Utapeli mtandaoni kutoka Mtanzania anayeishi Dubai

Kibenje KK

JF-Expert Member
May 28, 2016
267
380
Hakuna kitu kinarudisha Nyuma maendeleo ya wafanyabiashara wengi kama utapeli wa Mtandaoni.

Mtu unafanya kazi unajikusanya alafu mtu anakuja kukutapeli.

Nimekutana na tapeli ambaye anaishi Dubai na kazi yake ni kutapeli Watanzania kwa kudanganya kuwa anauza magari. Ametutapeli zaidi ya watu sita na sasa tunaojuana wote Tsh 20M na zaidi

Alikua akificha majina yake na sura lakini tumepata vyote majina na picha zake na watu wa karibu walio huko wanaomjua.

Ni Mtanzania bado.

Naomba msaada wa utaratibu wa kuamkamata mtu kama huyu aliye Dubai na anatia watu Hasara.

NB. Sio wale wanye namba za Dubai alafu wanaishi Tanzania. Huyu ni Mtanzania na yuko Dubai.

Msaada wa utaratibu wa kumpata na kumkamata.
 
Back
Top Bottom