USHUHUDA: Safari yangu katika hatua za kupunguza uzito wa mwili

annahprosper

New Member
Jul 24, 2021
1
4
Kumekuwa na wimbi kubwa la watu naweza kuwaita ni wafanyabiashara wakitumia fursa hii ya kuelimisha ni jinsi gani unaweza kufanya ili upunguze mwili. Wengine wakitoa mbinu za kupunguza kutambi wengine mikono n.k lakini utaenda nao sambaba mwisho wa siku hawakupi zile hatua unazotakiwa kufuata mpaka ulipie mafunzo kwa kupitia namba wanazoweka mwishoni kama ukihitaji.

Katika historia hii naamini inaenda kubadilisha maisha yako bila kutumia gharama zozote zile na hatimae utaweza kufanikiwa kabisa kupungua na kupata kilo unazotaka.

Kwa majina naitwa Annah Moshi nina miaka ipatayo 32 sasa na nimekuwa muhanga wa jambo hili kwa muda mrefu sana. Kwa sasa nina kilo 93 kutoka kilo 126 na nina mwezi wa 6 toka nimeanza programu ambayo niliona itanifaa mimi na hata wengine wenzangu na mimi bila kutumia gharama kubwa na kuathiri mfumo mzima wa upangiliaji wa chakula nyumbani kwako.

Hivyo bado naendelea nayo na mpaka sa hii nimeweza kufanikisha kutoa kilo 33 na bila kuonesha kuchoka au kupauka.

Lakini pia huwa nafanya na mazoezi hasa kukimbia na kuruka kamba na ninafurahia maisha kabisa hivyo nimeona niwashirikishe na wadau wengine kama mimi tuweze kusaidiana katika hili jambo

IFUATAYO NI MILO YA KUFUATA

ASUBUHI

Matunda aina yoyote isipokuwa ndizi na parachichi au mbogamboga. Huna uwezekano wakupata matunda usikae njaa kabisa kunywa uji wa dona robo lita na sukari weka kijiko 1cha chai.

MCHANA
Kula chochote unachotamani kwa wakati huu ila kwa kiasi huu ni muda wa kujidai

JIONI
Fanya kama ulivyofanya asubuhi ila ni vizuri ukanywa na maji ya vuguvugu yaliyotiwa limao na kama una madonda ya tumbo juisi ya matango kama huna namna ya kufanya juisi, kula matunda yenyewe nanasi, matikiti, machungwa, matofaa, mapapai ndo yanayopendekezwa. Itakufaa kunywa na maji ya kutosha kwa kila mlo ufanyao.

Kwa hiyo;
Ukifuata mlolongo huu utakuwezesha kupungua kila siku wala hautaongezeka tena na utashangaa na tumbo litakavyopukutika ila ukitaka matokeo ya haraka ufanye mazoezi pia angalau nusu saa kwa siku. Lakini pia siyo lazima kama huwezi

Asanteni sana ukihitaji maelezo simu no 0712857801. Ushauri ni bure kabsa.

IMG-20200101-WA0003.jpg
20210701_124443.jpg
20210701_154325.jpg
20181201_143330.jpg
 
kwani ni makosa kufanya hvyo
Si makosa. Inategemea na lengo lako la kujiunga humu. Kama hutukani viongozi wala kusema siri zako za ndani huna haja ya kujificha. By the way hongera sana kwa kupunguza kilo. Kwa nini kwenye program yako mlo nisile parachichi?
 
Si makosa. Inategemea na lengo lako la kujiunga humu. Kama hutukani viongozi wala kusema siri zako za ndani huna haja ya kujificha. By the way hongera sana kwa kupunguza kilo. Kwa nini kwenye program yako mlo nisile parachichi?
Parachichi ni zao la protein mkuu ivyo unaongeza mwili kwa kas sana
 
Si makosa. Inategemea na lengo lako la kujiunga humu. Kama hutukani viongozi wala kusema siri zako za ndani huna haja ya kujificha. By the way hongera sana kwa kupunguza kilo. Kwa nini kwenye program yako mlo nisile parachichi?
Na kwanini utukane kiongozi wako?
Kwani huwezi kutoa Hoja zikasikilizwa bila tusi?

Kukua kiakili huendana na hekima
 
Back
Top Bottom