Utafiti: Uchungu wa uzazi kwa wanaume.

Mkeshaji

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
4,262
1,416
Madaktari bingwa walikuwa wanafanya majaribio ya utafiti wao walioufanya.

Utafiti huo ulikuwa ni kuhusu dawa ya ambayo anapewa mama mjamzito muda mfupi kabla ya kujifungua ili uchungu wa uzazi uhamie kwa mume aliyempa ujauzito.

Mama mmoja alikwenda kujifungua na akapewa dawa hiyo. Mumewe naye alishapewa taarifa hizo ambazo alikubaliana nazo (kwamba dawa apewe mkewe ili uchungu uhamie kwake mwanaume). Kwa mantiki hiyo mumewe alitakiwa kuwepo pale maeneo ya hospitali ili kuhakiki matokeo ya utafiti.

Mama hakupata uchungu. Cha ajabu mumewe naye hakupata uchungu. Kuona vile madaktari wakamwongezea mama dozi. Safari hii tena si mke wala mume, wote hakuna aliyepata uchungu. Dozi iliendelea kuongezwa tena na tena hadi mama akajifungua lakini bila kupata uchungu, si yeye wala mumewe.

Wawili hao na kachanga kao wakatoka kuelekea nyumbani. Kufika kule wakamkuta housboy wao yuko hoi mahututi kwa uchungu.
 
Hahahaha hii kali,duh houseboy ndo baba mtoto ama.kwakwakwa mbavu zangu
 
Ndoa inateketea hivi hivi, technolojia nyingine mh cjui kama zitakaa zitokee!
 
mtoto ata asifanane na mimi ata masikio...naua
Yaelekea bado hujapata mtoto.
Wapo waswahili tena wakorofi kweli wanalea watoto wa kihindi/kiarabu/kizungu na wamezaliwa ndani ya ndoa ambayo baba na mama ni waswahili pyua.
 
Yaelekea bado hujapata mtoto.
Wapo waswahili tena wakorofi kweli wanalea watoto wa kihindi/kiarabu/kizungu na wamezaliwa ndani ya ndoa ambayo baba na mama ni waswahili pyua.

we unaongea nini mkuu, nipe mwanao wa kike nioe afu anizalie mtoto sio wangu uone nitamfanyaje
 
Back
Top Bottom