Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Ni kawaida kwamba katika nchi nyingi matajiri wakubwa utakuta ni wafanya biashara, lakini sio Tanzania. Kwa sasa wanaoongoza kwa kuwa matajiri wakubwa Tanzania ni wanasiasa waliopo madarakani au waliokuwa madarakani huko nyuma. Halafu wanafuatiwa na viongozi wa serikali, pamoja na ndugu zao.
Imefikia kwamba hata ukiwa mfanya biashara, ili utajirike kwa haraka lazima uwe na connection na wanasiasa na viongozi wa serikali, kuanzia connection za ofisi ya raisi, makamu wake au mawaziri. Hata vjana wadogo kabisa wenye hizi connections sasa wanaibukia kuwa na fedha nyingi sana za kufuja na kuishi maisha ya anasa sana.
Inatokea pia kwamba kikundi hiki cha matajiri wa kisiasa uongozi wanalinda sana himaya yao, mara nyingi kwa kutumia vyombo vya dola kama polisi, na sasa hata wanajaribu kutumia jeshi la ulinzi, JW. Hawataki watu wengine wa "kawaida" wawe kama wao. Kwa hiyo wanajaribu kuendelea umiliki wa himaya zao kwa kuwekeza katika watoto wao ili kuja kuwarithisha kuwa "wenye nchi" pamoja na utajiri wao. Hii ni kutia ndani kuendelea kufanya ufisadi mkubwa ili hata vizazi vyao vya baade viendelee kuwa katika neema ya kuwa tofauti na Watanzania wa kawaida.
Wengi wasichojua ni kwamba tatizo kubwa la serikali kukataa uraia pacha sio suala la "usalama wa nchi", bali ni usalama wa hiki kikundi kuona Watanzania walioko nje wana uhuru wa mawazo na upeo wa kuona wanachokifanya. Ndio maana hawataki watu wa diaspora wapewe nafasi ya kuja kuwa tishio kwa himaya yao. Wanawaogopa sana watu wa diaspora na wanaona kuwapa uraia pacha ni kuleta hatari ya kuondolewa katika "ufalme wao". Hawa "wenye nchi" wanajua watu wa diaspora hawana "political illiteracy" ambayo wameijenga katika Watanzania wanaoishi nchini. Wanadiaspora wana macho na wanaona, na wanaogopwa.
Lakini nataka nitoe tahadhari kwa watu hawa, kwamba katika jamii yoyote ile, hali kama hii iliyopo Tanzania huwa haidumu. Kuna wakati itafikia critical point, na kutakuwa na mlipuko mkubwa ambao ni namna fulani ya mapinduzi, ili kuliondoa tabaka hili la "wenye nchi" katika hii himaya yao ambayo kwa sasa wanaifurahia sana na kujaribu kuilinda kwa kila namna. Hili ndilo lililotokea nchi kama Tunisia na Misri, na si muda mrefu litatokea Tanzania, hali ikiendelea hivi.