Usikubali kufanywa 'Bakora' ya wapendanao...!

Kigarama

JF-Expert Member
Apr 23, 2007
2,492
1,230
Katika hatua za mapenzi kwenye mahusiano hakuna hatua ambayo ni tata kama pale kila mmoja anataka kutoka kwenye mahusiano yaliyopo lakini anajikuta anamhitaji mwenzake kwa ajili ya maisha "halisi" hivyo inambidi kubaki. Katika hatua hii ndipo baadhi ya wanandoa au walio katika mahusiano hutamani kuwa na mahusiano na watu wengine.

Lakini mahusiano hayo huwa si yale yenye lengo la kwenda mbele zaidi kwenye kuvunja mahusiano ya awali badala yake mahusiano hayo (yanaweza yasihusishe ngono) hutumika kujenga wivu kwa mume/mke au kwa Girlfriend/Boyfriend ili kufufua upendo uliopotea.

Bahati mbaya kuna watu wakiingizwa kwenye mahusiano ya aina hii wao hutaka kujenga kiota na kutamani kumpindua mhusika mpenzi wa awali. Haiwezekani kumpindua na katika mahusiano hatari na yenye kuchosha ni haya ya kuingilia kati uhusiano wenye upendo uliofiifia na wewe ukadhani utaweza kuteka moyo wa yule mliye kwenye mahusiano naye.

Kiukweli wewe unatumiwa kama Bakora tu ya kumchapia mpinzani wa huyo anayejidai uko naye kwenye mahusiano wakati yeye lengo lake ni kukutumia wewe kama silaha ya kumrejesha mpenzi wake anayeonekana kumponyoka.

Jihadhari!!
 
Kwangu hii ni thread ya mwaka...baeleza labda bata kuelewa...Lol...jina lingine ni mapozeo!
 
hapa mie na deklea interesti,
hii iliwahi kunikuta miezi kadhaa iliyopita.

bi dada nilirusha ndoano, kawa nasuasua baada ya kumsarandia sana akanikubali,
tumeenda kidogo ndo akatoboa siri kuwa jamaa yake kamkwaza sana ndo maana kanikubali,
mie nikawa nambembeleza / kumfariji/nikumwahidi mabaya aliofanyiwa sitamfanyia (hapa alinieleza aliyoyakuta kwa mshkaji wake) Inaelekea alimpenda sana huyo jamaa.

dah siku ya siku ananiambia jamaa kaja kuomba msamaha na anampa last chance, du nikaumia lakin nikasema no sweti nikaendelea na maisha.

nikasema mtu alieachika/ anaekaribia kuachika mie NO
 
ilikuwaje mzee,.uliinjoi kwa nuda gani. Lakini mzigo si ulikula!??...
 
ahahaaa acha kunitishia bwana
sasa vitu vipya utatoa wapi?
 
ahahaaa acha kunitishia bwana
sasa vitu vipya utatoa wapi?
hapa lazima awe keshaachika kabisa, na nijiridhishe hatorudi tena,
vinginevyo wanakuja na gia za ajabu ajabu ooh unajua yy ndo men wangu wa kwanza alienitoa naniliu sitaki kumpoteza!!!! agrrrh,
sio ambao hatujawah kukata ribon tuna kaz kweli !!!
 
ilikuwaje mzee,.uliinjoi kwa nuda gani. Lakini mzigo si ulikula!??...
ilikuwa km miez 4 hiv pamoja na ile ya kuzungushwa kabla jamaa hajarudi na kupiga goti ili asemehewe.

Mie bi dada nilimpenda coz hakuwa mtu wa vinyongo na alikuwa rahis sana kusamehe, nikataman niwe nae.

Mie mambo ya kula mzigo hayakuwa kipaombele saaaana!!!
si unajua tena hauwezi kuanza urafiki ambao unataka mtu awe mke uache kupiga muhuri wa certification kuwa the product is ok for use!!!!Hapa nilikuwa naangalia km product ni original au mchina product.
 
ahahaaa acha kunitishia bwana
sasa vitu vipya utatoa wapi?
Wanaume huwa hawatafuti upya wa mwili Smile, bali upya wa mitazamo na utayari wa kuishi pamoja kwenye shida (?) na raha!!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom