Ushauri: Namna nzuri ya kumwambia mpenzi wako kuwa sehemu ya mwili wake inatoa harufu kali

Kama ni kunuka kikwapa mpelekee zawadi ya Deodorant. Muambie darling, hii itasaidia kukata jasho na harufu. Ni nzuri sana, hata mimi naitumia.

Kama ni kunuka mdomo, mnunulie mswaki mzuri pamoja na dawa ya meno ukiambatanisha na mouth wash. Muambie sweetheart, kuna trend kubwa sana ya watu kung'oa meno. Ni kwa sababu tunashindwa kusafisha kwa usahihi na kutumia dawa ambazo hazina ubora. Tunapaswa kuswaki namna hii (huku ukimuelekeza). Tukishakula endapo hatuna nafasi ya kuswaki, basi tusukutue kwa mouth wash yetu hii. Ni bora sana na inafaa kwa watu wa kisasa.

Kama ananuka uchi, mueleze mfike kwa daktari. Muambie unawashwa maeneo hivyo muende kwa pamoja kutafuta suluhisho.

Mambo ya miguu, mchane ukweli. Hatojisikia vibaya.

Puani hakunaga harufu. Mdomo ukinuka basi puani napo hutoa harufu mbaya.

Masikioni, nunua pamba. Kachezeni bafuni, ukirudi shika pamba ukijidai kupeana raha za kutekenyana masikio. Huku unamsafisha.

Kumuambia ni jambo moja. Utekelezaji ni jambo jingine. Kumsaidia kuondokana na tatizo hilo ni muhimu sana kuliko kumuambia.

Wasalaam.
Eeeeeh hiyo shughuli pevu,,,Kwa Nini msiwe tu marafiki muongee in very friendly way?maana mwingine unaweza mpa deodorant bila kujua ana kikwapa akaipuuzia akawa hapaki wala nini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom