Ushindi wa CCM Igunga: Mchango wa Nape Ulikuwa ni nini?

View attachment 38433nape hana mchango kabisa ushindi wa Igunga

Hapo ulikuwa Isakamaliwa Igunga

View attachment 38434 UJUE NAPE HAKUKANYAGA KABISAAAAA IGUNGA.....(hapa akiwa sokoni Igunga siku mbili kabla ya kufungua kampeni Rasmi)

Hapo Igunga sokoni

View attachment 38435"ukivaa nenda kashushe ile bendera yenye rangi ya damu Igunga is for CCM"... sawa kamanda soko lote hili Igunga tuna ijua CCM tu wengine hawa wananogesha harusi. rudi tarehe 03/10/2011 kuja kumchukua mbunge wa CCM

Hapo Mbutu Darajani
View attachment 38436wana Igunga msifanye makosa eeeh!!!!

Hapo nyumbani kwa Rostam A

View attachment 38438MMEPOKEAJE KUJIVUA GAMBA IGUNGA?" Ooooh kamanda subiri tarehe 02/10/2011 kama hawajaondoka bila kuaga wala kulipia geusthouse walizolala>>>>>>>>> hahaaaa teh hahaa

Hapo unawaeleza jinsi ulivyolipia pango la CUF

Oooooh pole kumbe nawe imekugusa sana eeeh? Pole sana sana!!!! Si makusudi imetokea bahati mbaya si kukusudia wewe bahati mbaya umepitia hapa.....

mitaani.


Nape fanya kazi moja nyingine kubwa pepeta mdomo magamba waliobakia waamwagike. Lowasa na Chenge watu wanataka mechi nyingine Mwanza na loliondo.

Halafu kuna ile list mpya mwambie mzee wa pipa aanze majungu awamwage ili tuwe na viwanja viwingi. Usijali CCM inakuwa kwa asilimia 85 mpo kwenye njia nzuri. Usisikilize watu eti CCM inaporomoka. Masahani ya pilau na fedha kichele, shule zenyewe za kata. Wananchi wakiona vitambi na mashangingi ya kijani wote wanakubali. Wake za watu wakiwaona vijana mlivyoiva aah makada wenzenu wanakarimu. Kanyaga twende kamanda. Chuo cha propoganda kurasini kilifanya kazi nzuri. Hapa swala ni propoganda kwa kwenda mbele kama waziri wa habari wa hayati Sadam Hussein, aliwaaminisha wa Iraq kwamba Baghad iko salama siku zote. Nakutakia afya njema wapepete magamba wote mechi zianze upya.

Ila inabidi tusaidiane kuwaeleza takukuru kuwa rushwa ni takrima, na matumizi ya watumishi wa serikali na mali za umma haina ubaya kwenye kampeni. Vilevile tuwaambie polisi ukiwa madarakani huna kosa, makosa yote ni ya mtu anayeipinga CCM. Mwana CCM akikuteka, akikuibia ni wewe mwizi. Mwana CCM akivaa kitambaa, au kofia vyote ni hijab na akikiangusha karibu yako umemdhalilisha. Mwana CCM akifyatua risasi ni mpizani kwani bastola zao zina maji. Mwana CCM ruhusa kutembea na silaha ya moto hata kwenye mikutano ya hadhara. Mwana CCM ruksa kumtukana polisi bila kesi. Mwana CCM kulala na wake za watu kisha kumtuliza mume au mume kujikuta anakesi kubwa. Mwana CCM ruhusa kutoa ahadi yeyote ile hata kama ni uongo.

Mwana umaarufu wa CCM unakuwa sana tena sana. Kama hujui muulize Nchemba nini alikifanya Igunga, wake wote wa makada wa CCM wanamfahamu.

Nakutakia kila heri kuvua magamba yaliyobakia kiunoni.

Chief Mkwawa wa Kalenga- Haki na usawa wa sheria hupatikana kwa jasho la damu.
 
Back
Top Bottom