Utekelezaji wa kutangaza mali za viongozi wa umma

Majipu yote yatakapoiva yatatumbuliwa a la yatatumbuka yenyewe. There is no worry to the need with regards to ufisadi. Ufisadi ni dhambi mbaya kuliko kula nyama ya mtu kwani kula nyama ya mtu kuna kipindi utashiba au kukosa wa kula BUT ufisadi is deadly.

My mother's common saying when is not sure of what is going to happen used to tell me "Just wait and see"
 
Ndugu zangu, kama nakumbuka vyema "Kingpin Mkapa" alianzisha utaratibu wa kutangaza mali za viongozi wa serikali - kupitia Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Hivi karibuni tumeshuhudia Yona, Mramba na Mgonja wakijiwekea dhamana kwa kutumia baadhi ya mali zisizohamishika, zenye thamani kubwa ya fedha - mabilioni.Hawa viongozi hawana background ya biashara, ni kweli kwa savings za allowance za serikalini wameweza kukusanya utajiri mkubwa kiasi hicho?

Hivi kweli hawa binadamu walafi, waliandikisha hizo mali kwenye Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma?Nina wasi wasi, wenzetu mlioko jikoni tugahamisheni.Ingawa hiyo sheria inasema unaweza kuangalia nyaraka husika, lakini huruhusiwi kuzitoa nje.

Kuna haja ya kuanzisha upya mjadala kuhusu umuhimu wa marekebisho ya sherio hizo ambazo ni sawa na kuambiwa unaweza kwenda uwanjani, lakini huruhusiwi kuangalia mechi.Umekuwa mlinzi wewe?
 
Kwani mali za Mkapa mwenyewe ziliandikishwa? Je leo hii akitakiwa dhamana ya bilioni 15atashindwa?
 
Viongozi wadanganya mali zao
Mwandishi Wetu
Daily News; Tuesday,December 23, 2008 @21:15

Serikali inachunguza baadhi ya viongozi baada kubaini kuwa wana mali zaidi ya walizozitaja katika tamko la mali na madeni ya viongozi wa umma. Hatua hiyo inafanyika baada ya kuhakiki mali na madeni ya viongozi wa umma 260 wa ngazi mbalimbali nchini kote ili kubaini usahihi wa taarifa walizotoa kuhusu mali na madeni yao.

Taarifa ya mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne katika kipindi cha miaka mitatu, kuanzia Desemba 2005 hadi mwezi huu, ilisema kutokana na uhakiki huo viongozi wanne, walibainika kuwa na mali zaidi ya walizotaja.

“Kutokana na uhakiki huo, viongozi wanne walibainika kuwa na mali zaidi ya zile walizotaja katika tamko lao na Sekretarieti (ya Maadili ya Viongozi wa Umma) imeanzisha uchunguzi wa kina dhidi yao,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba.

Licha ya waliotaja mali zisizo sahihi, Ofisi hiyo ya Rais imesema pia itachukua hatua za kisheria dhidi ya viongozi waliokaidi kurejesha fomu za tamko la mali na madeni. Kulingana na taarifa hiyo, kati ya viongozi 7,447 waliotumiwa fomu za tamko, ni viongozi 4,864 waliorejesha. Viongozi wa siasa ni 2,130 kati ya 3,983 wakati viongozi wa utumishi wa umma ni 2,734 kati ya 3,464.

“Orodha ya viongozi wa umma 3,186 ambao hawajarejesha fomu za tamko kwa majina na mahali walipo, imeandaliwa na hatua zaidi zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria,” ilisema taarifa hiyo iliyotolewa kwa vyombo vya habari ikiwa na picha ya Waziri Simba na Katibu Mkuu Ikulu, Michael Mwanda.

Kulingana na sheria, miongoni mwa viongozi wanaotakiwa kujaza fomu hizo ni wabunge, mawaziri na manaibu wao, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya. Kwa upande wa malalamiko yaliyowasilishwa na wananchi dhidi ya viongozi wanaotuhumiwa kukiuka maadili, taarifa hiyo ilisema malalamiko 88 yalipokelewa.

Malalamiko hayo yako katika hatua mbalimbali za uchunguzi baada ya kufanyiwa uchambuzi wa awali ili kubaini yale yanayohusiana na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Gazeti hili halikufanikiwa kumpata Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Stephen Ihema kufafanua kwa kina juu taarifa hizo hususani kutaja majina na adhabu wanazostahili kupewa waliotaja mali zisizo sahihi na wale wasiorudisha fomu.

Kazi hiyo ya kubaini viongozi waliodanganya mali, inakidhi agizo la Rais Jakaya Kikwete kwa chombo hicho cha maadili ya viongozi wa umma alilolitoa wakati akihutubia Bunge, Agosti mwaka huu kwa kuitaka ifanye kazi ipasavyo. Aliitaka itimize wajibu ikiwamo kusajili, kuhakiki taarifa za mali na madeni ya viongozi kila mwaka na kushauri kwamba kiongozi anaposema ana mali kiasi fulani wafuatilie wajue alivyozipata na atoe maelezo ya kina jinsi alivyoipata.

Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kinatajwa kuwa chombo kikuu kinachohusika na kujenga imani ya wananchi kuhusu uadilifu wa viongozi wa umma. Inatekeleza majukumu yake kama yalivyoainishwa katika Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Namba 13 ya mwaka 1995.
 
Date::12/31/2008
Spika awacharukia wabunge
Exuper Kachenje
Mwananchi

WABUNGE wametakiwa kurejesha fomu za tamko la mali zao walizopatiwa na Ofisi ya Kamishna wa Maadili ndani ya siku 14 kuanzia leo, Spika wa Bunge Samuel Sitta amesema.

Spika Sitta alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na gazeti hili kuhusu urejeshwaji wa fomu hizo ambao tarehe yake ya mwisho ilikuwa jana.

Sitta, ambaye pia ni mbunge wa Urambo Mashariki, alisema: "Fomu hizo zilitolewa na Kamishna wa Tume ya Maadili, lakini ofisi yangu ilikuwa kama posta ya kuwafikishia wabunge majimboni.

Tarehe ya mwisho ya kurejesha fomu hizo ni leo (jana), lakini tunawapa wabunge siku 14 wawe wamezirejesha kutekeleza sheria Namba 13 ya maadili ya mwaka 1995."

Hata hivyo, jana Ofisi ya Bunge ilitoa taarifa inayobainisha kuwa baadhi ya wabunge hawakuzipata fomu hizo kama ilivyokusudiwa na Ofisi ya Kamishna wa Maadili mwenye dhamana na zoezi hilo.

Taarifa hiyo ilisema kutokana na hali hiyo, ofisi ya Bunge inaandaa utaratibu utakaowezesha wabunge ambao hawajapata fomu hizo kuzipata na kuzirejesha haraka inavyowezekana.

"Imebainika sasa kwamba baadhi ya waheshimiwa wabunge hawakuzipata fomu hizo. Kwa hiyo, ofisi inaandaa utaratibu ili wale waheshimiwa wabunge ambao hawajazipata fomu hizo, sasa wazichukue kutoka Ofisi ya Spika mara moja na kuzirejesha hapo haraka inavyowezekana," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo ya Ofisi ya Bunge.

Taarifa hiyo, iliyosainiwa na kaimu katibu wake, Eliakim Mrema imeeleza kuwa, wabunge watakaochelewa kurudisha fomu hizo watatakiwa kuandika maelezo na kueleza sababu za ucheleweshaji huo.

Katika maelezo yake, Spika Sitta alisema kuwa mfumo uliotumika mwaka jana kuwafikishia wabunge fomu hizo kwa kuzituma majimboni mwao umesababisha usumbufu, tofauti na ule wa miaka iliyopita wakati wabunge walipokuwa wakigawiwa fomu hizo kwenye kikao chao cha mwezi Novemba.

Alisema utaratibu wa mwaka huu umekuwa mgumu kwa kuwa ililazimu kila mbunge afike jimboni kwake ndani ya kipindi hicho cha mwezi Novemba ndipo apate fomu hiyo, jambo alilosema sehemu nyingine ilishindikana kwa kuwa wabunge hawakutembelea majimbo yao.

Sitta aliongeza kuwa, wamewasiliana na Ofisi ya Kamishna wa Maadili na kueleza hali hiyo na ndiyo sababu ofisi yake imetoa tamko kuwataka wabunge wasiopata fomu hizo kuzifuata ofisini kwake.

Kuhusu utekelezaji wa kazi za Bunge kwa mwaka huu mpya wa 2009, Spika Sitta alisema atahakikisha unafuata katiba na sheria.

"Kwa mwaka mpya wa 2009, tutafanya kazi zetu tukiweka umuhimu katika kufuata sheria na katiba ya nchi. Tutaendelea kufanya kazi kwa kufuata sheria na katiba," alisema Sitta
 
Last edited by a moderator:
Katika maelezo yake, Spika Sitta alisema kuwa mfumo uliotumika mwaka jana kuwafikishia wabunge fomu hizo kwa kuzituma majimboni mwao umesababisha usumbufu, tofauti na ule wa miaka iliyopita wakati wabunge walipokuwa wakigawiwa fomu hizo kwenye kikao chao cha mwezi Novemba.

Hivi mheshimiwa Spika alikuwa hajui kwamba hawa waheshimiwa hawakai majimboni kwao? Huwa wanaenda kufanya ziara tu hasa uchaguzi unapokaribia.

Angetuma forms Dar, wote wangezipata on time.
 
Vigogo matajiri sasa kubanwa
Mwandishi Wetu Disemba 31, 2008
Raia Mwema
*Wamo mawaziri, makatibu wakuu
*Watakiwa kutoa maelezo ya utajiri wao
*Baadhi kufikishwa mahakamani 2009

VYOMBO vya Dola vinachunguza ili kujua walikopata utajiri wa kutisha wa baadhi ya wanasiasa waandamizi na watendaji wa sasa na wa zamani serikalini, Raia Mwema imethibitishiwa.

Habari za uhakika kutoka serikalini zimethibitisha kwamba vyombo hivyo, ikiwamo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) vimekwisha kuwasiliana na wahusika, baadhi yao wakiwa wametakiwa kutoa maelezo ya kina kuhusu utajiri wa kutisha walioupata wakiwa madarakani.

Sambamba na uchunguzi huo, Serikali imezifanyia marekebisho makubwa fomu za maelezo ya mali na madeni ya viongozi wa umma kwa kuongeza kipengele kinachotaka maelezo ya mali na fedha zilizo nje ya nchi, kipengele ambacho kimeelezwa kuongezwa baada ya viongozi wengi kubainika kuwa na mali na fedha nyingi nje.

Kwa mujibu wa habari hizo, kabla ya kuwaandikia barua wanasiasa na watendaji hao mwanzoni mwa Desemba, 2008, vyombo vya dola vilikuwa vimekwisha kukamilisha sehemu kubwa ya uchunguzi wake kuhusiana na ukwasi mkubwa wa wanasiasa na watendaji hao waandamizi serikalini baadhi wakiwa wamestaafu, kujiuzulu ama kuachishwa na wengine wakiwa bado kazini.

Raia Mwema imethibitisha kwamba tayari baadhi ya wanasiasa hao wamekwisha kuandaa utetezi wa jinsi walivyopata mali walizo nazo ikiwa ni pamoja na zile ambazo wanazimiliki kupitia kwa familia zao ama marafiki wa karibu, mali ambazo hata katika fomu zao za kutangaza mali wanazomiliki hazimo.

Imeelezwa kwamba uchunguzi wa vyombo vya dola kuhusiana na mali walizonazo viongozi hao uliongezewa nguvu na uchunguzi unaoendelea kuhusu tuhuma mbalimbali dhidi ya wahusika, ikiwa ni pamoja na baadhi ya tuhuma ambazo tayari wahusika wamekwisha kufikishwa mahakamani.

Uchunguzi wa Raia Mwema umebaini kwamba pamoja na majalada ya kesi mbalimbali kuvisaidia vyombo vya dola kubaini kiasi kikubwa cha fedha na mali zilizomo mikononi mwa viongozi hao na familia zao, baadhi ya waliofikishwa mahakamani walijidhamini kwa kutumia mali wanazozimiliki wao na 'marafiki' zao mali ambazo nazo zinachunguzwa.

Baadhi ya majalada ambayo yako mikononi mwa vyombo vya dola ama yaliwahi kupitia mikononi mwa vyombo hivyo ni pamoja na tuhuma za rushwa kuhusiana na mkataba wa mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo Kahama mkoani Shinyanga, tuhuma za ufisadi katika kampuni za Meremeta Gold, Tangold, Deep Green na Mwananchi.

Tuhuma za mkataba wa Buzwagi zilimgusa aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, ambaye kwa sasa inaelezwa kwamba uchunguzi dhidi yake umekwama kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa kumfikisha mahakamani kwa tuhuma za rushwa baada ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kupitia jalada lake.

Tuhuma za ufisadi katika kampuni ya Meremeta, Tangold na Deep Green inawagusa watendaji wa sasa na wa zamani akiwamo aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika serikali ya Mkapa, Andrew Chenge. Chenge aliendelea katika serikali ya sasa ya Rais Jakaya Kikwete kwa kupewa uwaziri lakini alijiuzulu baada ya kutajwa katika tuhuma ya ununuzi wa rada ya kijeshi kutoa kampuni ya BAE Systems ya Uingereza.

Mbali ya Chenge wengine wanaotajwa katika Meremeta na Tangold, kampuni zinazohusishwa na upotevu wa Sh bilioni 155 za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ni pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Vincent Mrisho ambaye aliingizwa katika ukurugenzi wa kampuni ya Tangold alipokuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, kipindi ambacho ilielezwa kwamba Meremeta inaendesha shughuli zake za biashara ya dhahabu kwa ufanisi mkubwa.

Kampuni ya Meremeta ilikuwa ikifanya biashara ya kununua na kuuza dhahabu na kuendesha mgodi wa dhahabu wa Buhemba uliopo Buhemba mkoani Mara, kabla ya mgodi huo kufungwa.

Mbali ya Mrisho, wakurugenzi wengine wa Tangold Limited ni pamoja na aliyekuwa Gavana wa BoT Dk. Daudi Ballali (sasa marehemu), aliyefukuzwa kazi kwa tuhuma za ufisadi uliofanyika kupitia Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) wakati akiwa katika matibabu Marekani.

Yumo pia Gray Mgonja aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Uchumi, ambaye kwa sasa amestaafu na kufikishwa mahakamani akihusishwa na ufisadi unaohusu kampuni ya ukaguzi wa dhahabu ya Alex Stewarts. Mgonja aliunganishwa katika kesi iliyokuwa ikiwakabili mawaziri wa Mkapa, Daniel Yona na Basil Mramba, wakituhumiwa kusamehe kodi ya Sh bilioni 11 kwa kampuni hiyo.

Mtendaji mwingine aliyehusishwa na kampuni hizo ni aliyepata kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Patrick Rutabanzibwa.

Tuhuma kuhusiana na kampuni ya Mwananchi Gold, pamoja na watendaji wa BoT inahusishwa pia na waziri mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba, ambaye amekwisha kubainisha kwamba vitisho dhidi yake kuhusiana na kampuni hiyo ni vya kipuuzi kwa maelezo kwamba uanzishwaji wake ulilenga kusaidia wananchi.

Tuhuma nyingine ambazo zimekuwa zikipitia mikononi mwa vyombo vya dola ni tuhuma za ufisadi katika mradi wa umeme wa dharura uliokabidhiwa kampuni ya Richmond Development LLC ya Marekani, mradi ambao ulisababisha kujiuzulu kwa mawaziri watatu akiwamo aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.

Mawaziri wengine walioanguka kuhusiana na sakata la Richmond ni mawaziri waliowahi kuongoza Wizara ya Nishati na Madini, Dk. Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi, ambao pamoja na Lowassa walilazimika kujiuzulu mbele ya Bunge kutokana na shinikizo lililoelekezwa kwao baada ya uchunguzi wa Kamati Teule ya Bunge iliyoongozwa na Mbunge wa Kyela (CCM), Dk. Harrison Mwakyembe.

Kumbukumbu zinaonyesha kwamba majalada mengine yaliyopitia mikononi mwa vyombo vya dola ni uchunguzi katika mradi wa mkaa wa mawe wa Kiwira (Kiwira Coal Mines).

Habari zinasema uchunguzi huu unaweza kuwa ni matokeo ya awali ua utekelezaji wa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya Mwaka 2007 inayompa mamlaka ofisa yeyote wa taasisi hiyo kwa idhini ya Mkurugenzi Mkuu kumtaka mtendaji ama kiongozi wa umma kutoa maelezo ya mali anazomiliki.

"Ofisa yeyote wa Taasisi aliyeidhinishwa kwa maandishi na Mkurugenzi Mkuu anaweza, kwa taarifa ya maandishi kwa ofisa yeyote wa umma, kumtaka ofisa huyo wa umma kutoa, ndani ya muda na utaratibu kama itakavyokuwa imeelezwa katika taarifa hiyo, maelezo kamili na ya kweli kuhusu mali yote au aina yoyote ya mali ambayo ofisa huyo au wakala wake anaimiliki au ambayo ofisa huyo au wakala wake aliwahi kumiliki wakati wowote ambapo ofisa huyo wa umma alikuwa na wadhifa," inaeleza sheria hiyo.

Sheria hiyo inatoa mamlaka pia kwa ofisa uchunguzi wa TAKUKURU kumtaka ofisa ama kiongozi huyo "kutoa maelezo ya kweli ya namna alivyoipata mali ile" na kwamba maelezo ambayo yaliwahi kutolewa mahakamani kwa maandishi yanaweza kutumika kama ushahidi dhidi ya wahusika.

"Ofisa yeyote wa umma ambaye atashindwa kukidhi matakwa ya taarifa aliyopewa kwa mujibu wa kifungu hiki, au huku akijua anatoa maelezo ya uongo kuhusiana na mali yoyote, anakuwa anatenda kosa, na ikiwa atapatikana na hatia atahukumiwa kulipa faini isiyopungua shilingi laki mbili lakini isiyozidi shilingi laki tano au kufungwa jela kwa kipindi kisichopungua miaka miwili lakini kisichozidi miaka mitatu au adhabu zote kwa pamoja," inaeleza sehemu ya sheria hiyo.

Mbali ya kiongozi ama mtendaji, watu wa karibu nao wanaotajwa na sheria kama "wakala" watachunguzwa ikiwa ni pamoja na "mume, mke au mtoto, au mtu yeyote anayedaiwa, au mtu mwingine yeyote yule anayetenda kwa niaba" ya mhusika na hiyo hujumuisha mtu yeyote anayemiliki mali ambayo kupatikana kwake, yote au sehemu yake kulisababishwa na kiongozi ama mtendaji wa umma.

Sheria hiyo ambayo ndio imetumika kuwachunguza viongozi na watendaji hao wa umma inabainisha wazi kwamba ni kosa kisheria kwa mtu ambaye, akiwa au baada ya kuwa ofisa wa serikali, "anaishi maisha ya kiwango cha juu kuliko yale yanayolingana na kipato chake halali cha wakati huo au cha wakati uliopita; "anamiliki mali ambayo hailingani na kipato chake cha wakati huo au cha wakati uliopita, isipokuwa kama anatoa maelezo ya kuridhisha "mbele ya mahakama" kuonyesha jinsi alivyoweza kuishi maisha hayo au jinsi alivyoweza kupata mali hiyo.”

Imeelezwa kwamba ili kukidhi sheria hiyo ya TAKUKURU iliyopitishwa na Bunge na kusainiwa na Rais Kikwete, watuhumiwa waliotakiwa kuelezea mali zao watafikishwa mahakamani ili kujitetea kuhusiana na mali hizo, ikiwa ni pamoja na zile ambazo zimo mikononi mwa watu wa karibu nao.

Kifungu hicho kinabainisha kwamba, "Pale ambapo mashitaka yatakuwa yanaendelea, mahakama itaridhika kuwa, kwa kuzingatia ukaribu au uhusiano wa mshitakiwa na mazingira mengine, kuna sababu ya kuamini kuwa mtu yeyote ana au alikuwa na mali kwa dhamana ya au vinginevyo kwa niaba ya mshitakiwa au amepata mali hiyo kama zawadi kutoka kwa mhusika."

Hukumu inayotajwa na sheria hiyo kwa watu wanaomiliki mali isiyo maelezo ni pamoja na kifungo na faini na vyote vinatajwa kuweza kwenda kwa pamoja na pia inaelezwa kwamba mahakama itatoa amri ya kutaifisha mali inayohusishwa nae na sheria hiyo inabainisha;

"Atahukumiwa kulipa faini isiyopungua shilingi milioni moja lakini kisichozidi shilingi milioni tatu au kufungwa jela kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu lakini kisichozidi miaka mitano au adhabu zote pamoja.

Mahakama itaamuru ufanyike utaifishaji wa manufaa yoyote ya kifedha au mali inayomilikiwa na mtuhumiwa; na ya kiasi au thamani ya fedha iliyozidi kiasi au thamani ya pato la kifedha au mali ambayo upatikanaji wake haukuelezwa ipasavyo kiasi cha kuiridhisha mahakama."

Mwaka huu tutasikia na kuona mengi sana sana....sijui atabakia nani huko serikalini maana mmm wote karibu wachafu jamani sijui hata mkuu wa kaya kama atakoswa angalau kutajwa tu maana nae yumo jahazini tangu 1988...IPTL sidhani kama itamkosa.....yangu macho na masikio
 
JK kukaza buti ndiyo jibu pekee la CCM yako kuwa na wabunge wengi mwakani ila kama una zuga tu utalia sana labda utumie polisi kulazimisha ushindi kwenye ballot boxes uchaguzi ujao .
 
..jamani naomba kuuliza hivi hawa vigogo wanalipwa kiasi gani kwa mwaka? hapa nazungumzia mshahara,marupurupu ya safari,semina,kongamanos,warsha,vikao vya bodi etc etc.

..just by an estimate vigogo on average wanatakiwa wasizidishe kiasi gani kwa mwaka?
 
Wana JF,

Je haya matamko ya mali za waheshimiwa ni makrabasha ya Umma?

Nimekaa najiuliza, wanafanya uhakiki gani kuhusu hizo mali?

Ukidanganya unachukuliwa hatua gani?

Toka haya maadili yaanze 1995 ni wangapi wamakiuka na kutotekeleza maagizo hayo?

Ni nini makusudio ya zoezi hili? haswa kutaka kujua mali walizonazo-uongozi bora, namna ya kumfanya awe fisadi(sic),????

Ni Vitu-swali ambayo wananchi wanahitaji kuelimishwa

Nawasilisha
 
Kama haya yote yanafanyika kwa nia ya dhati na kwa utimilifu, Tanzania itaondoka kwenye ufukara wa kutupwa sooner than later. Kila mara ninapoulizwa na watu kutoka nje ya nchi ni nini kinachoifanya TZ kuwepo kwenye kundi la nchi 10 fukara zaidi ulimwenguni, nakosa jibu. Jibu sasa tunalo, ni ulafi na ukatili wa hawa jamaa waliopewa dhamani ya kutuondoa kwenye huu ufukara kwa miaka 47 sasa!! Ndio maana kila mara nikisikia jina la Mkapa napatwa na uchungu na hasira kwa pamoja! Let's wait and see!
 
MPs face deadline to reveal assets

SEBASTIAN MRINDOKO
THIS DAY
Dar es Salaam​

MEMBERS of Parliament, facing a two-week extended deadline to reveal their assets, are scrambling to comply with the mandatory regulation in the New Year to avoid losing their coveted Bunge seats.

According to the country’s laws, public leaders are required to submit their asset declaration forms at the end of each year.

However, by December 31, scores of MPs were yet to reveal their assets as required by the Public Leadership Code of Ethics Act Number 13 of 1995, due to reported delays in receiving the forms.

Submissions must be made in a written declaration on a prescribed form provided by the Ethics Secretariat.

The Bunge office recently issued a statement instructing MPs who are yet to receive the asset declaration forms to contact the Speaker’s Office immediately and ensure they fill the forms as soon as possible.

The statement warned that lawmakers who fail to reveal their wealth in due time would be required to explain themselves in writing.

Acting Clerk of the National Assembly Eliakim Mrema confirmed to THISDAY that some MPs were yet to submit their asset declaration forms as of yesterday.

He acknowledged that there were delays in distributing the assets declaration forms to lawmakers last year, which could explain why some MPs failed to meet the deadline.

’’After MPs fill up the assets declaration forms, they are required to submit the documents to the Ethics Secretariat, not the Speaker’s Office,’’ he said when asked to say how many lawmakers had so far failed to reveal their assets.

National Assembly Speaker Samwel Sitta was quoted as saying that he had given MPs a 14-day extension to reveal their assets.

As part of the broader fight against corruption, President Jakaya Kikwete’s government has been keen to ensure all public leaders stipulated in the law declare their assets on an annual basis.

Some public leaders suspected of under-declaring their wealth in previous years are already under investigation.

The existing legislation says the Ethics Secretariat ’may’ take action when public leaders fail to declare their assets.

Critics say such a legal loophole was a stumbling- block in the fight against corruption, and are calling for a major reform of the legislation to ensure heavy penalty to dishonest leaders.

Parliamentary sources say there is a sense of urgency among lawmakers who are yet to reveal their assets to do so in the coming week.

’’This government seems to be getting serious about leadership ethics, so many MPs are anxious to submit their asset declaration forms to avoid legal complications,’’ said a well-placed parliament official.
 
Thread hii imejirudia, lakini nimeshindwa kuifuta. Nadhani Mod ataiondoa
 
Vigogo matajiri sasa kubanwa

lC.gif
Mwandishi Wetu

Disemba 31, 2009
rC.jpg

bul2.gif
Wamo mawaziri, makatibu wakuu

bul2.gif
Watakiwa kutoa maelezo ya utajiri wao

bul2.gif
Baadhi kufikishwa mahakamani 2009

VYOMBO vya Dola vinachunguza ili kujua walikopata utajiri wa kutisha wa baadhi ya wanasiasa waandamizi na watendaji wa sasa na wa zamani serikalini, Raia Mwema imethibitishiwa.
Habari za uhakika kutoka serikalini zimethibitisha kwamba vyombo hivyo, ikiwamo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) vimekwisha kuwasiliana na wahusika, baadhi yao wakiwa wametakiwa kutoa maelezo ya kina kuhusu utajiri wa kutisha walioupata wakiwa madarakani.

Sambamba na uchunguzi huo, Serikali imezifanyia marekebisho makubwa fomu za maelezo ya mali na madeni ya viongozi wa umma kwa kuongeza kipengele kinachotaka maelezo ya mali na fedha zilizo nje ya nchi, kipengele ambacho kimeelezwa kuongezwa baada ya viongozi wengi kubainika kuwa na mali na fedha nyingi nje.

Kwa mujibu wa habari hizo, kabla ya kuwaandikia barua wanasiasa na watendaji hao mwanzoni mwa Desemba, 2008, vyombo vya dola vilikuwa vimekwisha kukamilisha sehemu kubwa ya uchunguzi wake kuhusiana na ukwasi mkubwa wa wanasiasa na watendaji hao waandamizi serikalini baadhi wakiwa wamestaafu, kujiuzulu ama kuachishwa na wengine wakiwa bado kazini.

Raia Mwema imethibitisha kwamba tayari baadhi ya wanasiasa hao wamekwisha kuandaa utetezi wa jinsi walivyopata mali walizo nazo ikiwa ni pamoja na zile ambazo wanazimiliki kupitia kwa familia zao ama marafiki wa karibu, mali ambazo hata katika fomu zao za kutangaza mali wanazomiliki hazimo.
Imeelezwa kwamba uchunguzi wa vyombo vya dola kuhusiana na mali walizonazo viongozi hao uliongezewa nguvu na uchunguzi unaoendelea kuhusu tuhuma mbalimbali dhidi ya wahusika, ikiwa ni pamoja na baadhi ya tuhuma ambazo tayari wahusika wamekwisha kufikishwa mahakamani.

Uchunguzi wa Raia Mwema umebaini kwamba pamoja na majalada ya kesi mbalimbali kuvisaidia vyombo vya dola kubaini kiasi kikubwa cha fedha na mali zilizomo mikononi mwa viongozi hao na familia zao, baadhi ya waliofikishwa mahakamani walijidhamini kwa kutumia mali wanazozimiliki wao na 'marafiki' zao mali ambazo nazo zinachunguzwa.
Baadhi ya majalada ambayo yako mikononi mwa vyombo vya dola ama yaliwahi kupitia mikononi mwa vyombo hivyo ni pamoja na tuhuma za rushwa kuhusiana na mkataba wa mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo Kahama mkoani Shinyanga, tuhuma za ufisadi katika kampuni za Meremeta Gold, Tangold, Deep Green na Mwananchi.

Tuhuma za mkataba wa Buzwagi zilimgusa aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, ambaye kwa sasa inaelezwa kwamba uchunguzi dhidi yake umekwama kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa kumfikisha mahakamani kwa tuhuma za rushwa baada ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kupitia jalada lake.

Tuhuma za ufisadi katika kampuni ya Meremeta, Tangold na Deep Green inawagusa watendaji wa sasa na wa zamani akiwamo aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika serikali ya Mkapa, Andrew Chenge. Chenge aliendelea katika serikali ya sasa ya Rais Jakaya Kikwete kwa kupewa uwaziri lakini alijiuzulu baada ya kutajwa katika tuhuma ya ununuzi wa rada ya kijeshi kutoa kampuni ya BAE Systems ya Uingereza.
Mbali ya Chenge wengine wanaotajwa katika Meremeta na Tangold, kampuni zinazohusishwa na upotevu wa Sh bilioni 155 za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ni pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Vincent Mrisho ambaye aliingizwa katika ukurugenzi wa kampuni ya Tangold alipokuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, kipindi ambacho ilielezwa kwamba Meremeta inaendesha shughuli zake za biashara ya dhahabu kwa ufanisi mkubwa.

Kampuni ya Meremeta ilikuwa ikifanya biashara ya kununua na kuuza dhahabu na kuendesha mgodi wa dhahabu wa Buhemba uliopo Buhemba mkoani Mara, kabla ya mgodi huo kufungwa.
Mbali ya Mrisho, wakurugenzi wengine wa Tangold Limited ni pamoja na aliyekuwa Gavana wa BoT Dk. Daudi Ballali (sasa marehemu), aliyefukuzwa kazi kwa tuhuma za ufisadi uliofanyika kupitia Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) wakati akiwa katika matibabu Marekani.

Yumo pia Gray Mgonja aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Uchumi, ambaye kwa sasa amestaafu na kufikishwa mahakamani akihusishwa na ufisadi unaohusu kampuni ya ukaguzi wa dhahabu ya Alex Stewarts. Mgonja aliunganishwa katika kesi iliyokuwa ikiwakabili mawaziri wa Mkapa, Daniel Yona na Basil Mramba, wakituhumiwa kusamehe kodi ya Sh bilioni 11 kwa kampuni hiyo.

Mtendaji mwingine aliyehusishwa na kampuni hizo ni aliyepata kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Patrick Rutabanzibwa.

Tuhuma kuhusiana na kampuni ya Mwananchi Gold, pamoja na watendaji wa BoT inahusishwa pia na waziri mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba, ambaye amekwisha kubainisha kwamba vitisho dhidi yake kuhusiana na kampuni hiyo ni vya kipuuzi kwa maelezo kwamba uanzishwaji wake ulilenga kusaidia wananchi.
Tuhuma nyingine ambazo zimekuwa zikipitia mikononi mwa vyombo vya dola ni tuhuma za ufisadi katika mradi wa umeme wa dharura uliokabidhiwa kampuni ya Richmond Development LLC ya Marekani, mradi ambao ulisababisha kujiuzulu kwa mawaziri watatu akiwamo aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.

Mawaziri wengine walioanguka kuhusiana na sakata la Richmond ni mawaziri waliowahi kuongoza Wizara ya Nishati na Madini, Dk. Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi, ambao pamoja na Lowassa walilazimika kujiuzulu mbele ya Bunge kutokana na shinikizo lililoelekezwa kwao baada ya uchunguzi wa Kamati Teule ya Bunge iliyoongozwa na Mbunge wa Kyela (CCM), Dk. Harrison Mwakyembe.

Kumbukumbu zinaonyesha kwamba majalada mengine yaliyopitia mikononi mwa vyombo vya dola ni uchunguzi katika mradi wa mkaa wa mawe wa Kiwira (Kiwira Coal Mines).
Habari zinasema uchunguzi huu unaweza kuwa ni matokeo ya awali ua utekelezaji wa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya Mwaka 2007 inayompa mamlaka ofisa yeyote wa taasisi hiyo kwa idhini ya Mkurugenzi Mkuu kumtaka mtendaji ama kiongozi wa umma kutoa maelezo ya mali anazomiliki.
"Ofisa yeyote wa Taasisi aliyeidhinishwa kwa maandishi na Mkurugenzi Mkuu anaweza, kwa taarifa ya maandishi kwa ofisa yeyote wa umma, kumtaka ofisa huyo wa umma kutoa, ndani ya muda na utaratibu kama itakavyokuwa imeelezwa katika taarifa hiyo, maelezo kamili na ya kweli kuhusu mali yote au aina yoyote ya mali ambayo ofisa huyo au wakala wake anaimiliki au ambayo ofisa huyo au wakala wake aliwahi kumiliki wakati wowote ambapo ofisa huyo wa umma alikuwa na wadhifa," inaeleza sheria hiyo.

Sheria hiyo inatoa mamlaka pia kwa ofisa uchunguzi wa TAKUKURU kumtaka ofisa ama kiongozi huyo "kutoa maelezo ya kweli ya namna alivyoipata mali ile" na kwamba maelezo ambayo yaliwahi kutolewa mahakamani kwa maandishi yanaweza kutumika kama ushahidi dhidi ya wahusika.
"Ofisa yeyote wa umma ambaye atashindwa kukidhi matakwa ya taarifa aliyopewa kwa mujibu wa kifungu hiki, au huku akijua anatoa maelezo ya uongo kuhusiana na mali yoyote, anakuwa anatenda kosa, na ikiwa atapatikana na hatia atahukumiwa kulipa faini isiyopungua shilingi laki mbili lakini isiyozidi shilingi laki tano au kufungwa jela kwa kipindi kisichopungua miaka miwili lakini kisichozidi miaka mitatu au adhabu zote kwa pamoja," inaeleza sehemu ya sheria hiyo.
Mbali ya kiongozi ama mtendaji, watu wa karibu nao wanaotajwa na sheria kama "wakala" watachunguzwa ikiwa ni pamoja na "mume, mke au mtoto, au mtu yeyote anayedaiwa, au mtu mwingine yeyote yule anayetenda kwa niaba" ya mhusika na hiyo hujumuisha mtu yeyote anayemiliki mali ambayo kupatikana kwake, yote au sehemu yake kulisababishwa na kiongozi ama mtendaji wa umma.
Sheria hiyo ambayo ndio imetumika kuwachunguza viongozi na watendaji hao wa umma inabainisha wazi kwamba ni kosa kisheria kwa mtu ambaye, akiwa au baada ya kuwa ofisa wa serikali, "anaishi maisha ya kiwango cha juu kuliko yale yanayolingana na kipato chake halali cha wakati huo au cha wakati uliopita; "anamiliki mali ambayo hailingani na kipato chake cha wakati huo au cha wakati uliopita, isipokuwa kama anatoa maelezo ya kuridhisha "mbele ya mahakama" kuonyesha jinsi alivyoweza kuishi maisha hayo au jinsi alivyoweza kupata mali hiyo.”

Imeelezwa kwamba ili kukidhi sheria hiyo ya TAKUKURU iliyopitishwa na Bunge na kusainiwa na Rais Kikwete, watuhumiwa waliotakiwa kuelezea mali zao watafikishwa mahakamani ili kujitetea kuhusiana na mali hizo, ikiwa ni pamoja na zile ambazo zimo mikononi mwa watu wa karibu nao.

Kifungu hicho kinabainisha kwamba, "Pale ambapo mashitaka yatakuwa yanaendelea, mahakama itaridhika kuwa, kwa kuzingatia ukaribu au uhusiano wa mshitakiwa na mazingira mengine, kuna sababu ya kuamini kuwa mtu yeyote ana au alikuwa na mali kwa dhamana ya au vinginevyo kwa niaba ya mshitakiwa au amepata mali hiyo kama zawadi kutoka kwa mhusika."

Hukumu inayotajwa na sheria hiyo kwa watu wanaomiliki mali isiyo maelezo ni pamoja na kifungo na faini na vyote vinatajwa kuweza kwenda kwa pamoja na pia inaelezwa kwamba mahakama itatoa amri ya kutaifisha mali inayohusishwa nae na sheria hiyo inabainisha;

"Atahukumiwa kulipa faini isiyopungua shilingi milioni moja lakini kisichozidi shilingi milioni tatu au kufungwa jela kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu lakini kisichozidi miaka mitano au adhabu zote pamoja.

Mahakama itaamuru ufanyike utaifishaji wa manufaa yoyote ya kifedha au mali inayomilikiwa na mtuhumiwa; na ya kiasi au thamani ya fedha iliyozidi kiasi au thamani ya pato la kifedha au mali ambayo upatikanaji wake haukuelezwa ipasavyo kiasi cha kuiridhisha mahakama."

Nimejaribu kutafuta sheria watakazotumia kuwashitaki lakini sikuzipata. Nimeona ile ya Money-Laundering na ile ya Anti-Corrpution, lakini zote zina adhabu ndogo ndogo tu kwa watu waliotafuna mabilioni ya nchi. Mtu mwenye visenti ukijidai utampiga faini ya Shilingi milioni mia mbili ni kama unatwanga maji kwenye kinu.
 
Mtu aliyeiba mabilioni na unamchaji laki 3 mpaka 5, Ila labda hiyo ya kutaifisha mali sawa. Tutaona itakapofikia/.
 
Willo,
Zoezi kama hili sio Ukomunist hata kidogo isipokuwa kuwepo na malengo ya kuendesha zoezi kama hili ndio muhimu. Sheria husimama pale wanasheria wana sauti kusimamisha mashtaka.. TZ hakuna sheria isipokuwa ile ya kesi za jinai, vibaka, wabinjukaji na wale wa ofisini ambao hesabu hazikubaliani.

Maelezo yako yote yame -base kwenye nchi za magharibi ambako wao system yao tayari hairuhusu kabisa vitendo kama hivi na wala kingozi wa serikali hawezi kuwa mfanyabiashara kwa wakati mmoja... lini ataweza kulitumikia taifa?..Sisi tumeshindwa kabisa kutofautisha kati ya kiongozi ndani ya chama na yule wa serikali. Kiongozi wa ngazi ya juu CCM anayo sauti kubwa kuliko kiongozi yeyote nje...hata kama mtu huyo akistaafu kazi serikalini bado chama kitamlinda kwa hali na mali.

Kwa hiyo zoezi lolote lile huendeshwa pale sheria iliposhindwa na huyo Sumaye asingeweza kujilimbikiza mali zote hizo kama sheria imesimama na imechukua mkondo wake. Ni kweli zoezi kama hili haliwezi kufanikiwa na sababu kubwa ni kwamba hakuna sheria zaidi ya sheria hizo kuwa vitabuni ndani ya makabati.

Zoezi la Sokoine - fagio la chuma halikuwa na matatizo kwa raia ila haohao viongozi ambao walikuwa above the law. Je, kuna mbinu gani zaidi kuhakikisha viongozi hawana sauti zaidi ya sheria hasa ktk nchi ambayo imefuata sera ya Chukua Chako Mapema....

tacha nani kasema...kama unavyokufanya si ulale..kwa nn ucomment
 
Back
Top Bottom