Ushauri kwa mkuu wa shule ya sekondari Nyiendo, wilayani Bunda

Mjukuu wa kigogo

JF-Expert Member
Sep 19, 2023
201
438
Salaam zikufikie mkuu wa shule ya Sekondari Nyiendo halmashauri ya mji wa Bunda.

1. Punguza makundi. Umeigawa shule katika makundi matatu.Kundi la machawa(wafuasi maslahi).Hili ndilo kundi lenye nguvu zaidi Kwa sasa shuleni.Maazimio yoyote yasipokubaliwa na hawa hayapiti.Hawa wana kura ya veto(Turufu)Kama ni Taifa Duniani hawa ni USA. Hawa pia kazi yao kuu ni kuharibia wengine kwako Kwa kukuletea maneno chonganishi ili wenzao wasipate nafasi za fursa mbalimbali za usimamizi,na ndivyo ilivyo wateswa wako wote umeamua makusudi kuwanyima fursa za usimamizi wa mitihani. Hii ni dhambi kubwa sana na itakutesa sana siku za mbeleni. Kwa asilimia kubwa hili kundi limekuteka na limefanikiwa kutimiza adhma yao. Kundi la pili ni wale usiowakubali(yatima)hawa Kwa sasa wameanza kujitenga kabisa mpaka wanafunzi wanafahamu hili suala mpaka majumbani wanaongea Kwa wazazi. Hili ni kundi lililokata tamaa likisubiri tu umalize muda wako uondoke. Kundi la tatu ni lile lijulikanalo kama chaja ya Kobe(Wanafiki)Hawa hawaonyeshi moja Kwa moja wanaunga mkono kundi lipi ila mara nyingi wanaishi kulingana na upepo unavuma wapi.Ni mwalimu mmoja tu asiye kwenye hayo makundi,ni maji ya kunde,mwembamba toka Kanda ya kaskazini ambaye hayupo kwenye hayo makundi.

2. Kuwa makini na mmoja kati ya wasaidizi wako (washauri)wa juu anayetoka kati ya ofisi mojawapo kati ya hizi(Ofisi ya makamu,Taaluma na malezi). Huyu anakufanyia unafiki sana anapokuwa na jamii anakupiga vita sana na hupendelea kutumia maneno "Huyu mama kazeeka awaachie wengine mambo mengi anatufelisha yeye"ila wewe ukiwa nae mnasocialize vizuri huku akikupaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Imefikia hatua watu wameanza kuamini yeye ndie kila kitu katika shule kiasi kwamba bila yeye shule haiwezi kusonga mbele.

3. Penda wale unaoaminishwa ni maadui zako.Walimu wanaohoji hadharani ndani ya vikao siyo maadui kama watu wanaokuzunguka wanavyokuaminisha.

4. Walimu wako wanalalamika unakuwa parade Kila siku kuliko hata mwalimu wa zamu.Hii pia linakupunguzia uzito.Tokea parade wakati wa matukio nyeti tunili kulinda hadhi yako isizoeleke ovyo.

5. Usiingize urafiki kwenye maamuzi.Kuna mwanafunzi(jina kapuni) aliiba vifaa vya Maabara (reagents)ila uliweka ngumu asifukuzwe bali apewe uhamisho huku watoto wengine wa wasio na watetezi wakifukuzwa. Katika kuchunguza ilibainika ni mtoto wa swaiba wako(family friend). Hii imekuongezea wakosoaji wengi!Siyo fair madam!

6. Narudia punguza machawa ambao wameanza kukuharibia madam.Kuna mwalimu mmoja wa kike jumatatu wiki iliyopita wakati wa chai alimweleza mwenzake kama ana hoja ampe yeye(chawa)Kisha chawa ataiwasilisha kwako personally maana anakumudu mno anapongea na wewe huwezi kukataa!
Fursa zako sasa hivi kwa walimu zinatabirika kabisa.Wape nafasi na wale ambao umeaminishwa ni maadui ili wakusaidie hasa wale 3 dadaz ambao umewatupa!

7. Next time angalia sana umakini katika kuteua bodi ya shule.Jiulize wanakusaidia nini zaidi ya kukuachia mzigo wa mambo mengi huku wao wakinyemelea tu posho!Mbaya zaidi na wao wakiwa nje huku wanasema hushauriki

8. Wajali walimu wa kujitolea(Part time teachers)hawa japo hujawagundua wanapiga kazi sana kuliko walimu wako wa kuajiriwa.Hamasa ya wanafunzi kutoa pesa Kwa ajili ya hawa walimu haipo. Miezi mitatu iliyopita mlikusanya 64000=mkawaita hawa walimu ambao idadi yao ni walimu nane mkawagawanyisha 8000\=kwa kila mmoja hii siyo haki. Wewe au walimu wako ni nani kati yenu anaweza kuishi Kwa 8000 Kwa mwezi? Pia mmewatenga sana huku mkiwazuia kutoa adhabu Kwa watoto wakorofi matokeo yake wanaishi na wanafunzi kama 'chibaba na chimamy' wake. Kauli zako maarufu "wewe chapa tu likikufika utalimaliza mwenyewe"

9. Kama utaweza vunja ofisi ya taaluma weka wapya.Hapa sihitaji kukufafanulia zaidi ila ivunje kwa maslahi ya shule au wabadilishie idara.Pkease vunja hii ofisi,usiogope kuanza upya

10. Washauri walimu wako wawe pia wanahudhuria vikao vya ofisini(staff meetings)badala ya kuvipuuza na kuishia kulalamika tu.

11. Kuna mwalimu mmoja wa kujitolea(part time teacher)ambaye ni kiongozi wa walimu wa muda,Huyu kwa kuwa hana cheti cha ualimu amekuwa akiwahujumu wenzake ofisini waonekane wabaya kwa kutoa Siri za vikao vyao ili aendelee kukumbatiwa kuwepo shuleni.Lengo la kuwasaliti wenzake ni uongozi umpende na kuwa Kinga kwake maana hana cheti.

Je, unakumbuka mgogoro mkubwa uliotikisa shule yako ndani ya miaka mitatu mfululizo iliyopita kati ya mwalimu mmoja mahiri wa kike anayefundisha somo la hesabu na wataaluma waandamizi, mgogoro ambao mpaka ulihusisha Imani za kishirikina? Ulibaini nani alikuwa chanzo cha tatizo?Anyway nikukumbushe punguza kuangalia pale shule inapoangukia bali angalia pale ilipojikwaa!
 
Uliyoyaandika yote hayo una uhakika atayasoma humu humu JF?
Ninamashaka na wee ni mmojawapo wa Walimu wasioudhuria vikao Vya staff alafu unaifanya JF kama ndiyo staff meeting yako.
Au una uhakika ana akaunti humu JF?
 
Maswala ya kwenda kumshari mkuu wako huko ofisini kwenu unakuja kutuletea jamii forum huku kama sio kutujazia savers ninini?
 
Mleta mada mtumie kwa sanduku la barua huyo Madam asome ujumbe wako humu tunasoma tusiohusika na mambo yenu ya ualimu au mnataka Mpwayungu Village aje kuwapa za uso?
 
Back
Top Bottom