Ushahidi kwa NIDA kuhusu suala la vitambulisho vya taifa

Cesar Saint

JF-Expert Member
Nov 18, 2016
424
725
Wasalaam,

Ikiwa kesho ndio tamati ya nyongeza ya muda wa Wananchi kujisajisili simcard zao kwa mfumo mpya unaohitaji namba ya vitambulisho vya taifa (NIDA) inategemewa kuwepo kwa kundi kubwa la watu watakao athiriwa na zoezi hili.

Zoezi hili linausisha taasisi mbili za Serikali NIDA na TCRA ambapo kwa sehemu kubwa ufanisi wa zoezi hili utategemea kasi na utendaji kazi wa NIDA.

Zoezi hili athari yake itawakumba wengi kuliko lile la kuhama kutoka analog kwenda digital lililohusisha TCRA kutokana na Tanzania kuwa na watumiaji wengi wa simu kama njia ya kuu ya mawasiliano.

Hii inatokana na watanzania wengi kukulia katika mfumo wa kiholela usiowahitaji kuwa na vitambulisho (utambulisho) matokeo yake wengi wamekuwa wakitumia barua za wenyeviti wa mitaa kama vitambulisho vyao pale wanapohitajika kufanya hivyo.

Watanzania wengi hawana vyeti vya kuzaliwa, vitambulisho vya kazi, vyeti vya elimu nk hii ni baadhi ya changamoto kubwa zilizokumba zoezi hili achilia mbali matatizo ya vitendea kazi.

SULUHISHO.
Kwa maoni yangu nafikiri ingefaa sana kama NIDA wangekuwa na hatua mbili katika zoezi hili.

Hatua ya kwanza ungehusisha zoezi hili kufanywa na wananchi husika kupitia simu zao za mikononi kwa kujaza taarifa zao na mambo mengine ikiwamo picha na kisha mtu akishafanya hivi anapatiwa namba ya maombi ambayo hii itamwenzesha kusajili simcard yake kipindi anasubiri majibu.

Attachments zinaweza kufanyika pia kwenye mtandao kwa walioko mijini na kwa wale wa vijijini zoezi hili linaweza kufanywa kwenye ofisi za kata husika.

Hatua ya pili iwe ni uhakiki (physical verifications) wa mwombaji pamoja na kumpatia kitambulisho hii itaondoa usumbufu kwa wale ambao watakamilisha mahitaji ya maombi yao bila kutia mashaka lakini pia kuwapa mamlaka nafasi ya kuzuia mamluki pale inapowalazimu kufanya hivyo.

Kwa hatua hizi ni imani yangu kutafanikisha zoezi hili kwa ufanisi mkubwa.

Asante
 
Back
Top Bottom