USHAURI: TRA, Rudisha na kusanya Kodi ilojulikana maarufu kama Kodi ya matching guy Kwa mfumo Bora zaidi

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,560
23,347
Nimekaa nikifikiri Kwa muda sasa ni jinsi Gani mfanyabiashara mwenye mtaji wa 10 ml, alipaye Kodi ya pango ml 2, afanyaye biashara ya stationery, household goods, saluni nk nk awezaje kulipa Kodi ya lak 8, akalipa umeme, service levy, mshahara wa wafanyakazi, maji, taka, akabaki na pesa kulipa Kodi ya nyumba, akasomesha watoto, akalisha family, nk nk na Bado akasave pesa na kukuza mtaji Hadi kutoboa na kuwa tajiri, natatizika.

Watumishi wengi waliokuwa watumishi TRA baada ya kustaafu, wamejaribu kufanya biashara zile zile walizokuwa wakizitoza Kodi, na matokeo yake pia wamekumbana na changamoto kubwa na kulazimika kutumia ujanja ujanja kuendesha biashara kutokana na mfumo uliopo kuzuia kabisa nafasi ya mtu aliyenyooka kutokufika popote.

USHAURI:
1.WANAFUNZI WANAOHITIMU VYUO MBALIMBALI.

Hawa wasilipe chochote Kwa kipindi Cha miaka Mitano Ili kuwapa nafasi ya Kupata uzoefu wa business ideas walizonazo Ili zipate ground na uhalisia Ili waje kuwa msaada siku zijazo.

Makampuni Kutoka nje tumekuwa tukisikia wakipata msamaha wa Kodi, nashauri pia wanafunzi Kutoka VYUO vikuu vya ufundi nk nk,nao wasamehewe.

2. MATCHIN GUYS NA BIASHARA NDOGO CHINI YA MTAJI WA ML 5
Hawa wasajiliwe wote, wapate msamaha wa miaka 2, walipe ada kidogo ya Elfu 50 Kwa mwaka.

Wapewe TIN namba na wawe wakilipa moja Kwa moja kupitia control numbers kupitia simu zao.

3: BAJAJ ZA ABIRIA NA MIZIGO ZA TAIRI 3
Hawa wamekuwa wakilipishwa Kodi za mapato, Kwa maoni yangu, huu ni uonevu, nashauri pia walipe 50 pekee Kwa mwaka, tozo zingine za tarura nk nk zifutwe.

Pikipiki za miguu miwili zitafutiwe namna ya kuondoshwa au kubaniwa lesseni Ili zipungue mtaani Ili kupunguza Ajali.

4. WAKULIMA WADOGO
Wapewe msamaha wa miaka 2 Ili watengeneze uwezo mzuri wa kujisimamia.

Wapewe ruzuku ya mbolea na bank ya KILIMO isogee zaidi Hadi wilayani, wakopeshwe tractors Ili walime KILIMO Cha kisasa.

Nao walipie Kodi moja tu isozidi Elfu 50 Kwa mwaka kulingana na msimu inavyoenda.

5. BIASHARA ZA KATI ZENYE MTAJI CHINI YA ML 20
Hawa wapewe grace period ya miaka 2 bila kulipa chochote, mwaka wa tatu walipie Laki 1 tu Kwa mwaka.

Wafutiwe Kodi za lesseni za biashara na service levy. Nk nk.

6. WAJASIRIAMALI MITANDAONI NA WABUNIFU MBALIMBALI
Hawa wapewe grace period ya miaka 2.

Na baada ya hapa waanze kulipa 50 Elfu Kwa mwaka. Hii itaongeza ushiriki wa wengi kwenye Uchumi na Kodi itaongezeka mara dufu.

7. WAVUVI WADOGO WENYE KUTUMIA MITUMBWI NA MAJAHAZI
Hawa wasilipe sent Tano, wajengewe uwezo, wakusanywe ktk vikondi Ili wakopeshwe boat za kisiasa Ili wavue samaki Kwa TIJA.

Wasitozwe chochote Kwa miaka 5, baada ya hapo walipe 50 tu Kwa mwaka, ushuru ufutwe.

FAIDA ZA KUCHUKUA HATUA HIZO
1. Tax base itaongezeka Kwa biashara nyingi zilizofungwa na mpya zitaanzishwa.

2. Utegemezi utapungua katika JAMII Hasa uchawa.

3. Unemployment rate itapungua, sababu wafanyabiashara hao wakikua watatoa ajira Kwa wengi.

4. Exportation ya bidhaa za ndani itaongezeka.

5. Mfumuko wa Bei utapungua sababu mzunguko wa pesa na biashara utapaa.

6. Pesa za kigeni zitaongezeka sababu ya ukuaji wa biashara ya ndani au domestic trade.

7. Serikali itapunguza utegemezi wa misaada Kutoka nje yenye masharti magumu kwenye budget sababu kuu ni kuwa Uchumi utashirikisha wigo mpana zaidi.

Nakaribisha wadau kuchangia namna Bora ya kunasua uchumi wetu.

Karibu🙏🙏
 
Hizo akili za kuelewa hiki ulichoandika hapa, sidhani kama wanazo. Wenyewe wakiona sehemu kuna mnuso tu, wanaanzisha kodi/tozo.

Hii serikali haijawahi kuwa na kodi rafiki kwa wananchi wake. Kodi zote ni kandamizi tu.
 
Watumishi wengi waliokuwa watumishi TRA baada ya kustaafu, wamejaribu kufanya biashara zile zile walizokuwa wakizitoza Kodi, na matokeo yake pia wamekumbana na changamoto kubwa na kulazimika kutumia ujanja ujanja kuendesha biashara kutokana na mfumo uliopo kuzuia kabisa nafasi ya mtu aliyenyooka kutokufika popote.
Wengi huwa wanazifunga hizo biashara lakini wakiwa wanakusanya kodi wanakwambia unapata faida sn, haswa Afisa wa TRA awe ni mhaya utakoma hizo tambo
 
Kuna polisi alistaafu akajaribu kuwa jambazi aliishia kupigwa risasi na polisi wenzie
 
Watumishi wengi waliokuwa watumishi TRA baada ya kustaafu, wamejaribu kufanya biashara zile zile walizokuwa wakizitoza Kodi, na matokeo yake pia wamekumbana na changamoto kubwa na kulazimika kutumia ujanja ujanja kuendesha biashara kutokana na mfumo uliopo kuzuia kabisa nafasi ya mtu aliyenyooka kutokufika popote.
Wengi huwa wanazifunga hizo biashara lakini wakiwa wanakusanya kodi wanakwambia unapata faida sn, haswa Afisa wa TRA awe ni mhaya utakoma hizo tambo
Hiyo Inaitwa mkuki Kwa nguruwe!!!

Mifumo ya ukusanyaji Kodi iliyopo ni ya copy and paste Kutoka Kwa wakoloni.

Haiakisi uhalisia ktk Uchumi wetu.

Imagine biashara yenye mtaji w ml 15 unaambiwa uajiri mhasibu wa kuandaa hesabu za Kodi na kupeleka return ya Kila mwezi TRA!!
 
Ni ujinga mtupu, huyo mhasibu mwenye CPA utakuwa unamlipa nini?
 
Wanajua Haiwezekani, husema hivyo Ili kutengeneza mazingira ya RUSHWA.

So kama nchi hatuwezi kuruhusu mweneno wa aina hii.

Tubadili mifumo ya ukusanyaji Kodi.

KATIBA mpya ni sasa 2023.
 
Usisahau na leseni ya biashara ya manispaa pia na yenyewe inakwamisha sana wajasiriamali wenye mitaji midogo kuanzia 5m -10m plus iyo YA TRA ya makadirio ya kodi
 
Nimekaa nikifikiri Kwa muda sasa ni jinsi Gani mfanyabiashara mwenye mtaji wa 10 ml, alipaye Kodi ya pango ml 2, afanyaye biashara ya stationery, household goods, saluni nk nk awezaje kulipa Kodi ya lak 8, akalipa umeme, service levy, mshahara wa wafanyakazi, maji, taka, akabaki na pesa kulipa Kodi ya nyumba, akasomesha watoto, akalisha family, nk nk na Bado akasave pesa na kukuza mtaji Hadi kutoboa na kuwa tajiri, natatizika.

Watumishi wengi waliokuwa watumishi TRA baada ya kustaafu, wamejaribu kufanya biashara zile zile walizokuwa wakizitoza Kodi, na matokeo yake pia wamekumbana na changamoto kubwa na kulazimika kutumia ujanja ujanja kuendesha biashara kutokana na mfumo uliopo kuzuia kabisa nafasi ya mtu aliyenyooka kutokufika popote.

USHAURI:
1.WANAFUNZI WANAOHITIMU VYUO MBALIMBALI.

Hawa wasilipe chochote Kwa kipindi Cha miaka Mitano Ili kuwapa nafasi ya Kupata uzoefu wa business ideas walizonazo Ili zipate ground na uhalisia Ili waje kuwa msaada siku zijazo.

Makampuni Kutoka nje tumekuwa tukisikia wakipata msamaha wa Kodi, nashauri pia wanafunzi Kutoka VYUO vikuu vya ufundi nk nk,nao wasamehewe.

2. MATCHIN GUYS NA BIASHARA NDOGO CHINI YA MTAJI WA ML 5
Hawa wasajiliwe wote, wapate msamaha wa miaka 2, walipe ada kidogo ya Elfu 10 Kwa mwaka.

Wapewe TIN namba na wawe wakilipa moja Kwa moja kupitia control numbers kupitia simu zao.

3: BAJAJ ZA ABIRIA NA MIZIGO ZA TAIRI 3
Hawa wamekuwa wakilipishwa Kodi za mapato, Kwa maoni yangu, huu ni uonevu, nashauri pia walipe 50 pekee Kwa mwaka, tozo zingine za tarura nk nk zifutwe.

Pikipiki za miguu miwili zitafutiwe namna ya kuondoshwa au kubaniwa lesseni Ili zipungue mtaani Ili kupunguza Ajali.

4. WAKULIMA WADOGO
Wapewe msamaha wa miaka 2 Ili watengeneze uwezo mzuri wa kujisimamia.

Wapewe ruzuku ya mbolea na bank ya KILIMO isogee zaidi Hadi wilayani, wakopeshwe tractors Ili walime KILIMO Cha kisasa.

Nao walipie Kodi moja tu isozidi Elfu 20 Kwa mwaka kulingana na msimu inavyoenda.

5. BIASHARA ZA KATI ZENYE MTAJI CHINI YA ML 20
Hawa wapewe grace period ya miaka 2 bila kulipa chochote, mwaka wa tatu walipie Laki 1 tu Kwa mwaka.

Wafutiwe Kodi za lesseni za biashara na service levy. Nk nk.

6. WAJASIRIAMALI MITANDAONI NA WABUNIFU MBALIMBALI
Hawa wapewe grace period ya miaka 5.

Na baada ya hapa waanze kulipa 50 Elfu Kwa mwaka. Hii itaongeza ushiriki wa wengi kwenye Uchumi na Kodi itaongezeka mara dufu.

7. WAVUVI WADOGO WENYE KUTUMIA MITUMBWI NA MAJAHAZI
Hawa wasilipe sent Tano, wajengewe uwezo, wakusanywe ktk vikondi Ili wakopeshwe boat za kisiasa Ili wavue samaki Kwa TIJA.

Wasitozwe chochote Kwa miaka 5, baada ya hapo walipe 50 tu Kwa mwaka, ushuru ufutwe.

FAIDA ZA KUCHUKUA HATUA HIZO
1. Tax base itaongezeka Kwa biashara nyingi zilizofungwa na mpya zitaanzishwa.

2. Utegemezi utapungua katika JAMII Hasa uchawa.

3. Unemployment rate itapungua, sababu wafanyabiashara hao wakikua watatoa ajira Kwa wengi.

4. Exportation ya bidhaa za ndani itaongezeka.

5. Mfumuko wa Bei utapungua sababu mzunguko wa pesa na biashara utapaa.

6. Pesa za kigeni zitaongezeka sababu ya ukuaji wa biashara ya ndani au domestic trade.

7. Serikali itapunguza utegemezi wa misaada Kutoka nje yenye masharti magumu kwenye budget sababu kuu ni kuwa Uchumi utashirikisha wigo mpana zaidi.

Nakaribisha wadau kuchangia namna Bora ya kunasua uchumi wetu.

Karibu
Saa100 akifanya hivyo atakosa kodi ya kununulia magoli ya yanga na simba
 
Usisahau na leseni ya biashara ya manispaa pia na yenyewe inakwamisha sana wajasiriamali wenye mitaji midogo kuanzia 5m -10m plus iyo YA TRA ya makadirio ya kodi
Zamani enzi za Nyerere katika kuhamasisha KILIMO, palikuwa na kitu maofisini na wizara ya KILIMO kiitwacho Shamba darasa.

TRA Kila wilaya pia wangeanzisha biashara kutupa mfano tuone uhalishia.

Pia Kuna uozo inaitwa "Service Levy" Hiyo wanafika ofisini, walichukua efd Yako wanaoangalia mauzo Kwa mwaka Kisha unaambiwa, Kwa mauzo haya ya ml 20, lipa service levy 1ml,

Inasikitisha.
 
Saa100 akifanya hivyo atakosa kodi ya kununulia magoli ya yanga na simba
Najiuliza sababu za kuacha kukusanya Kodi ya machinga Ile 20,000 Kwa mwaka na kukimbilia kukopa!!

Anyway, kupunguza Kodi ni kuongeza tax base, idadi ya walipakodi itaongezeka na kuongeza pia makusanyo ya Kodi maradufu kuliko sasa.
 
Hizo akili za kuelewa hiki ulichoandika hapa, sidhani kama wanazo. Wenyewe wakiona sehemu kuna mnuso tu, wanaanzisha kodi/tozo.

Hii serikali haijawahi kuwa na kodi rafiki kwa wananchi wake. Kodi zote ni kandamizi tu.
Itafika time, mikopo itashindikana kulipika, watazikimbia ofisi,

Ndipo tutatafuta viongozi big brains watakapokuja kufufuka threads aina hii na kuzifanyia KAZI.

Pale Uganda, biashara zimechangamka Hasa na hawana bandari.
 
Lipa kodi unayoona unaiweza nyingine tafuta namna mpaka ufanikiwe. Code ni hiyo. Hii nchi unatakiwa kutumia akili sababu adui yako si TRA, adui yako ni bunge lako kupitia wafanyabiashara wenzako wakubwa. TRA wanasimamia sheria ila yule mfanyabiashara mkubwa anayeingiza bidhaa kutoka China na kukupa wewe ndo hataki ukue ulingane naye sababu ya usalama wa soko na faida, anatafuta namna ya kuhakikisha kuna ukuta na ili ufanikiwe lazima uweze kuuruka. Fanya tafiti kidogo utanielewa boss.
 
Kwann nifanye Utafiti wa jambo ambalo tayari umelitafiti?

Fafanua, mfanyabiashara mkubwa mwenye kuagiza china anawekaje ukuta Kwa mfanyabiashara mdogo na WA kati?
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Kwann nifanye Utafiti wa jambo ambalo tayari umelitafiti?

Fafanua, mfanyabiashara mkubwa mwenye kuagiza china anawekaje ukuta Kwa mfanyabiashara mdogo na WA kati?

Ok boss, ntakupa Mfano unaofanana na hivi vikwazo ambavyo wafanya biashara wakubwa wananufaika navyo kupunguza ushindani, Si rahisi hata kama una mtaji kuanzisha biashara mpya. lets say unataka kuwa supplier mkuu heinken beer Tanzania. Yaani wewe uimport halafu usambaze kwa wauzaji wa jumla Tanzania.

Utakutana na ukuta wa vibali, utakutana na ukuta wa sera, utakutana na ukuta wa vigezo vya importation, utakutana na ukuta wa watu wa udhibiti vyanzo vya mitaji, ukivuka hapo mzigo ukafika unakutana na mambo mengine mengi kama stika, viwango vya ubora, utunzaji wa bidhaa za vyakula n.k kwanini? Unadhani kwanini hakuna chombo kimoja kinachosimamia biashara kubwa mpya ili kuulinda mtaji wa huyu mtu anayetaka kuwa mlipa kodi mpya? Anaachwa apigane mpaka tone la mwisho?

Sababu ambayo si rasmi bali maoni binafsi ni wahusika wa hiyo biashara, wanalinda hiyo biashara na mojawapo ya mbinu ni kuhakikisha sheria, sera na taratibu ni ngumu kwa mtu mgeni wa biashara na ili afanikiwe analazimika kupigana na sera, sheria na utaratibu au kutumia njia za panya na kama sio mafia au mzoefu basi atakamatwa na mtaji wote utaishia kwenye kulipa mafaini na kuzima kesi.
 
Back
Top Bottom