Ushindi arumeru wawachanganya watawala UDOM

Posho City

JF-Expert Member
Mar 15, 2012
646
415
Kuna wanafunzi zaidi ya 25 walisimamishwa masomo katika chuo kikuu cha Dodoma wiki iliyopita tarehe 28.03.2012,sababu ni kuwa waliondoka chuoni wakiwa wamevaa sare za chadema wakienda huko kata ya Chang'ombe manispaa ya Dodoma kushiriki kampeni za uchaguzi wa udiwani,walipofika geti la chuo gari lilikamatwa, likapelekwa utawala,wakalazimishwa kuvaa bendera na kupigwa picha.Kesho yake tarehe29.03.2012 wote walipewa barua za kusimamishwa masomo siku 21.Lakini tofauti na kawaida siku ya jana wote wamerudi chuo kwa kilicho tafsiriwa ni kiwewe cha matokeo ya Arumeru Mashariki.Maana kuna watu wengi wamefukuzwa mwezi wa2 bila sababu hadi leo hawajaitwa,
 
Wekeni bidii kwenye masomo yatawasaidia, msikubali kutumiwa kisiasa na wanasiasa waroho wa madaraka. Huu ni ushauri wangu msije juta. kesho mkidisco mtasema kwa kuwa nyie CDM.
 
unajua ccm sasa kwa hali waliyofikia wanadhani adui yao ni chadema, na nina hakika kwa fikra finyu walizo nazo kamwe hawawezi kufika popote. Wamesahau kuwa adui yao ni umaskini wa watanzania, hali ngumu ya maisha, madadhi, huduma mbaya za jamii kama barabara, maji, elimu, afya na usalama ambapo sasa kila kukicha ni mabomu, vipigo kwa raia nk. Sasa hii ya wao kutaka kupambana na chama dume nadhani inawachimbia kaburi lao wenyewe. Maana kwa sasa chadema ni rafiki ya wanyonge na ccm ni adui ya wanyonge, siku zote mnyonge hukimbilia kwa rafiki yake na si kwa adui yake.
 
Kipenda roho hula nyama mbichi. Hao viongozi wa UDOM wanahangaika tu, kujipendekeza kwa CCM. Aibu tupu.
 
Huo ushauri wako wa wanachuo ku-disco,ungeanza kuwashauri wana vyuo wanaojifanya wakereketwa wa magamba.hata hivyo sijawahi kusikia wame-disco.
 
Msijali 2015 CDM chama tawala, tutawashughulikia wote wanaocha kufanya kazi kwa mujibu wa taratibu na kujipendekeza kwa CCM
 
Udom pamekuwa kama uwanja wa siasa kati ya watawala wapenda magamba na wanafunzi wapenda mabadiliko! Imefikia hatua baadhi ya wanafunzi wanaogopa kuongea hata kwa kudai haki zao za msingi! Mfano; kule EDUCATION wanamsemo wao maarufu sasa hivi wa "utaitwa kuchukua barua yako" hasa pale wanapokuta wenzao wanazungumzia matatizo mbali mbali ya chuo! Na wangi wa wanaofukuzwa kwa sasa wanatokea COLLEGE OF EDUCATION ambapo inaaminika kuwa chadema wameweka mizizi! Ni vizuri mlio karibu na PROF. KIKULA mmshauri aepuke kutumiwa na wanasiasa kwani anadhalilisha taaluma yake!
 
Ccm huwezi ukazuia ufahamu ,UDOM itageuka kata muda simrefu badala ya kisima cha fikra
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom