Utatuzi wa kizungumkuti cha ajira na maslahi kwa Watumishi wa Umma chini ya Rais Samia

Nyabukika

JF-Expert Member
Jun 15, 2022
1,402
942
Katika zama hizi za mapinduzi ya sayansi na teknolojia moja ya changamoto kubwa Katika nchi zinazoendelea haswa barani Afrika ni suala la ajira na maslahi kwa watumishi. Hili suala limekuwa ni kizungumkuti au kitendawili kisichokuwa na majibu.

Viongozi wengi suala hili la ajira kwa vijana limekuwa likiwaumiza kichwa na pengine hata kuleta machafuko Katika nchi husika, kwa kuona hilo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ameamua kuliangalia kwa jicho la tatu na kuanza kulitolea masuluhisho.

Licha ya ajira 16,676 zilizotolewa hivi karibuni kwa wahitimu mbalimbali katika sekta ya Afya na Elimu. Bado nafasi 736 ziko wazi katika maeneo ya Daktari meno (50), Tabibu Meno(43), Tabibu msaidizi(244), Mteknolojia Mionzi(86) na Muuguzi cheti(313). Haijawahi kutokea ajira zikabaki, hii ni kubwa kuliko.

Pamoja na ajira hizi, mambo mengine yaliyofanywa katika kipindi kifupi cha Rais Samia katika kada ya utumishi wa umma;

Suala la kupandishwa madaraja WATUMISHI laki moja tisini elfu na miatano sitini na mbili~ 190,562 (Kwa wasioelewa, hii imeigharimu Serikali kiasi cha takribani TZS BILIONI 39.6). Suala hili linatoa nafasi ya ajira mpya zaidi kujaza nafasi mbalimbali za waliopandishwa vyeo nk. Hakika hii ni hatua kubwa sana.

Vile vile Mhe Rais Samia aliruhusu taasisi zote zenye uhitaji wa wafanyakazi kupewa vibali vya ajira mpya na kutolewa vibali kwa watumishi walioomba kubadilisha vituo na kwenda kuongeza taaluma kwa mujibu wa taratibu na sheria za utumishi wa umma. Hakika hii pia ni nafasi ya kuajiriwa kwa watumishi wapya kwenda kujaza nafasi wazi zitakazo achwa.

Vilevile suala la kuondolewa kwa mzigo wa tozo ya 6%(VALUE RETENTION FEE) kwa watumishi waliokuwa wanufaika wa mikopo ya Elimu ya juu (HESLB). Kiwango hiki cha 6% kimekuwa mzigo mzito kwa watumishi hususani vijana wanaotoka Vyuo Vikuu, Rais Samia atakumbukwa sana kwa hili. Kuboreshwa kwa mazingira ya kazi ya watumishi. Hii inatupa hamasa watumishi kutoa huduma bora na itoshe kusema kwamba Rais Samia Suluhu Hassan amejidhatiti haswa katika kutatua tatizo la ajira kwa vijana na uboreshaji sekta ya utumishi serikalini.

Tumuunge mkono azidi kuijenga Tanzania yetu.
 
Back
Top Bottom