Ushauri kwa Prof Ndalichako: Achana na vyeti, angalia uwezo kazini

mansakankanmusa

JF-Expert Member
Sep 30, 2010
4,163
787
Achana na Vyeti Angalia Uwezo kwa Wakio Tayari Kazini.
Acha kuwafrustrate Watu Walio waadilifu.

Tunapigania taifa kwa ajili ya elimu ya kujitegemea tunapinga bookish na certification, kwa nini unawavutia watu wakariri....Tunapaswa kuto entertain repetiting school mwenzetu watatumia hata extra hour studies, markup test. Tanzania tukitaka tuachane na repeaters...

Ushauri wa bure achana waliosoma vyuoni na kufaulu vizuri yawezekana mazingira yao katika background zao.

Utaharibu..... my words.

USA universities entry qualifications
US Admissions Criteria | Undergraduate Study in the USA | US-UK Fulbright Commission

UK Country specific application advice
 
Nilimsikia kiongozi mmoja mwanza akitoa mifano mizuri ya watu waliopitia foundation course mpaka phd.Wanakuwa wazuri zaidi kuliko hao formsix! Dada yangu ndalichako usikazanie sana hiyo formsix nyingine huwa ni feki na sio wote ambao hawasomi formsix basi hawana uwezo wa chuo. Fikiria nje ya ukuta Tanzania ya leo imebadilika!
 
Kuna watu walimuona ndalichaku sie miaka kadhaa nyuma hapo. Mkawapinga na kuwakashifu mkadhani ubaya una kwao au kabila? Wacha isomwe namba. Ikibidi hilo zoezi liondoe wote wasio na Div One form 4 na 6.
 
Maprofesa nyie hamuwajui tuulizeni tunaosimamiwa nao kwenye thesis.
Yaani anachokijua professor huwezi kubadilisha hata iweje. Solution hawa wanatakiwa wawe watendaji sio watoa maamuzi. Huyu maza wamrudishe kusimamia thesis huku udsm huko wakae wenye diplona au degree anatosha sana.

Hafanyi kitu hapo maslai kwa walimu hazungumzii ambalo ndo jambo la muhimu yeye na form six form six. Utadhani ndo shule pekee au moarobaini wa matatizo ya elimu kumbe ni "political platitudes" tu hizo
 
Maprofessa wangu wa SUA walipitia Diploma na wakafanya vizuri sana BSc, walipokwenda Universities za Norway, Sweden na Uingereza walifanya vizuri zaidi na wakakubaika. Wengine walivushwa kwenda PHD moja kwa moja baada ya kufanya course work za Masters.

Tusizuie vipaji vilivyofifishwa na mazingira (phenotype) pamoja na umaskini. Bila shaka SUA watakuwa na data. Mwanabailogia/ Mvumbuzi maarufu Duniani wa Genetics/ Father of Evolution Dr. Charles Darwin hakupitia Form VI.

Pitia hii link: Timeline of the life of Charles Robert Darwin: Darwin Online

side_illus-right.png
 
Huyu mama simwelewii kabsaaa,, kipindi anaondolewa necta niliona kaonewa kumbe sababu za kiutendaji zisizo na mwelekeo,, mara GPA 3.5 :mara 3.0 :mara mfumo wa udahili hautawatambua,, hii hatari sana
 
Wako maprofesa na ma-doctors wa kutosha wa education, kwa mfano, ambao wamefika hapo walipo kupitia route tofauti na F.6 - Case Study: UDSM Faculty of Education. Hata kama baadhi wana F.6 lakini kilichowaingiza chuo ni "equivalent qualifications" na sio F.6; tena baadhi walianzia UPE, Grade IIIA, hivyo hivyo na leo ni watu wazito na muhimu nchi hii. Fanya kautafiti kadogo utagundua hilo.

Hii kitu inahitaji mjadala mpana wa kitaifa badala ya waziri kujiamulia peke yake bila hata kutoa sababu za maana ku-justify maamuzi yake.
 
Zoezi hili halitamuacha Dr.bana yule wa UDSM make nasikia naye aliungaunga alikuwa mwal..wa msingi....wacha sasa zianze kusomwa namba za kirumi
 
Mtu mwenye muda saa hivi aangalie iwe kama sampling ya minimum sifa za kujiunga na degree kwa vyuo vitatu Africa mashariki na viwili ulaya na kimoja Marekani halafu alete majibu hapa mtapata jibu sahihi.

Tujipe muda kidogo ili tutowe hukumu ya haki
 
Duniani kote, mtu huangaliwa sifa za elimu yake kupitia vyeti kwanza!! Prof yupo sahihi - uhakiki uendelee.
 
Yani Haya Mambo yanatokea sasahivi yanashangaza sana,dunia yote hajuna mtu anayebanywa lazima apitie njia moja kwenda kupata degree.Sasa huyu mama sijui hilo wazo amelipata wapi,na hata Rais mstaafu mkapa ameshasema haya matamko kuhusu elimu watu wanasema tu bila hata kukaa na wataalamu na kujadiliana,anatokea mtu mmoja tu anasema kwanzia leo itakuwa hivi.Watu wameishi hivyo miaka yote na kwa kuangalia na wenzao duniani wanafanyaje leo hii inaonekana haina maana haifai kwakuwa wewe ndio unaakili sana kuliko watu wote kwenye hii dunia.Kama anajiona anaakili sana amegundua kitu gani cha kutusaidia katika uprofesa wake?Nyelele naye alisema pasipo kuwa na utawala wa sheria na kujua wajibu wako kiongozi ataambiwa jambo huko na mke wake atakuja atatangaza kwanzia leo nataka Hivi.,Hivi hizi sheria na sera zote zilizopo hazina maana kweli?inamaana ni mbovu?mbona nchi nyingine zinakuja Tanzania kujifunza hizo sera na kuzikopi na kuzitumia kwao na zinafanya vizuri?Kwakweli huyu waziri wetu naona aaangaliwe upya kama anaweza kuongoza hii wiazara kweli kwa maana elimu sio nzuri ya kuichezea kiasi hicho.
 
Duniani kote, mtu huangaliwa sifa za elimu yake kupitia vyeti kwanza!! Prof yupo sahihi - uhakiki uendelee.
Uko sahihi lakini vingine apart from F.6 pia ni vyeti. La muhimu ni kuweka minimum entry/pass mark badala yu kuvi-rule out completely.
 
Polen sana ndugu zangu,muacheni mama arekebishe elimu maana ilipofikia kila mtu alikua ana laumu.sasa anainyoosha tunalalama.HiviWatz sisi mafundi wa kukosoa tu?.Kila siku watu wanalalamika watoto wanaingia chuo mambumbumbu wasiojua hata Tzilipata uhuru mwaka gani.Hawajui hata aina za constitution,hawana wasi wanajua wakifeli wataenda cheti.Matokeo yake ni vyuo kuzalisha vilaza wengi wasioajirika kabisa
 
Back
Top Bottom