Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,557
- 21,515
Habari wakuu,
Husika na kichwa cha habari hapo juu,
Nimewaza na kutafakari kuwa kama Taifa la Tanzania tuna watu wenye upeo na akili kubwa sana ila ni kama wamesahaulika.
Wapo watanzania ambao wanaonekana kuwa wana maono na upeo makubwa na kama wangepewa nafasi basi wangetufikisha kama Taifa mahali pazuri.
Nimekuwa msomaji wa muda mrefu sana hasa hapa JamiiForums na nimegundua hapa kuna watu ambao hawafahamiki ila kama watapewa nafasi ya kuongoza Taifa la Tanzania watalipeleka mahali.
Kama viongozi Serikali ya Tanzania wangekuwa na muda wa kupitia na kusoma hoja za watu huku JamiiForums Kuna watu wenye michango au maoni mazuri na hoja zenye tija kwa jamii na Taifa kwa ujumla.
Ifike mahali hata Rais awe anaangalia Hawa watu wanaotoka katika platform ya JamiiForums na kuwapa vitengo.
Kuna hoja huku zinatolewa na mwisho wa siku zimekuwa zikiibiwa na viongozi wengine na wanazifanyia kazi.
Sasa ni wakati wa Viongozi kutoka katika platform hii ya JamiiForums maana wana hoja za msingi kwa maendeleo la Taifa letu pendwa la Tanzania.
Sasa tumeona huko mitandao ya Instagram kuna viongozi wamechaguliwa kupitia hiyo mitandao.
Ni wakati wa kupenda mitandao yetu kama huku JamiiForums, wao wanafahamika kwa kuandika sio sura zao.
Watu hawa wamekuwa wakiandika vitu vyenye tija kuliko wale ambao wanajulikana kwa sura zao.
Wamekuwa wabunifu, wamekuwa na hoja zenye tija sana kwa uongozi wa Tanzania katika jamii na siasa.
Serikali fungueni macho yenu, hawa waliopo huku JamiiForums wanaupeo mkubwa katika kufikisha Tanzania kwenye Ile nchi yetu ya ahadi.
Niwashukuru sana Serikali ya Tanzania hasa kwa kufanyia kazi na hoja zinazowekwa huku JamiiForums.
Ni ombi langu kuona tunawapa nafasi na hawa watu waliopo JamiiForums.
Tunaweza wataja member hapa...