Mwezi wa pili wa juhudi ya kupunguza uzito wa mwili; umegoma kuleta matokeo. Tatizo ni nini?

Covax

JF-Expert Member
Feb 15, 2021
6,275
21,448
Kama nilio anza juhudi zangu za kupunguza uzito, huu ni mwezi wapili kwa kutumia mfumo ule ule wa kula mlo moja mboga za majani sana na kuepuka vyakula vyenye wanga sana kama chapati ugali na chapati. Mwezi wa kwanza matokeo yali patikana kwa kupungua 8kg.

Kwa kuendelea na utaratibu huo huo mwezi wa pili nimepima leo matokeo ni kwamba ni mepungua 0.5kg nusu kg tatizo ni nini? Mwili umezoea huo mfumo kuna haja ya kubadili diet au mfumo na mda wa kula?

Target yangu ni kumpungua 20kg ndani ya mwezi mitatu ila naona mwezi wa pili nimepunguza nusu kilo tu, na bado nimebakiza mwezi moja. Kila ninapoweka juhudi za kupungua uzito, ndio naongezeka!
 
Kinachonenepesha ni wanga, sukari na mafuta.

Acha kabisa kula wanga kwa mwezi mmoja- mlo wako uwe mbogamboga, nyama, samaki, dangaa, matunda. usitumie kabisa sukari. nyama isiwe ya mafuta mengi. kunywa maji kulingana na kiu yako. Jaribu hiyo then ukuje utuhabarishe
 
Mbona ni metumia hivo hivo soma uzi wangu kwa makini kisha utowe maoni yako.
 
Hapana haujagoma kuoungua na upo vizuri mbona na HONGERA. jielimishe unapoanza safari ya kupunguza mwli jinsi mwili unavozipunguza kilo za uzito, ni suala la hatua kwa hatua sio kama unavotaka wewe.

Huo mwezi wa kwanza mwili ulianza na kupunguza maji (water loss) na ndio maana kilo nyingi zaidi zilipotea. Kadiri muda unavokwenda uzito unaoupunguza lazima ueende unapungua na kuwa unaoteza kidogo.

Pia angalia ulianza na uzito kiasi gani, Mweznye uzito mkubwa sana atapoteza kilo nyingi sana tofauti na mwenye uzito wa wastani au uzito kidogo. Mwwnye kingi atapoteza kingi na mwenye kidogo atapoteza kidogo.

Pia tumia body mass index BMI kwa kulinganisha urefu na uzito wako.
 
Maoni yangu ni kama ifuatavyo

1. Ku skip milo pekee sio sababu ya kupunguza uzito. Unaweza kula ratio kidogo ukala mara kadha. Kunywa maji glasi 2 kabla ya kila mlo.

2. Unatumia kilevi? Maana hua inachangia kuwa na uplanned consumtion/appetite ya kula zaidi ya unachotaka.

3. Labda umeweka focus sana kwenye matokeo (kupungua uzito) kuliko mchakato au day by day progress ya kupungua uzito. Please keep more focus on the process rather than the outcome.

4. Unaweza nikosoa ila kupungua kg 20 kwa miezi mitatu inaweza kuwa ngumu ukizingatia harakati za kila siku za kutafuta maisha. Tunakua occupied na mambo mengi ya lazima. Mf kazi, familia, etc.

5. Nakushari badilisha mentality ya approach yako isiwe tu kupunguza uzito bali iwe kama lifestyle.

6. Mwisho kuna mambo yaliyo nje ya uwezo wetu mfano vitu kama genetics za mtu husika, kuwa na historia ya uzito mkubwa kwenye bloodline yenu etc.

All the best, najua wajuvi watakupa dondoo nyingine zaidi
 
Mkuu kweli kwa mwezi mzima upunguze nusu kilo huo naona kama sio trend sahihi bora zingepùngua kilo mbili my BMI sio mbaya japo nataka kupungua zaidi ya huo uzito.
 
Kinachonenepesha ni wanga, sukari na mafuta.
Acha kabisa kula wanga kwa mwezi mmoja- mlo wako uwe mbogamboga, nyama, samaki, dangaa, matunda. usitumie kabisa sukari. nyama isiwe ya mafuta mengi. kunywa maji kulingana na kiu yako. Jaribu hiyo then ukuje utuhabarishe
Kwani maji pia yananenepesha? Naona umemwambia anywe kulingana na kiu yake.
 
Kuna jamaa yangu aliniambia kama nataka kupunguza uzito nikakope benki. Jokes mkuu. Uko vizur we endelea komaa hapo hapo
 
Kama unakunywa pombe sidhani kama utafikia lengo! Unapiga mazoezi then unaenda kula kitimoto au nyama choma unashushia na bia?
 
Natafuta dawa ya kuongeza unene...msaada tafadhari....pole mtoa mada
Heheheee! Usithubutu kuongeza mwili kwa style yoyote ile, wembamba sio adhabu, sio kilema wala sio ugonjwa. Mimi nilikuwa mwembamba hadi watu wananitania chikondemu ila sasa ninamwili hadi natamani wembamba wangu, unene ni mateso mzee
 
Mkuu kweli kwa mwezi mzima upunguze nusu kilo huo naona kama sio trend sahihi bora zingepùngua kilo mbili my BMI sio mbaya japo nataka kupungua zaidi ya huo uzito.
Sasa mkuu unataka kuoingana na mfumo mwili unavojiendesha, nikivokueleza hapo juu ndivyo ilivyo mzee.

Elewa unapoanza safari ya kupunguza mwili ujue vitu unavopunguza ni MAFUTA (fats), MUSCLE, na WATER (maji). Cha kwanza kupungua huwa ni maji wanaita water loss.

Huo mwezi wa kwanza uliopteza hizo kg nyingi hayo yalikuwa ni maji, upunguaji wa maji huwa ni wa kasi na mkubwa ukilinganisha na upunguaji fats mafuta.

Huo mwezi wa pili unaolalamika ulipoteza kidogo sana ndio umeanza kupunguza mafuta fats. (Upunguaji wake ni wa polepole sana na kidogo).

Afu upunguaji wa kasi wa uzito wa mwili kama utakavyo sio salama kwa afya yako.
 
Kama nilio anza juhudi zangu za kupunguza uzito, huu ni mwezi wapili kwa kutumia mfumo ule ule wa kula mlo moja mboga za majani sana na kuepuka vyakula vyenye wanga sana kama chapati ugali na chapati. Mwezi wa kwanza matokeo yali patikana kwa kupungua 8kg.

Kwa kuendelea na utaratibu huo huo mwezi wa pili nimepima leo matokeo ni kwamba ni mepungua 0.5kg nusu kg tatizo ni nini? Mwili umezoea huo mfumo kuna haja ya kubadili diet au mfumo na mda wa kula?

Target yangu ni kumpungua 20kg ndani ya mwezi mitatu ila naona mwezi wa pili nimepunguza nusu kilo tu, na bado nimebakiza mwezi moja. Kila ninapoweka juhudi za kupungua uzito, ndio naongezeka!
Kinywa maji yam moto, yachemshe kama ya chai lakini usitie kitu, maji tu.

Kabla hujala kitu hakikisha unapata lita moja, kianzia hapo mpaka inapofika saaza chakula cha mchana, hakikisha umeshapiga lita nyingine moja. Baadaya chakula cha mchana piga lita mpoja. Baada ya chakula cha usiku, kabla hujalala hakikisha lita nyingine moja.

Usinywe tena maji ya baribi, fanya maji ya moto ndiyo maji yako. Utakojowa kwa wingi na unene utakutoka tu, na maradhi mengine yoyote yataondoka. Inaitwa "hot water therapy".
 
Maoni yangu ni kama ifuatavyo

1. Ku skip milo pekee sio sababu ya kupunguza uzito. Unaweza kula ratio kidogo ukala mara kadha. Kunywa maji glasi 2 kabla ya kila mlo.

2. Unatumia kilevi? Maana hua inachangia kuwa na uplanned consumtion/appetite ya kula zaidi ya unachotaka.

3. Labda umeweka focus sana kwenye matokeo (kupungua uzito) kuliko mchakato au day by day progress ya kupungua uzito. Please keep more focus on the process rather than the outcome.

4. Unaweza nikosoa ila kupungua kg 20 kwa miezi mitatu inaweza kuwa ngumu ukizingatia harakati za kila siku za kutafuta maisha. Tunakua occupied na mambo mengi ya lazima. Mf kazi, familia, etc.

5. Nakushari badilisha mentality ya approach yako isiwe tu kupunguza uzito bali iwe kama lifestyle.

6. Mwisho kuna mambo yaliyo nje ya uwezo wetu mfano vitu kama genetics za mtu husika, kuwa na historia ya uzito mkubwa kwenye bloodline yenu etc.

All the best, najua wajuvi watakupa dondoo nyingine zaidi
Mkuu ahsante kwa ushauri wako mzuri reaction yangu ni hi.
1. Sinywi pombe au kilevi chochote.
2. Kazi zangu ni za kukaa sana sina mda wakutembea kwa miguu siku nzima.
3. Napenda sana ku-compose kwa kulala au kukaa kimya kwa mda mrefu.
4. Spendi kula nje ya nyumbani na nyumbani na kula mboga mboga sana na ugali kdgo.
 
Back
Top Bottom