Ushirikina (Ujinga) karne hii

Mr Kijoka nadhani hujaelewa mtoa mada anachozungumzia, maana point zako zinalenga kumkabili bila yakuelewa anacho maanisha, nadhani point sio kukashifu imani za watu wala kuziona hazifai ila swala muhimu hizo imani zina uelekeo mzuri kwa jamii? Hebu fikiri mtu anakutwa na ngozi ya mwanadamu mwenzake je hiyo imani ni sawa?
Kamwe hatuna mamlaka ya kuingilia imani za watu ila na wao imani zao hazina mamlaka ya kuifanya jamii iwe na hofu kwao,,, uchawi wa kukata viungo vya binadamu mwenzako huo ni upuuzi tena ni zama za giza kabisa!

Tafuta sehemu ambayo nimesapoti uchawi, au nimeunga mkono mauaji ya kikatili...
We nawe hebu acha kukurupuka kama Kibonde lool
 
So jifunze kuheshimu imani za watu kama ambavyo wenzako wanavyokuheshimu wewe na imani yako hiyo uliyoletewa na mkoloni na kisha kuitupilia mbali imani yako ya asili....

Mkuu Gang Chomba labda na mimi sikukuelewa, lakini kweli unaweza kusimama mbele ya kadamnasi na kutetea haya aliyosema mleta mada (yaani ushirikina kama viungo vya albino, viungo mbalimbali vya watu wa jinsia zote, ngozi ya binadamu na wiki hii, VIUNGO vya watoto njiti na maiti za vichanga unaweza kupaka picha moja chafu kwelikweli kuhusu UJINGA ULIVYOKITHIRI katika jamii ya Watanzania) kwa kutumia pazia la kumini? I don't think so mkuu. Hizi imani inabidi zipigwe vita vitakatifu.
Hizi imani ndizo zinazochangia kumrudisha nyuma Mtanzania wa kizazi hichi hatuna haja ya kuzikumbatia kwani tuliona yaliyotokea kwa mabibi zetu kule kanda ya Magharibi kwa sababu ya ushirikina, ambako inaamika zaidi ya watu 20,000 haswa (mabibi kizee)waliuwawa.
In 1987, Raisi mstahafu Ally Hassani Mwinyi aliwaasa wenyeji wa kanda ya magharibi kwa kuwambia,

"You are killing innocent women, some of them your own mothers, grandmothers or old
people who have all along taken good care of you: how come they suddenly become
witches? Do (you) pay them back by killing them?"


Haya ndiyo madhara ya ushirikina anayoongelea mtoa mada (Double Seven).
 
hivi kwa nini masharti ya ushirikina always ni magumu na yakikatili.......kwa nini siku moja sharti lisiwe, nenda kale korosho? au sharti mkonyeze demu bomba? au sharti imba ule wimbo wa ABCD?

Mkuu elewa kuwa shetani hana hukumu ya mwisho. Hivyo ndo maana hutoa adhabu na masharti instantly. Hizo imani zote chanzo ni shetani.
 
Mimi naona yote hii yatokana na watu kua watupu rohoni ama kichwani na kutojiamini. Ili kukidhi haja zao ambazo hawana uwezo nazo ndio maana wanaamini kufanya hivyo vitu ama kuabudu hivyo vitu. Imani inaleta uhuru, mategemeo mazuri, faraja ya kimawazo na afya njema. Hivi ni vitu ambayo binadamu yeyote anatarajia na kupenda kua navyo.

Hivyo ni jukumu letu kuwasaidia wanaoamini kuua vitoto, ama viongozi wanakimbilia kuagua ama kujizindika, nk na tukawaombee ili noa wamjue bwana - kwa maana ya kwamba tuwasaidie kubadili imani yao ya kitaboo (taboo zingine zinatisha) na wajiunge na imani ya kumjua bwana wao wa kweli. Wakishamjua bwana wala hawatamdhuru albino wala nani, hawatasoma abadiri, wala hawatakua na visasi na yeyote, mioyo yao itajaa furaha na kujiamini zaidi na watategemea utashi wa akili zao kutafuta suluhu ya matatitizo yao ama na kuongoza watu wao. Kwa kufanya hiyvo watakua wanaabudu ama kuamini kama binadamu wengine wenye akili timamu.
 
Akili za binadamu zinatakiwa ziwe huru na tena ziwe huru kweli kweli.
Ziondokane na vifungo vya imani potofu, waganga wa kichawi, wachungaji wa kitapeli wanaohubiri wokovu kwa kuwanyonya waumini na imani nyingine zote zitakazoangamiza miili na roho zao.
 
Yaani ni kweli kabisa, na ndio maana tunaendelea kuwa masikini.Taifa gani litaendelea kwa kuamini imani za kishirikina? Kuanzia Viongozi mpaka wananchi wa kawaida wote ushirikina.Taifa hilo litazidi kuwa masikini milele na milele kwa sababu Mungu ameshalipa kisogo na hatutapata neema ya Mungu.Mpaka tubadilike ndio tutaona maendeleo ya kweli lakini kama tutaendelea hivihivi hatufanyi vitu mpaka ukacheck "jamaa" walai hatutaendelea.

TUtaishia kuwa kama Haiti
 
Back
Top Bottom