Hongera sana Mkuu wa shule ya Sekondari Nyiendo wilayani Bunda ila hebu tupia jicho ila hili limetia doa

Mjukuu wa kigogo

JF-Expert Member
Sep 19, 2023
201
439
Awali wakati tunaanza kulalamikia mambo kadhaa kadhaa hapo shuleni, baadhi waliamini ni chuki binafsi, vita ya kugombania madaraka, watu kukosa fursa, n.k. Lengo letu halikuwa baya. Kwa wafuatiliaji wa mitandao, tumefanya haya kukosoa na kupongeza taasisi mbalimbali nchini, mfano St. Mathew, Elohim, Bugando, Teofilo Kisanji, n.k., kwa hiyo hatujaanza leo!

Tukirudi kwenye hoja ya msingi, tunapenda kuutumia uzi huu kukupongeza kwa dhati kabisa! Tangu tumeripoti changamoto kwenye kituo chako, umebadilika sana! Tunamaanisha mabadiliko chanya! Hata yule bwanyenye aliyekuwa anaonekana shuleni kama kakakuona kaanza kuhudhuria! Makundi shuleni yameanza kufa! Ari ya kufanya kazi iliyopotea imeanza kurudi!

Sasa kuna hili hapa linafuka moshi! Kuna taarifa za wanafunzi wa kike kunyanyaswa kimapenzi na baadhi ya walimu wa kiume! Na wamewataja kwenye vikao vyao! Suala hili tunaomba lifanyiwe kazi haraka lisiachwe maana hapa kuna mambo makuu mawili, inaweza kuwa mbinu ya wanafunzi husika kuwachafua na kuwavunja moyo walimu husika wasiweze kutimiza majukumu yao ipasavyo (hili pia ni kawaida kutokea kwenye taasisi mbalimbali duniani). Ikibainika wanafunzi wananyanyaswa, wahusika wachukuliwe hatua kali, na endapo ni mbinu za wanafunzi, pia wanatakiwa kupewa adhabu kali sana itakayoambatana na kumtambua aliye nyuma yao anayeendesha hii hujuma!

Sasa linaloendana na hilo, ambalo sasa ndio limeleta huu uzi, kuna mwalimu wako mmoja wa kike ambaye inasemekana ana mahusiano na mmoja wa walimu wako wa kiume. Huyu sasa kalikoroga kweli kweli. Kuna mazingira yanaonyesha huyo mwalimu wa kiume anatembea na mwalimu wa kike pamoja na mwanafunzi (anawachanganya). Sasa hili sijui tuliiteje, sijui kughafirika au kupitiwa!

Hivi inaingia akilini mwalimu wa kike kumuita mwanafunzi husika chumba na kumchamba kisa kupambania penzi! Mbaya zaidi wakiwa watatu (mwalimu wa kike, mwalimu wa kiume, na mwanafunzi husika). Zaidi ya masaa matatu walimu mnareconcile conflict ya kimapenzi na mwanafunzi? Hii ni hatari na inashusha hadhi ya mwalimu! Bahati nzuri mwanafunzi mnamjua, na hao walimu wanajulikana! Sasa hivi hii issue ndio story ya wanafunzi! Mkuu waite walimu husika uongee nao!

Jingine ni hili la mwalimu wako mmoja kumnyima maji mwalimu mwenzake mgonjwa ambaye alikuwa anahitaji maji ya kumezea dawa! Kutoa chupa moja ya nusu lita angepungukiwa nini kwenye katoni tatu zilizokuwepo? Wakumbushe walimu wako waache roho mbaya! Haya yafanyie kazi!

Lengo letu ni kujenga na si kubomoa!
 
Dah mwalimu mwalimu mwalimu kwa busara hii ungepungukiwa Nini ungeongea na mkuu wako kumpa ushirikiano huu?huoni aibu kuichafua ofisi yako kwa tuhuma ambazo kama mwalimu mwenye maadili mngeweza kuongea tu hapo ofisini kweli maji ya lita moja na nusu nayo ishu huyo mwalimu alieomba maji Hana mshahara? Binafsi ni mwalimu ila kwenye ualimu Kuna majamaa Wana mambo ya kiwaki sana unashindwaje kwenda shule na maji yako ya kunywa?yani huwezi kukuta story za maendeleo ni majungu majungu na umbea kwa style hii hatutaheshimiwa kamwe!!! Mwisho vishkwambi virudishwe tu vimeongeza wimbi la walimu wasio kuwa na subira kuleta mambo yasiyokuwa ya msingi mbele ya jamii mfano mtoa hii post kila akipost ni majungu tu ila anakuja kwa gia kama mwana harakati stupid
 
Back
Top Bottom