Kabla hujaziruhusu hasira ndani yako jifunze kitu hapa...

Denis1729

Member
Sep 9, 2021
34
109
Hasira ni hisia zilizoshindwa kujikabili baada yakufanyiwa au kufanyika kitendo kinachoaminiwa si cha kiungwana kwa mtendwa au mtendewa.
Hasira ni hisia kama namna tumejifunza kuwa hisia ni matokeo.

Kundi kubwa la watu wenye kushindwa kuzikabili hasira ndani yao huwa ni wenye kupata majuto sana ambayo awali hawakuyafikiria au kudhania ingewezekana kutokea

Hasira hazijawahi kuwa zenye faida kwa namna yoyote ile kwenye maisha ya mahusiano hata ndoa.

Kuna hasara na athari nyingi sana zitokanazo na hasira,
ikiwemo;

1.Kuvunjika kwa mahusiano au ndoa

Kwenye hasira kuna maneno mengi yanatolewa yenye kukwaza wenza,
na endapo inakuwa ni muendelezo wa mara kwa mara basi hujikuta inafikia mwisho wa uvumilivu na kuamua kuachana na mwenza.

2.Hushusha thamani pamoja na hadhi yako

Hasira zinaposhindwa kukabiliwa kinywani hutoka maneno mengi yaliyokosa stara na kuvuka mipaka ya heshima iliyokuwa imejengwa kabla, hivyo unaporuhusu tegemea baada ya hapo kutokewa na nilichokibainisha.

3.Kuwa hatiani kisheria

Hapa ni wale wanaoshindwa kabisa hata kujikuta wakijichukulia sheria mkononi,
ya kuwapiga hata kuwaua wenza wao walionao kwenye mahusiano au ndoa.

4.Chanzo cha kuyumba kimaisha/kupoteza baraka

Kutokana na hasira watu wengi hujikuta wakiwapoteza watu sahihi ambao kipindi cha uwepo wao pamoja hawakuwa wenye kuwasaidia pesa,
ila mawazo yao wanayoyatoa ilikuwa ni sehemu ya chanzo cha hatua za kimafanikio,
pale hasira zinaporuhusiwa kwa fikra hujikuta wakibaki wenyewe hata kufikia kushuka kiuchumi kwa kuwa yule aliyekuwa akimpa muongozo au alikuwa akifanyika baraka kwenye maisha yake si mtu tena aliye sehemu ya maisha yake.

5.Hubadili tabia zilizo zoeleka

Hasira hufanya watu kuachana kama nilivyoeleza awali,
ndani yake baada ya muda watu hujikuta kukosa kabisa aliye mwenye upendo wa dhati kulinganisha na yule aliyesababisha aende kufikia kujikatia tamaa na kupelekea kujikuta kuanza kufanya tabia ambazo awali hazikuwa sehemu ya maisha yako kwa jumla kutokana na majuto.

6.Hujenga hofu na kutokujiamini

Unapofikia kushindwa kujizuia kuhusu hasira zako maana ake ni kwamba unamjengea hofu mwenza kwenye kuondoa imani ya hatima kuhusu mahusiano,
kudumu kwa furaha na amani ndani yake muda ambao anaendelea kuwa karibu nawe,
hivyo utamfanya asiwe mwenye kujiamini kwako na itamfanya akosee zaidi.

Je,
hasara au athari ipi ya hasira unayoifahamu kwenye mahusiano au ndoa?
Share nasi kwenye comment

Nakukumbusha pale unapoona umeshindwa kuzizuia hisia zako basi na kuruhusu hasira basi ni vyema kujipa utulivu kabla haujazungumza au kuchukua hatua yoyote ile dhidi ya mwenza wako,
Waliosema "hasira ni hasara"
walikaa na walitafakari athari zake

Hasira siyo suluhu kwa mwenza kukuelewa,
na utambue mahusiano au ndoa hayahitaji usiriazi huo kwenye kila kosa kutokea kwa mwenza wako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom