Utapeli kwa Kutumia Harufu..............

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,146
13,216
Haijanitokea lakini kwa kuwa imemtokea myu aliyenipa ushuhuda wote nimeona si haba kuwajuza wanajamvi la kama ilishajuzwa si vibaya kukumbushana mintaarafu kuna wanachama wapya kila uchao

Ni Jumatau hii tu!! (17/1/2012) Rafiki yangu mmoja alitoka Morogoro kuja kuhudhuria mkutano hapa DSM ambapo na mimi nilikuwepo, wakati anavuka barabara maeneo ya PPF Tower kijana mmoja akamjongea na kumpa shikamoo, jamaa hakuitikia, kijana akasisitiza, jamaa hakuitikia, in the process ghafla akasikia harufu mbaya sana..........kijana akasalimu mara ya tatu rafiki yangu akaamua kuondoa kinu juani na kuitikia..........dogo akamuuliza jamaa eneo hili nasikia kuna harufu chafu.....jamaa yangu ghafla akajisikia kama anaishiwa nguvu.....yule dogo akaendelea na hamsini zake (kwa mnyato kama vile anasikilizia kitu fulani) jamaa yangu akajitahidi kuvuka barabara lakini akajikuta anapepesuka ndiposa akaamua atulie kwa muda....aliangalia ng'ambo na kumuona kijana akigeuka..kwa kuwa alishamshtukia kijana akatokomea kwenye magari......thanlk God jamaa aka-regain na kujiuliza sana.................

J eumeshakutana na utapeli huu????

Tujuze mwanawane na mbinu ulizotumia.................
 
sijui kama atapona mtu kwa staili hii, cha msingi ni kuchukua tahadhari na ujamaa wetu wa kusalimiana, na habari zaidi kwamba huwa wanaty maeneo yenye ukimya (yasiyo na watu)
mmmh! hii kali
 
Jamii zetu zimeharibika.. Zamani una gari hata iwe usiku wa manane,ukipita stendi ya daladala,ukiona kuna wanaongojea usafiri,unasimama,unauliza wanakoenda,kama kunaelekeana na unakoenda,unawachukua. Au kamma sio stendi,nawe huna usafiri na ni barabarani magari yanapita,ukisimamisha,unapewa lifti ya walau kukupunguzia safari kama dereva ana uelekeo wa huko uendako.
Sasa hivi,thubutuuu....
Hatuaminiani!
 
Kwahiyo mkuu unanishauri hata nikisikia harufu ya KIJAMBO tuchukue tahadhari sio?
 
Back
Top Bottom