Ushauri: Ameniacha anataka tuwe dada na kaka

The next JPM

Member
Feb 22, 2023
22
44
Habar wakuu,

Mimi ni Kijana wa 23 nipo chuo kikuu kimoja hapa Tanzania.

Nilikuwa na mahusiano na binti mmoja kiukweli nilimpenda sana, ilikuwa ngumu kwa yeye kunikubali lakini baadaye alikubali, tumekaa kwenye mahusiano kwa miezi sita tu lakini kwangu ilikuwa ni uchungu kwani nilitumia nguvu sana kulinda mahusiano yetu.

Yeye alikuwa kama hajali kuhusu mimi, ilipofika mwezi wa kumi na moja mwaka jana akasema tuachane na ananichukulia kama kaka yake.

Kiukweli nilliumia sana, nikambembeleza sana lakini hakutaka, na mimi sikuwa na kosa na sijui kwanini aliamua hivyo.

Wakuu shida yangu ni hii, toka aniache nahisi maumivu makali moyoni mwangu kila nikimkumbuka.

Kila siku huwa namuomba turudi kama zamani lakini hataki kabisa. Mimi sijawahi kupenda before, ukweli sina nafasi kwake lakini moyo wangu unasema bado nina nafasi kwake.

Nahisi sitopendatena, pia najihisi kuwa sitapata kama yeye, japokuwa sikuwahi kufanya nae mapenzi maana mimi nimeokoka.

Naombeni ushauri, najihisi nipo isolated, najihisi maumivu mabaya sana.
 
Acha kuwa dhaifu kama wale wanaoogopa ndoa sababu ya wanawake vimeo kama huyo anayekuzuzua...

Mwanaume amaumbwa kuwa imara, jasiri, anayepanga kesho yake iweje na ndio maana halisi ya kuwa kichwa...

Jifunze ukubwa wa uanaume wako kupitia hata viumbe hai vingine vilivyoumbwa na Maulana...

Ona namna jogoo linavyomtawala mtetea, au ona namna simba dume linavyokuwa na milki ya eneo fulani...

Mwanamke kimeo akizingua piga chini bonyeza kabisa Shift + Delete apotee mazima, mwache akakutane na wanaume dhaifu wale wasio taka ndoa au mahusiano yenye afya, maana aina hiyo ya wanawake vimeo ndio chakula ya wanaume dhaifu...
 
Ila jambo ni kawaida na dunia haina huruma sio wewe tu ...Maisha ndo yalivyo ni mateso kwenda mbele we komaa tu mpotezee litapita ,najua ni mwanzo tu ila utasahau amini nakwambia.

Wapo vijana mademu zao wameolewa ila miaka kadhaa walipiga moyo konde na woa wakaoa na kupata familia na kusahau yote yaliyopita..
 
"Kila siku huwa na muomba turudi kama zamani lakn hataki kabisa mm sijawahi"
"kwangu Ilikuwa ni uchungu kwan nilitumia Nguvu sana kulinda mahusiano yetu."

Hayo juu ni maelezo yako na bado unaomba ushauri Ili ukapambanie kupendwa badala ya kupambania hela
 
Habar wakuu,

Mimi ni Kijana wa 23 nipo chuo kikuu kimoja hapa Tanzania.

Nilikuwa na mahusiano na binti mmoja kiukweli nilimpenda sana, nili ulikuwa ngumu kwa yeye kunikubali lakini baadaye alikubali, lakini tumekaa kwenye mahusiano kwa miezi sita tu lkan kwangu Ilikuwa ni uchungu kwan nilitumia Nguvu sana kulinda mahusiano yetu.

Yeye alikuwa kama hajali kuhusu mimi, lakini ilipofika mwezi wa kumi na moja mwaka Jana akasema tuachane na ananichukulia kama kaka yake.

Kiukwel nilliumia sana nikambembeleza Sana lakini hakutaka, na mimi sikuwa na kosa na sijui kwanini aliamua hivyo.

Wakuu shida yangu ni hii Toka aniache na nahisi maumivu Makali moyoni mwangu kila nikimkumbuka.

Kila siku huwa na muomba turudi kama zamani lakn hataki kabisa mm sijawahi kupenda before, ukweli sina nafasi kwake lakn moyo wangu una SEMA bado ni nanafas kwake.

Nahisi sitopenda tena pia najihisi kuwa sitapata kama yeye, japo kuwa sikuwahi kufanya nae mapenzi maana mimi nimeokoka.

Naombeni ushauri najihisi nipo isolated, najihisi maumivu mabaya sana.
Dogo sikiliza;
Wewe bado mdogo sana kukata tamaa eti hutopata mwingine kama yeye.
Wewe ni wa kiume huna la kupoteza.

Kwa kawaida wanaume mwanzoni tunaumizwa sana na akina dada kwani tunakuwa hatuko stable kiuchumi na wenzetu wanaangalia sana uchumi.

Huyo anagongwa na lizee lenye pesa chafu achana naye kwani huna la kupoteza kwani hutashika mimba wala nyonyo hazitalala kama lapa bali yeye ana ukomo wa muda wa kusumbua.

Somo
Tafuta pesa
Vitoto vizuri vinakua utajichagulia kama nguo kwa Vunja bei.
Wazo katili hili
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom