Uspika: Dr. Kashilila anakuwa overlooked sana kwenye nafasi hiyo

Ng'wanamangilingili

JF-Expert Member
Aug 22, 2015
5,706
4,748
CCM wanaweza kuushangaza umma kama enzi za 2015GE, watu wakapigana mapembe na kambi zao then JPM akawapita katikati yao kama maandiko ya Jesus alivyowapita wanafunzi wake kati kati yao.

Mi naona kwa sasa anatafutwa spika wa ku cool temperature kuelekea lango la 2025 marathon, na si spika wa miaka mitatu astaafu aanze kulipwa pension. Naona CCM wanaweza wasichelee kumpatia spika yeyote mwenye followers ama ambae yuko established kwa sbb they need a fella mwenye kulisimamia bunge kwa weredi hadi 2025.

Hazihitajiki mbwembwe sijui much know blah blah makundi afterall Piga ua mhimili ni Serikali tu hizo zingine mbwembwe,hata Tulia mtamlaumu bure huo ndio ukweli alikua anakitete cha kutetea chakula yake na familia. Rejea ya Six alivyotaka kuwa mhimili yaliyomkuta.

Having said that, yule ex-katibu wa bunge anaweza akawa surprise pick ya CC na wakaletewa mezani kumaliza mchezo. Ni msekwa ama Six sijui nae alianzaga na ukarani wa bunge, so Dr Thomas Kashililah ana uzoefu wa kutosha na madubwasha ya kanuni and the likes.

Simjui hanijui simpigii debe huo ni mtazamo wangu kama wengine wanavyoona muona Msukuma, sijui Jakumwi yule na kishort mwenye jina la kufikia la baba wa Taifa. Manake akili na macho na masikio ya watu yameelekezwa kwa Bi Stern aka Relax na Fire au moto wa kijenge wa kufukiza balaaa ze ikiwemo wachawi kwa kabila lake aka Chenge pamoja na Yankees.

CCM haijawahi kufeli jambo ila wenye jambo ndio hufeli sometimes.

NB: Mode Penye Kigaigai weka Dr. Thomas Kashililah
 
CCM wanaweza kuushangaza umma kama enzi za 2015GE, watu wakapigana mapembe na kambi zao then JPM akawapita katikati yao kama maandiko ya Jesus alivyowapita wanafunzi wake kati kati yao.
...
... kwanza acha kufananisha vitu vya ajabu ajabu na jina lipitalo majina yote. Pili, ni biblia ipi hiyo inasema Jesus alipita katikati ya wanafunzi wake?
 
Tatizo ni siasa, wengi wakishaingia kwenye siasa kazi yao ni kuwaimbio watukufu, ukikengeuka tu unalo. Huoni yaliyomkuta Ndugai? Nani atapenda yamkute kama ya Ndugai?

Vv
 
Kwahiyo wanasiasa wetu tulionao zama hizi hakuna anayeweza kusimamia anachokiamini ??!!
 
Dr Thomas Kashilila amefanya kazi kwa nafasi ya katibu wa bunge kati 2009 chini ya Spika Samuel Sitta na eliondolewa Oct 2017 baada ya nafasi yake kuchukuliwa na Steve Kigaigai.

Kashilila anabebwa na uzoefu wa utawala kama house clerk wa kufanya kazi na maspika 3 Big Sam, Anne Makinda na Job.

Kisiasa hakuna anemjua hata kidogo akiongoza vikao vya bunge.

Anabebwa na assets za kujua bunge na mfumo wake wa utawala, anakuwa na liabilities kwenye kutojulikana kuonekana akiendesha vikao vya kisiasa. Bunge ni sehemu ya kufanya siasa na kwa kuwa kawa muajiriwa wa serikali, anaweza kuwa too soft kwa mamlaka ya Urais ambayo ameyatumikia kama house clerk na baadae N/katibu mkuu wizarani.

Kwa kuwa spika ni nafasi ya kisiasa na mkiti wa chama ambae pia ndie rais amehusika kwa namna moja au nyingine kuanguka kwa spika Job Ndugai, bila shaka ubinadamu unaweza kufanya mamlaka ya uteuzi ambayo ni CC itamsikiliza sana mkiti wao anataka spika wa aina gani.
Na baada ya majina 3 kutoka, tutaona namna ambavyo wajumbe ambao ni wabunge watakuwa "wakivuta" kutoka kwa majina 3.

Sipati picha namna miamala itatembea. Wakati wengine wanalia Januari imekula hela za ada na nyumba, kuna watu Januari wanapenyeza rupia ili kushawishi "wajumbe"kama jina likipenya 3 bora wawe na chance ya kakalia kiti cha ukuu wa jumba la kutunga sheria ambapo kwa nafasi hiyo inamfanya mhusika kuwa mjumbe wa CC pia.

This time 2021 sijui kama tuliwaza Taifa litaoitia mchakato wa kupata spika kwa sababu ambazo sote tumeziona zikitokea.

Bado najiuliza, Jim Mbatia kaishia wapi na hoja yake ya kwenda mahakamani kupinga maamuzi haya ya Job kumuandikia barua Katibu wa chama badala ya CEO wa bunge? nini kimemnyamazisha Mbatia?

Kila la heri wagombea wa ukuu wa mjengo wa Idodomya.
 
Spika wa Bunge si nafasi ya kisiasa, Spika kazi yake ni kuliendesha Bunge bila kujali upande wowote wa vyama vya siasa japo Ndugai hakufanya hivyo. Spika wa Bunge ni mwajiriwa wa serikari ni tofauti na wabunge ambao kila mmoja yupo ka ajili ya chama chake.
 
Ndugu yangu, ingekuwa spika anatokana na mfumo wa utumishi wa umma, hoja yako ya kuwa spika ni "muajiriwa wa serikali" ingekuwa na mashiko.

Ila kama ulivyoona jana na huko nyuma, mgombea wa uspika anatakiwa kuchukua form kwenye chama chake then apate udhamini wa chama na jina lake lipelekwe tume ya uchaguzi kuwa XYZ amedhaminiwa na chama chake kugombea nafasi iliyo wazi.

Tayari mpaka hapo tunakuwa anaingia kuongoza nyumba ya kutunga sheria anakuwa mwana siasa na kama atakuwa mwana CCM kama ambavyo imekuwa kwa maspika wote waliopita, mtu huyo anakuwa mjumbe wa kamati kuu (C) ya Halmashauri Kuu ya CCM. Unaposema mtu huyu sio mwanasiasa hoja yako inakosa mashiko.

Na kwa kuwa anategemea kuchaguliwa na wabunge akishindanishwa na wagombea wa vyama vingine bungeni, ikishakuwa kuna uchaguzi au "uchaguzi-endorsement" kama huu wa sasa, ni simple principle mtu huyo sio mteuliwa wa serikali.

Japo akishakalia kiti baada ya kula kiapo anapata fursa ya kuhudumiwa na serikali kwa stahiki chungu mzima ambazo bunge limeainisha spika apewe na ataishi "lavish life" baada ya kustaafu au kuiuzuru "mpaka kifo kimtenge na dunia"
 
Back
Top Bottom