Usimwambie mtu siri za ndoa yako

Denis1729

Member
Sep 9, 2021
34
109
Ndoa ni kiungo muhimu zaidi chenye raha na starehe kubwa wahusika wanapochunga mipaka na kutunzana vilivyo. Kwa upande mwingine, huweza kuwa chanzo na masikitiko makubwa maishani iwapo hutatumia hekima kwa mambo yanayohusiana nayo.

Je, wajua kuwa ulimi ndiyo huunda na kubomoa ndoa? Haya ni baadhi ya mambo ambayo kamwe hufai kutumia, na siri za kutotoa ili ndoa yako idumu.

Usiwahi kumwambia rafiki ama mtu yeyote kuhusu jinsi mumeo ama mkeo alivyo hodari kitandani. Yasalie kuwa kati yenyu tu.
Usimwambie mtu kumtongoza mkeo ama mumeo kama njia ya kudhibitisha kama ana uaminifu.
Usimwambie yeyote kuhusu makosa ya zamani ya mwenzio.
Usiwahi kuwaambia majirani au familia kuhusu uwezo wa mumeo kifedha.
Usimwambie mtu kuhusu jinsi mumeo au mkeo ni mdhaifu kitandani, watakuaibisha kwa kumcheka.
Usiwaaambie watoto kuwa baba au mama yao ni mtu mbaya.
Usiwe na mazoea ya kutangaza kwa urahisi shida, au tofauti zenyu. Watatumia nafasi hiyo kuwatenganisha kabisa.
Usimwambie hata mchungaji wenu kuhusu jinsi mvavyokwaruzana nyumbani, wengine watatumia hiyo katika kuandaa mahubiri.
Usiwahi kumwambia mama mkwe kuhusu kiwango cha pesa ambacho mumeo hukupa,
atakuwa na kinyongo bure.
Usiwaambie rafiki zako kuhusu jinsi mkeo au mumeo alivyo na tabia mbaya, fanya kila njia kuibadilisha tabia hiyo.

Hakuna ndoa hata moja duniani ambayo haina panda shuka, inahitaji wawili kulainisha tofauti zao na kufurahia maisha kama wanandoa.

Je, wajua kuwa ndoa tu ndiyo shule ambapo unapewaa cheti cha kufuzi kabla kuanza ya masomo na mtihani? Kila mmoja awe tayari kuchunga na kutunza uhusiano wake kikamilifu.
 
safi sana,haya mimi nayafanya
 
Pana watu wanatabia ngumu kuishi nao. Yaani unabeba madhara ya malezi mabovu ya mama yake, wakati wewe unaumia kihisia mama yake ameutua mzigo kwako kwa wewe kukosea kuoa. Huwezi jua tabia za mtu hadi uishi nae.
Ndio maana ma Kanali tunawaambia hakikisha mwanamke unayetaka kumuoa walau umekaa nae miezi 6 kinyumba ili kupima akili yake na uvumilivu wake bila yeye kujua. Kuna wanawake ni mafutuza sana yani ndani ya muda mchache sana anakuwa kashabadilika hana adabu au tabia hatarishi kama umalaya na uvivu zishajidhihirisha.
 
Nakubali hili bora kuishi nao uchumba sugu kwanza miezi mitatu mingi ni majibu.
Ukijiridhisha ndo unafunga nae ndoa.
Bila hivyo malezi mabovu ya mama yake kwake yatakuwa ndio chanzo cha magonjwa mbalimbali kwako pressure,sonona,stress,umasikini wako ( nyumbani kama pana vurugu mwanaume hawezi pata pesa).
Moyo wa mwanaume hauwezi imiliki makelele au kauli chafu za mwanamke aliyeyelewa vibaya.
 
Ni kweli kabisa Mkuu na hiyo ya kupeleka matatizo kwa viongozi wa dini wasuluhishe walio wengi wanajikuta wanapata tamaa badala ya kuleta maelewano huishia kutembea nao hao wake wa wanaopeleka matatizo na ikibidi kuwapokonya kabisa ambapo yule mtoa kesi anabakia na majuto.
 
Pana watu wanatabia ngumu kuishi nao. Yaani unabeba madhara ya malezi mabovu ya mama yake, wakati wewe unaumia kihisia mama yake ameutua mzigo kwako kwa wewe kukosea kuoa. Huwezi jua tabia za mtu hadi uishi nae.

Hii imemkuta mtu wangu karibu. Mbaya zaid mama hasemi, anakuacha upambane na mzigo wako.
Kama ni mwanaume kuwa na msimamo. Msimamo tu ndio utakubeba.
 
Ni kweli,usipokuwa na msimamo utayumba sana kwenye kila kitu...
 
Hii imemkuta mtu wangu karibu. Mbaya zaid mama hasemi, anakuacha upambane na mzigo wako.
Kama ni mwanaume kuwa na msimamo. Msimamo tu ndio utakubeba.
Msimamo haubadilishi tabia ngumu ya mke aliyepata malezi mabovu.
Pana wanawake wababe ukorofi upo ndani mwao, ngumi zinalika,wanahasira kuliko shetani, mshipa wa aibu ulishakata kubwatuka kukuaibisha kukuvua nguo mbele za watu kwake ni SAwa na kunywa maji.
Chaguzi ni tatu kwako.
1.Uwe na hekima mambo yaende
2.Ubebe begi ufungashe
3.Uoe mke wa pili dawa ya mwanamke mkorofi ni mwanamke mwenzake.
 
Mwanamke wa hivyo atakuonyesha ukorofi ukilega, ukimpa nafasi, ukionyesha kumuogopa. Hakika utachapika
Lakin ukiweka mipaka ukawa mkali, ukorofi atauonyesha nje, akija kwako hovyo vitu ataficha.

Hawa viumbe huwa wanachagua wa kuwafanyia hivyo vituko. Akikuona mkali anapunguza
 
Hapa shida ni swala la malezi upande wa mwanaume.
Haya mambo uwakuta
1.Wanaume wasomi waliostarabika wakaingia cha kike kukosea kuoa.
2.Watu wa maadili ya dini.
Mwanamke mkorofi anatakiwa akutane na mwanaume anaevuta bangi,ngumi mkononi neno moja la pili ngumi.
Wanaume waliostarabika ndoa zao pasua kichwa wake zao mzigo.
Ukiona boss mkorofi jua anatawaliwa na mke wake yaani nyumbani moto ule ukali ni kujaribu kuijaza ile nafasi ya uanaume aukosao nyumbani,hii ni real research.
 
Ndoa za siku hizi zina Siri?
Kila kinachpikwa kiko Watsap status..
Wakinunua Kochi liko watsap status..
Mtoto akicheka watsap status
Wakigombana kidogo Tu unaona watsap status...

Siri zipi hizo wafiche?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom