La Quica

JF-Expert Member
Dec 19, 2017
951
2,170
Asee wakuu kumbe kuna watu wana jax sana hii nchi. Nimeona huko Twitter kuwa huu ni usajili wa mabus 20 mapya ya Abood.

FBgbKxrWYAYv33u.jpeg

Tutafute hela wakuu.
 
Humjui abood wewe,utakuwa umezaliwa juzi,kila nusu saa kuna gari inatoka msamvu kuja dar na dar kwenda moro,bado route za mikoa bado yanayokodishwa,reserve na yaliyo service
Mimi sijui idadi yake lakini sitasahau tukio la almost 20 years ago!!!

Nimefika zangu Ubungo nimekuta basi la kampuni fulani hivi (nimesahau jina lake lakini sio Islam) likiwa na watu zaidi ya robo tatu kama sio zaidi.

Wakati huo huo, basi moja ya Aboud ndo lilikuwa linajitayarisha kupakia abiria, na kwahiyo halikuwa na abiria hata mmoja!!

Sasa kwavile sikuwa na uzoefu na mabasi yaendayo Morogoro, nikapanda lile nililoona limejaa zaidi ya 3/4 huku nikiamini ndo nitawahi kuondoka!!

Kitu ambacho sitasahau, ziliondoka Aboud kama sio 4 basi 5 wakati basi letu lililokuwa limejanza zaidi ya 3/4 kabla yao tukiwa pale pale!!

Na ninachotaka kusema kwamba, labda siku hizi kwavile magari ni mengi lakini kwa wakati, hiyo nusu saa ingekuwa zinaondoka Aboud angalau 3 kwa route moja!!!
 
Asee wakuu kumbe kuna watu wana jax sana hii nchi. Nimeona huko Twitter kuwa huu ni usajili wa mabus 20 mapya ya Abood.

View attachment 1972491
Tutafute hela wakuu.
Mimi ninadhani hicho ni kiwango cha kawaida tu kwa kampuni kama Abood. Hata alipoingiza hizi zilizopo sasa ni hivyohivyo tu. Ninakumbuka ilikuwa sherehe pale Msamvu, misele ya kufa mtu roundabout wakipokewa na bodaboda.

Ninafikiri kwetu wateja, muhimu sasa ni kuletewa basi zilizo comfortable na rafiki kimatumizi. Yutong tunazoletewa ni za kikuda sana. Pot za kuchajia zinadumu miezi,hazifiki mwaka. AC halikadhalika—ikishabuma mtakoma humo kwenye basi. Siti pia ni ndogoo,ukiwa mrefu ama kibonge imekula kwako.

Ninajua haya ndo huchangia kushusha bei ya basi huko sokoni uchina. Lakini,kwakuwa kampuni ina uwezo, ingia dau kubwa, lete chache za ukweli wenye uwezo wapande kwa bei elekezi. Wateja wapo. Tunaona BM ana zile zenye daraja la kwanza na la pili. Kila siku daraja la kwanza zinajaa fasta.

Halafu Abood kama mnanisoma acheni ubahili. Katikati ya Dar na Moro jengeni kahoteli uchwara ka kupata bites na kujisaidia. Mnahama vihoteli, mnapeleka abiria vihoteli vinanuka choo utasema vyoo vya stend. Bites za kiwango cha chiiini.

Safari ni starehe jamani.
 
Back
Top Bottom