Utawezaje kuishi Kwa Furaha?

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
UTAWEZAJE KUISHI KWA FURAHA?

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Nashukuru nilijifunza kuishi na Furaha tangu nikiwa mdogo. Popote utakapokutana na Taikon utamuona ni mwenye furaha, Kwa sababu Furaha inaishi ndani yangu. Furaha huishi kwa Washindi. Ndugu yangu sisemi haya kama motivation speaker Bali nazungumza Kwa uhalisia na uzoefu.

Wakati nafukuzwa Ada kipindi nasoma, bado nilikuwa nafuraha. Ni miaka hiyo nikiwa Makanya Huko nyumbani Kwa Bibi Nasemba nilikolelewa. Maisha yalikuwa magumu lakini yalikuwa mazuri Kwa sababu kulikuwa na upendo na Tumaini. Kukosa chakula au Kula chakula kilekile hakikuondoa furaha yangu Kwa sababu nilifundishwa kutosheka na kushukuru Kwa kila baraka itakayokuja katika Maisha yangu. Haijalishi mitazamo ya Watu wataiona baraka hiyo ni ndogo au kubwa lakini kwangu kila baraka niliyopewa niliichukulia kama Zawadi kubwa ambayo sikuistahili. Hicho kilinifanya niwe na furaha.

Maumbile yangu hayakuwahi kuwa kikwazo katika Yale niliyokuwa nayafanya. Nakumbuka nilikuwa miongoni mwa Watoto wanaoongea na ulimi(kithembe) Jambo ambalo Watu wasiowaadilifu walikuwa wakinikejeli na kunidhihaki. Maneno s na z nilikuwa naweka th na dh.
Maneno kama "sasa" ningetamka "thatha" na neno "zamani" ningetamka "Dhamani"

Lakini pia nilikuwa na kigugumizi ingawaje sio kile kikali. Hasa ninapoongea mambo serious. Lakini sikuwahi kujilaumu, kujichukia, na kuwa na huzuni juu yangu. Bali nilikuwa Natafuta namna ya kudhibiti Hali hizo ili niongee kama wengine.
Mara Kwa mara nilikuwa nikienda Kuomba Milimani na kujitathmini juu ya Maisha yangu. Ni kipindi hichohicho nikiwa shule ya Msingi. Huko ndiko nilikuwa najifunza Mimi ni Nani na nini ninatakiwa kukifanya juu ya Maisha yangu.
Kujipenda mwenyewe kutakupa furaha, kujikubali na kukubali Hali zako zote kutakufanya uishi Kwa furaha.

Kupambana ili kuwa Bora na kuwa na Tumaini la kujiboresha kutakufanya uwe na furaha. Hata kama uanguke mara ngapi.

Kuzaliwa kwenye shida kusikufanye uwe mwenye huzuni. Taikon alizaliwa na kulelewa katika mazingira magumu lakini hiyo haikunifanya nijihukumu Kwa yaliyopita au yaliyotokea. Haikunifanya niwahukumu walionizaa au kunilea.
Ili uishi Kwa furaha usiwe mtu wa lawama na kuhukumu wengine au kujihukumu mwenyewe. Bali uwe MTU wa kutafuta namna ya kuishi vile unavyotaka. Na NI Jambo lisilotokea Kwa Usiku mmoja. Ni mchakato wa miaka na miaka.

Na ili usilaumu na kuwadhulumu au kujihukumu ni lazima uwe na tabia ya kusamehe, kuwasamehe na kujisamehe. Huwezi kuwa MTU mwenye furaha kama hutoi Msamaha.
Taikon ni mtu mwenye furaha kwà sababu sio MTU mwenye kinyongo, anasamehe na kujisamehe. Kwa sababu hatuishi Kwa kwenda Mbele Bali tunaishi Kwa kusonga Mbele.

Ili uishi Kwa furaha usiishi Kwa kubagua na kudharau Watu, kujiona Bora kuliko wengine. Kwa sababu hicho ni Kiburi na dharau zako ndio zitakufanya uwe na chuki. Na Siku zote chuki haikai pamoja na furaha. Kujiona Bora ni kudhani kuwa unastahili kuliko wengine. Na hii itakufanya uwe na Wivu wakipumbavu.
Fikiria unajiona Bora kuliko mwingine alafu huyo mwingine anafanikiwa Kabla yako hapo ni lazima uchungu ukuingie ndani yako. Lazima upoteze furaha yako.

Taikon ambaye ndiye Mtibeli halisi, ninajua upendo ndio furaha yenyewe. Pale unapopenda wengine na kujipenda ndivyo unavyozidi kuwa na furaha.

Penda wengine wapate mambo Mema na mazuri. Usiwe Mchoyo. Wape wengine Yale uliyonayo kama utaona yatawasaidia. Hiyo ndio namna ya kuishi Kwa Furaha.

Kwa uwezo wa Mungu tulisoma na kumaliza shule. Tulisoma ili tuwafanye wale ambao hawakusoma wapate Elimu waliyoikosa. Tunajua kuwa wapo waliotamani kuwa na Elimu lakini mazingira yaliwakwamisha, pia wapo ambao walijichanganya Kutokana na changamoto za kitabia. Hiyo yote ni sehemu ya kujifunza. Na hatutawahukumu Kwa sababu Sisi ni kitu kimoja.
Ndio maana tutaandika kutoa angalau kidogo Kati ya Yale mengi Kwa Ndugu zetu ili nao wapate Elimu.
Furaha ni pamoja na ku-share mambo mazuri na Wengine. Hiyo ni namna ya kuishi Kwa Furaha.

Chochote ambacho umebarikiwa na kujaliwa iwe ni uzuri, Pesa, utajiri, Akili, Imani basi ili kikupe furaha lazima u-share na wengine ikiwezekana Bure Kabisa. Hivyo ndivyo utakavyoishi Kwa Furaha.

Usipende kuwazidi wengine lakini kuwa namba moja kwenye Wema katika kuwafanya Watu wawe na furaha, elimu, na Maisha mazuri. Hiyo ndio namna ya kuishi Kwa Furaha.

Huwezi ukawafanya Watu waishi Kwa Furaha alafu ukaishi Kwa taabu. Ukakosa mahitaji yako muhimu. Usipende kushindana ili kuwazidi Watu Kwa vitu. Utaipoteza furaha yako Kam vitu hivyo vinavyopoteza ubora wake Kwa ku-expire.

Ili uishi Kwa furaha ni lazima uizingatie Leo zaidi kuliko Jana na kesho.
Kesho isikusumbue, usiihangaikie kesho ambayo huijui wala kuiona. Hiyo itakufanya usiitendee Haki Leo. Najaribu kusema usiwe na matarajio Makubwa kuhusu kesho. Matarajio yako yawe katika kile ulichonacho naam ndio Leo ambayo unaishi. Ili usije ukadhulumu wengine Kwa ajili ya kesho.

Hivyo ndivyo namna ya kuwa na furaha katika Maisha yako.

Na utakapooa na kuwa na familia yako. Jifunze kuvaa viatu vya mwenzako Kabla ya kuvaa vyako. Jaribu kuishi kwenye nafasi ya Mwenza wako. Hisi kama anavyohisi, fikiri kama anavyofikiri. Muelewe kisha mtendee Haki, mpende na kisha uwe mwaminifu (mkweli) hayo yote yafanye Kwa Akili. Hivyo ndivyo utakapokuwa na furaha katika Maisha yako.
Usiwe na Kiburi katika Ndoa yako bila kujali Majaliwa yako. Ukishaoa Mkeo au kuolewa, ninyi ni wamoja, saidianeni sio Kwa mazuri tuu Bali hata Kwa mabaya. Sio Kwa ubora tuu Bali Kwa madhaifu pia.

Kabla hujahukumu Samehe, na usipende kuangalia Makosa ya mwenzako Bali Angalia Wema wake. Yaani Wema utangulie Ubaya. Hivyo ndivyo namna ya kuishi Kwa Furaha.

Hayo yote Taikon Baba yenu ameyafanya katika Maisha yake, na ndio maana siku zote amekuwa mtu wa furaha. Hivyo ndivyo utakavyoishi Kwa Furaha Binti na kijana wangu.

Acha nipumzike sasa.

Nawatakia Sabato njema.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
O.

Naweka kiti changu hapa narudi baadae kusoma
 
Umenena kweli ubarikiwe.
 
Uzi upo poa ,Tafadhali naomba unipe link ule Uzi wako wa anayekutenga na Yeye mtenge ..Kuna mtu nataka nimseme kifasihi.
 
Tatizo la binadamu ni kwamba ukitoa Bure wanakudharau sana ama hawakutilii maanani, so unakuwa na huzuni sana.
 
Back
Top Bottom