Ushauri wa bure kwa TFF na Bodi ya Ligi kuhusu utoaji we Tuzo kwa Msimu ujao 2022 / 2023

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,014
16,749
Kura zipigwe na Sisi Wadau wa Soka au na Makocha au na Wachezaji wa zamani na siyo na Watendaji wa TFF waliokaa hapo Karume na Vitambi vyao kama Mapipa ya SIMTANK ndiyo Wachague / Watuchagulie Washindi.

Huwezi kusema kwa Magoli yote yaliyofungwa katika Msimu wa Ligi Kuu Goli la Fiston Mayele ndiyo Goli Bora.

Pamoja na kwamba nashabikia Simba SC, ila nadhani Goli bora ni lile la Kiungo wa Yanga SC Feisal Salum alilotufunga Simba SC au lile la Sakho au la Kichuya ila kamwe siyo la Mayele ambalo Kwangu Mimi naliona ni la Kawaida na hata Wadogo zangu wengi Magomeni, Temeke na Tandika katika Michezo ya Ndondo wanayafunga mno.

Msimu ujao tutachagua Wenyewe.
 
Hiyo ni mistake kubwa hapo ndio utajua timu gani ina mashabiki wengi kati simba au yanga maana kura zitaoigwa kishabiki tuu na mwenye mashabiki wengi atazoa kura zoooote
Kwahiyo unadhani Maamuzi ya kumpa jana Tuzo Fiston Mayele hayakuwa na Ushabiki wa Simba na Yanga?
 
Unahisi ikifanyika hivyo Usimba na Uyanga hautakuwepo??
#Fei aliwafunga FA, Kichuya sijaona goli zuri la kuingia kwenye kinyang'anyiro, Goli la Sakho lipi??? Mechi gani?? Kidogoo Goli la Chrispin Ngushi (linafanana na la Mayele) kipindi hajatua Yanga
 
Kura zipigwe na Sisi Wadau wa Soka au na Makocha au na Wachezaji wa zamani na siyo na Watendaji wa TFF waliokaa hapo Karume na Vitambi vyao kama Mapipa ya SIMTANK ndiyo Wachague / Watuchagulie Washindi.

Huwezi kusema kwa Magoli yote yaliyofungwa katika Msimu wa Ligi Kuu Goli la Fiston Mayele ndiyo Goli Bora.

Pamoja na kwamba nashabikia Simba SC, ila nadhani Goli bora ni lile la Kiungo wa Yanga SC Feisal Salum alilotufunga Simba SC au lile la Sakho au la Kichuya ila kamwe siyo la Mayele ambalo Kwangu Mimi naliona ni la Kawaida na hata Wadogo zangu wengi Magomeni, Temeke na Tandika katika Michezo ya Ndondo wanayafunga mno.

Msimu ujao tutachagua Wenyewe.
Baada ya kupigwa ban umaanzisha mpya siyo.
 
Back
Top Bottom