji wa lile jengo ilikuwa ni shughuli pevu
 
ok, great ! lakini kama hospitali kama wengi tunavyofahamu ni jambo jema, sidhani kama kulikuwa na nia ya kuwekewa zongo achilia mbali na shortages za hospitali tanzania. nadhani ni sheria/taratibu pengine hazikuwa met, either way its good to see they ended up in a good place ! tumaini hospital.
 
Tumaini hospital ina uhusiano wowote na chuo cha tumaini moro ? if so, kile chuo cha tumaini ni cha kikristo kwa ufahamu wangu !

Tumaini ni chuo KIkuu na sio chuo cha kikristo. Tafadhali chunga sana unachoandika au unataka ministry zisitoe huduma hapa tanzania? Nilikuwa nakueshimu sana!
 
Ubaya siyo kuwepo kwa hosptiali ya Tumaini. Ubaya ni kuwa waganga wa muhimbili wanawanyima huduma wagonjwa na kuwanalazimisha waende Tumaini Hospital hata kama hakuna haja ya kufanya hivyo.
 
Ubaya siyo kuwepo kwa hosptiali ya Tumaini. Ubaya ni kuwa waganga wa muhimbili wanawanyima huduma wagonjwa na kuwanalazimisha waende Tumaini Hospital hata kama hakuna haja ya kufanya hivyo.

pengine wanafanya hivyo kwa sababu ile ile iliyowafanya wafanya strike kipindi kile jk ndio kwanza anaingia madarakani ! service first then comes the money, lakini nchini kwetu ni vice versa yake !
 
Tumaini ni chuo KIkuu na sio chuo cha kikristo. Tafadhali chunga sana unachoandika au unataka ministry zisitoe huduma hapa tanzania? Nilikuwa nakueshimu sana!

... msamehe ndugu yangu mara nyingi ulimi huteleza sembuse typing...

Ila nadhani Tumaini kama haina uhusiano na kigogo fulani basi itakuwa ni hospitali yenye wabia ambao ni watendaji kutoka hospitali za serikali...
 
..inaendeshwa na madaktari bingwa["wazalendo"] wenye chama chao waliopo nchini,hasa dar!

..hivyo basi wengi watakuwa wanatoka mnh!

..yawezekana huo umoja ndo unaomiliki hiyo hospitali.
 
Jamani am still dealing with the Tumaini issue maana ndiyo source ya mtoto kutoka Lindi kutelekezwa. Ni kweli kuna very senior doctors wanatoka Muhimbili ndiyo mradi wao pale .Lakini kibaya ni kwamba Patients are forced to undergo tests from Tumaini hata kama it is possible kwa Muhimbili . Hii ni mbaya sana na walalaho wanaumia na kujengewa chuki mara matokeo yakiwa vinginevyo na washinda hoi wale kudai pesa zao. Mfano ni wa huyu Mama toka Lindi na mwanae ambaye sasa kaanza kupewa matibabu lakini mwanzoni alichezewa na hata pesa yake kumfanya achukiwe . Yaani hawa jamaa wa Tumaini wao ni pesa mbele na huduma na utu baadaye.
 
hau kwa sababu ipo karibu na muhimbili ndio maana wanaambiwa kwenda pale.ukiangalia ma dr hao hao ndio utawakuta aga khan,hindumandal,na ile nyingine ya mikocheni.
 
TUMAINI UNIVERSITY

IRINGA UNIVERSITY COLLEGE

An Institution of higher education organised under the Evangelical Lutheran Church of Tanzania (ELCT)


UNIVERSITY TRAINING FOR FUTURE LEADERS

ACCREDITATION

Tumaini University, Iringa University College holds a Certificate of Full Registration from the Higher Education and Accreditation Council (HEAC).
 
Tumaini University, Iringa University College was founded as "Lutheran College at Iringa," a Lutheran Seminary, in 1993. A Bachelor of Business Administration began in 1995, followed by Bachelor of Arts (Journalism) in 1997, Bachelor of Law in 1998, and Bachelor of Education (Mathematics) in 2001. In 1995, Tumaini University, Iringa University College became the first private institution in Tanzania to offer a Bachelors Degree in 1995
 
tumaini hospital wakubwa ni mradi wa madoctor wa muhumbili,so ni lazima wawalete wagonjwa tumain ili nao wapate chochote kitu,MWAKYUSSAH NA AISHA KIGODA MNAFANYA NINI?ni ubadhilifu wa hali ya juu huu
 
wanahitaji wawajibishwe hawa walanguzi mana wanatunyonya sisi watu wa kipato cha chini,kutoa laki moja kwa kipimo si mchezo wakubwa...
 
Who cares, viongozi watibiwa nje. Licha ya kuwa bei za nje ni hata mara kumi za hizo lakini ni sisi wenyewe tumewapa 'uheshimiwa'. Mwalalamika nini, kila mtu kivyake vyake, hiyo ndio TZ.
 
Who cares, viongozi watibiwa nje. Licha ya kuwa bei za nje ni hata mara kumi za hizo lakini ni sisi wenyewe tumewapa 'uheshimiwa'. Mwalalamika nini, kila mtu kivyake vyake, hiyo ndio TZ.

............(TZ) ya siku hizi.
 
Posted Date::9/18/2007
Viongozi wa umma sasa kutaja mali za watoto, wake zao
Aziza Nangwa na Irene Lipende
Mwananchi


SERIKALI imeazimia kuifanyia marekebisho Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ili kuondoa mapungufu yaliyoko kwenye sheria hiyo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Philipo Marmo, alieleza hayo alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, jijini Dar es Salaam jana.

Alisema serikali imeamua kubadilisha sheria hiyo ili kuweza kuwaingiza viongozi wengi zaidi kwenye hatua ya kukaguliwa mali zao wakiwemo maofisa wa polisi wa wilaya na viongozi wengine waandamizi, ili kuziba mianya ya viongozi kujilimbikizia mali kwa njia zisizo halali

Aliongeza kusema kuwa fomu za kuorodheshea mali za viongozi, pia zitafanyiwa marekebisho kwa kuongeza kipengele cha kuwataka viongozi hao wataje mali za watoto na wake zao, ili kudhibiti udanganyifu unaoweza kufanywa.

Hata hivyo, Marmo, alifafanua kuwa kiongozi yeyote aliye madarakani hakatazwi kuwa na mali ili mradi tu mali hizo ziwe zimepatikana kihalali na zinatambulika kisheria.

Alisema zoezi la kukagua mali za viongozi linaendelea na kwamba hadi sasa theluthi ya viongozi wote wameshahakikiwa mali zao.

Naye Kamishna Mkuu wa Sekretarieti hiyo, Jaji Stephen Kihema, alisema mwezi huu na ujao wataendela kuhakiki mali za viongozi wengine 300 waliobaki zikipatikana fedha za kutosha.

Hata hivyo, Marmo aliwaonya wanasiasa kuache kutumia majukwaa ya siasa kuwakashifu viongozi wengine kwa tuhuma mbalimbali za ubadhilifu, badala yake waende kwenye vyombo vya sheria kupeleka malalamiko yao.
 
Back
Top Bottom