Usipowajibika kama mke, jua kuna mke mwenzio

livewise1

JF-Expert Member
May 25, 2019
837
952
Simple rule.

Kwa wale wanawake wasiotaka kuwajibika kwa wanaume wao kimajukumu ya mke, kama mwanaume anakupa kila unalostahili kupata basi ujue kuna mke mwenzio. Kivyovyote vile, kuna hali ya kuvumilia na ukomo wa kuvumilia pia upo.

Mke anavumilika kwa mapungufu flani flani nayo yasizidi. Mfano, kutokujua mapishi mbalimbali, kusahau baadhi ya maelekezo, kutoivana na ndugu wa mume, kutojua matumizi ya teknolojia nyumbani. Lakini visizidi maana itakuwa kikwazo.

Mwanamke havumiliki mambo kadhaa kama vile kurudi nyumbani kwa kuchelewa bila sababu za msingi, kudharau watu wa karibu wa mume, kuwa na mazoea kupitiliza na baadhi ya watu hasa wa kiume, kuleta ujuaji kwenye kila kitu hata asichojua, kelele za mara kwa mara zinazochosha akili ya mume, kujiunga vikoba bila taarifa hali inayopelekea kuathiri uchumi wa ndani, kutoka nyumbani ovyo ovyo bila taarifa na mengineyo.

Haya ni mambo yanayovunja ndoa au mahusiano au kusababisha uwe na mke mwenzio pembeni ambae atatimiza waajibu wa ki mke ipasavyo.

Safari inaendelea kusaka mwenye angalau atajitahidi kufanya waajibu wake.
 
Back
Top Bottom