Ushauri kwa CCM: CCM ijichimbie mizizi mirefu na imara

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Apr 19, 2021
1,502
4,408
Ndani ya CCM kumeibuka tabia ya baadhi ya wanachama kujiona wana nguvu sawa au kuliko Chama. Tuliona hivyo mwaka 2015 wakati Lowassa alipokatwa CCM kwamba CCM ikatike naye. Haiwezekani chungu akawa mkubwa kuliko mfinyanzi.

Tabia hii si tu inahatarisha uwepo wa CCM lakini pia inachangia kutengeneza mazingira ya kuwepo kwa mfumo mtu. Na hii itasababisha watu watachaguliwa ili kuilinda Chama. Je, watu hao wakitwaliwa?

Ni sharti Chama kiwe na mizizi mikubwa na imara kuliko mwanachama au kikundi chochote ndani ya Chama na pia kuepusha Chama kutegemea watu na si Chama kutegemewa na watu.

Ili kufikia hali hii ya Chama kutegemewa na wanachama siku zote nashauri yafuatayo:

i) Chama kutosita kukemea au hata kuondoa mwanachama au wanachama wanaoonesha dalili za kujikweza(kupandisha mabega)

ii)Chama kiweke mazingira rahisi na rafiki kwa kila mwanachama kuchaguliwa. Nashukuru hili mzee Kinana ameligusia kwa undani juu ya haki ya kuchaguliwa na kuchagua. Hivyo naamini utekelezaji utafanyika haraka.

iii) Chama kiwe na uwezo kwa maana ya rasilimali watu na fedha za kutosha kutekeleza majukumu yao ipasavyo. Tumeona mara nyingi matajiri wakihitajika kuchangia pesa za kuendeshea Chama hivyo inasababisha wanaofanya hivyo kujiona wamekinunua Chama.

iv) wakereketwa na wafia Chama wapewe nafasi za mbele ili kupata watu wenye weledi na ujuzi wa masuala ya Chama. Yaliyotokea miaka ya karibuni yaweza kuwa hayaridhishi kwa wafia Chama hivyo ni heri kuepukwa kuepusha misuguano na migongano

Kwa hayo machache na mengine mengi yakizingatiwa kwa uono wangu tutakuwa na Chama imara na chenye nguvu kuliko mwanachama au wanachama wake.

Kudumu Chama Cha Mapinduzi
 
Uchamadola unaoiweka ccm madarakani ndio huohuo unaoidhofisha hadi kufikia kuiba chaguzi. Ccm itafute mbinu za kujijenga nje ya uchama dola ili iingie mioyoni mwa watu.
 
Ndani ya CCM kumeibuka tabia ya baadhi ya wanachama kujiona wana nguvu sawa au kuliko Chama. Tuliona hivyo mwaka 2015 wakati Lowassa alipokatwa CCM kwamba CCM ikatike naye. Haiwezekani chungu akawa mkubwa kuliko mfinyanzi.

Tabia hii si tu inahatarisha uwepo wa CCM lakini pia inachangia kutengeneza mazingira ya kuwepo kwa mfumo mtu. Na hii itasababisha watu watachaguliwa ili kuilinda Chama. Je, watu hao wakitwaliwa?

Ni sharti Chama kiwe na mizizi mikubwa na imara kuliko mwanachama au kikundi chochote ndani ya Chama na pia kuepusha Chama kutegemea watu na si Chama kutegemewa na watu.

Ili kufikia hali hii ya Chama kutegemewa na wanachama siku zote nashauri yafuatayo:

i) Chama kutosita kukemea au hata kuondoa mwanachama au wanachama wanaoonesha dalili za kujikweza(kupandisha mabega)

ii)Chama kiweke mazingira rahisi na rafiki kwa kila mwanachama kuchaguliwa. Nashukuru hili mzee Kinana ameligusia kwa undani juu ya haki ya kuchaguliwa na kuchagua. Hivyo naamini utekelezaji utafanyika haraka.

iii) Chama kiwe na uwezo kwa maana ya rasilimali watu na fedha za kutosha kutekeleza majukumu yao ipasavyo. Tumeona mara nyingi matajiri wakihitajika kuchangia pesa za kuendeshea Chama hivyo inasababisha wanaofanya hivyo kujiona wamekinunua Chama.

iv) wakereketwa na wafia Chama wapewe nafasi za mbele ili kupata watu wenye weledi na ujuzi wa masuala ya Chama. Yaliyotokea miaka ya karibuni yaweza kuwa hayaridhishi kwa wafia Chama hivyo ni heri kuepukwa kuepusha misuguano na migongano

Kwa hayo machache na mengine mengi yakizingatiwa kwa uono wangu tutakuwa na Chama imara na chenye nguvu kuliko mwanachama au wanachama wake.

Kudumu Chama Cha Mapinduzi
CCM inaendelea kuwepo kwa sababu ya Umasiki make ndio mtaji wao, pili ni ujinga wa Watanzania
 
Pole kwa mtazamo hasi na mtazamo huu utakutesa sana

Tukianza na suala la umasikini. Hili suala linamuhusu MTU zaidi ya kusababishwa na serikali. Sera za CCM katika kukabiliana na umasikini ni muafaka. Hapa ni lazima tutambue umasikini unaondolewa kwa mchakato na mchakato huo hauwahusu wavivu na wazembe.

Tukija kwenye suala la ujinga. Naamini ujinga unaozungumziwa hapa ni ukosefu wa elimu. Lakini tuseme ukweli juhudi na jitihada za CCM kupunguza tatizo hili ni la kiwango gani? CCM kimefanya elimu bila malipo mpaka kidato cha sita na hii yote ni kuboresha elimu na kuondoa ujinga.

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, CCM kimefanya kazi kubwa na nzuri kupunguza na kuondoa umasikini na ujinga
 
Back
Top Bottom