AlmightyGod
Member
- May 21, 2023
- 94
- 347
Habari wanajamii,
Hili suala sasa limekuwa likinitatiza sana na kunipa hofu sana kwa kipindi kirefu mno sana.
Hapo awali nilikua na mahusiano na binti flani hivi na tulipendana sana katika mahusiano yetu, Kila mmoja alimweshimu na kujali hisia za mwenzake hata ilifikia kuamua kuishi pamoja kwa kipindi cha miaka mitano(5) na kila mmoja wetu alifahamika kwenye familia za wazazi wa pande zote mbili(2) mapenzi yalikua yameshamiri sana upendo wa kweli ulionekana baina yetu.
Tulijiwekea mipango mingi sana hapo mbeleni na baadhi tulishaanza kuifanyia kazi na ilifanikiwa kwa asilimia kadhaa hivi hadi pale ilipotokea upande wangu kusimamishwa kazi ndipo mipango michache haikuweza kusonga kutokana na upungufu wa kipato, Lkn mwanaume sikusita kupambana zaidi ili nimtimizie mwenza wangu mahitaji yake na siku ziweze kuendelea kwani nilitambua kutokua na ajira sio mwisho wa maisha wala mahusiano yangu kwa ujumla.
Pamoja na jitihada zangu zote zile sikua nafahamu nini kinachofuata mbele yangu, Ilikua bahati sana kufikia mwaka wa tano(5) kwenye mahusiano yetu binti alishika ujauzito na aliniambia hili mapema na mimi nikalipokea kwa furaha sana hata kuongeza juhudi za upambanaji sana mwenza wangu asijekuwa mtu wa mawazo na wasiwasi kulingana na hali aliyokuwa nayo kipindi hicho.
Ila kitu ambacho kilijitokeza na kufanya moyo wangu upasuke na kuogopa kuingia kwenye mahusiano tena ni yule binti alinisaliti na kukimbia na ujauzito wangu na kutokomea nchini Finland na mtasha mmoja hivi pasipo taarifa kwangu wala kwa wazazi wake, kwasababu jambo la kwanza nililofanya baada ya kukimbia na huyo binti niliwasiliana na familia yake(wazazi) ila majibu walionipa ni kuwa hawafahamu lolote lile juu ya hili, Kwakweli niliumia sana.
Zikapita siku, miezi na miaka miwili mbele nikapokea simu siku moja(1) Jumapili majira ya saa nne(4) asubuhi na namba ngeni kupitia WhatsApp video call na mimi sikusita kuipokea ila nilishangazwa kuona ninae zungumza naye alikua ni yule mpenzi wangu alienikimbia pasipo taarifa. Basi mwanaume nikakaza nafsi na kuzungumza naye kwa utulivu kabisa ndipo aliponiambia alijifungua salama na alipata mapacha wakiume na wakike ambao amewapa majina Allan na Mishell hili likanipa furaha sana moyoni.
Maongezi yaliendelea nikimsihi arudi nyumbani lakini sikuweza kumshawishi kamwe, kwani alisema tayari anauraia pacha na watoto sii watanzania na hataweza kurudi huku kwa sababu hiyo, Dah! Niliumia sana moyoni na ukazidi kuvunjika sana.
Hii ndio sababu iliyonifanya kubaki kuwa bachelorhood brother mwenye upweke moyoni hadi hivi leo na sifikirii kuingia penzini ilihali maisha yamenyooka sasa lkn hofu yangu ni kutendwa na binti mwingine kwa mara ya pili.
NAOMBENI USHAURI NINI NIFANYE JUU YA HILI; JE NIUFUNGUE MOYO WANGU TENA?