US honours Kilango

Nasubili Bunge lianze mapema hapo Mtakoooooooooooooma kumjua mama Kilango sasa atafanya kwa bidii zaidi mtajuta kumfahamu.
 
Hongera sana Anne umekuwa mdano wa wanawake shujaa. Kaza buti

Masa hii tuzo ilikuwapo ingawa si ya zamani sana. Mwanamke wa kwanza kutunukiwa tuzo hii alikuwa Bi Hellen Kijo Bisimba wa Kituo cha Haki za Binadamu mwaka jana 2008 kama sikosei au kumbukumbu zangu hazinipotei.
 
Hongera mama Anne Kilango-Malecela!
Mama anajiamini vizuri kwenye kuchangia hoja nzito sanasana bungeni. Endelea na uchapakazi wako mzuri na ubarikiwe sana!
 
Hongera sana Mama Anne Kilango-Malecela kwa tuzo ya heshima inayotambua jitihada zako kwa watu wa Taifa hili.

Nakuombea maisha marefu, uwe na nguvu na upendo kwa waTanzania wenzako wanaoendelea kuhujumiwa na watu wenye roho mbaya, nia mbaya na wasio na uchungu kuona watoto, na wazee wa Taifa hili wakiteseka kutokana na ulafi wa mali wasizostahili kuzimiliki.

Mungu akupe ujasiri zaidi. Kama ambavyo naamini siku zote, wewe na wenzako wenye nia kama yako ni lulu ya Taifa hili. Umeonyesha ujasiri bila woga, na woga ukae mbali nawe.
 
- Ni sasa hivi tu nimemaliza kuongea na Mama Anne, na amenisomea barua ya zawadi hii, ni kwamba hii zawadi inatoka moja kwa moja kwa Mama Clinton, na leo rais wa jamhuri amemtumia barua nzito sana ya kumhongera na tuzo hii.

Mungu amuongezee maisha Mheshimiwa Mbunge, na kumpa nguvu zaidi na busara mbele ya safari yake ya uongozi imara.

Ahsante.

William.
 
- Ni sasa hivi tu nimemaliza kuongea na Mama Anne, na amenisomea barua ya zawadi hii, ni kwamba hii zawadi inatoka moja kwa moja kwa Mama Clinton, na leo rais wa jamhuri amemtumia barua nzito sana ya kumhongera na tuzo hii.

Kwa kazi aliyoifanya mume wake, Mzee Malecela, ya kumpigia debe Kikwete, siwezi kushangaa kwa nini Kikwete asiendelee KUIHONGA hiyo familia. Utaona jinsi matangazo yake yatakavyokuwa makubwa.

Mola Wetu tuepushe na haya maigizo yanayotumika kuihadaa nchi na ulimwengu.
 
Kwa kazi aliyoifanya mume wake, Mzee Malecela, ya kumpigia debe Kikwete, siwezi kushangaa kwa nini Kikwete asiendelee KUIHONGA hiyo familia. Utaona jinsi matangazo yake yatakavyokuwa makubwa.

Mola Wetu tuepushe na haya maigizo yanayotumika kuihadaa nchi na ulimwengu.

- Mkuu mbona umekua ukitoa michango makini sana, lakini hapa hueleweki hebu fafanua kidogo jinsi Rais wa jamhuri yetu anavyohusika na kuihonga familia ya Mzee, halafu akamshawishi na Mama Clinton naye akaihonga zaidi na hii tuzo.

- Hivi wa-Tanzania tuna nini hasa? Mzee ametoa chaguo lake la anayemtaka kugombea urais mwakani na wewe na wananchi wote tutoe chaguo zetu, eti mimi ninaposema ninamtaka DR. Slaa awe rais wangu next familia yangu inakuwa imehongwa na Dr. Slaaa?

Mkuu mbona huwa nakuona unatoa ides nzito sana ambazo ni constructive hasa kwenye mjadala wa Zitto na Dowans, au kuna mtu ameiba code yako bro?

I mean this is strange, eti rais wa jamhuri anaihonga hii familia ndio maana US wakampa Mbunge tuzo, na yule mama aliyepewa mwaka jana alihongwa na nani mkuu? Kweli Tanzania tuna safari ndefu sana na demokrasia walioko ndani hawaijui na sisi tulioko nje hatuna idea kabisa!

Inasikitisha sana.

FMES!
 
wandugu,

..hongera mama anne kilango-malecela.

..naamini tuzo hii itampa moyo mama malecela kuendelea kupambana na ufisadi.

NB:

..kuna yeyote anafahama previous recepients wa tuzo hii?

..je, tuzo hiyo inakuja na cash prize?

..je, ubalozi wa Tanzania Washington DC unaweza kumtunza Mmarekani anayepambana dhidi ya ufisadi, kama upo, ktk serikali ya Mzee Obama?
 
Beyond a successful woman there's a man

Tusisahau kumpongeza na mzee wetu John S C Malecela pia...
 
Mkuu FMES na wakulu wengine,nimefarijika sana kwa huyu mama kupewa tuzo hii ya heshima..

Upendo wake kwa nchi hii ni heshima kubwa sana kwetu,william mwambie mama ana aendeleze libeneke na tupo naye kwenye ukurasa moja

William karibu jamvini,
 
hahahaha!Confilikiti ofu interesiti

- Ogopa waliowekeza kwenye kampuni ya umeme inayogombea uwanja na Rostam kule Singida, ndio maana tunaowajua tunamuonea huruma Shujaa Mwakyembe sijui alikutana nao wapi maana wengine ni matapeli wa kutupwa! Bwa! ha! ha! ha! Kuhongwaaa na utapeli zim zim zim! Bwa! ha! ah!

Wazee wa sauti ya umeme FMEs!
 
Mkuu FMES na wakulu wengine,nimefarijika sana kwa huyu mama kupewa tuzo hii ya heshima..

Upendo wake kwa nchi hii ni heshima kubwa sana kwetu,william mwambie mama ana aendeleze libeneke na tupo naye kwenye ukurasa moja

William karibu jamvini,

- Ahsante ndugu yangu nimeshakaribia yapata wiki tatu sasa, ameniahidi kunitumia copy ya barua ya tuzo na I am looking forward kuiweka hapa wapiganaji wote waione, kwa hiyo mkuu salam zako zimefika na tuko pamoja sana.

Ashante.

William.
 
Rais Kikwete ampongeza Anna Kilango kwa ujasiri dhidi ya ufisadi

Na Leon Bahati,

MWANANCHI, March 29, 2009

RAIS Jakaya Kikwete amempongeza Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango kwa kutunukiwa tuzo ya kimataifa ya Mwanamke Jasiri kwa mwaka 2009 na kwamba, ni ishara ya dunia kuutambua mchango wake katika kupambana na ufisadi nchini.


Taarifa iliyotolewa jana na Ikulu kwa vyombo vya habari, ilielezea kuwa Rais Kikwete alipokea kwa furaha kubwa habari za Kilango kutunukiwa tuzo hiyo.


Wiki hii, Kilango ambaye amekuwa mkali kwa kauli mbalimbali dhidi ya ufisadi, alikabidhiwa tuzo hiyo na Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Larry André.


Tuzo hiyo ya mwaka ilianzishwa kwa lengo la kutambua na kuthamini mchango wa mwanamke aliyeonyesha ujasiri wa kiwango cha juu na uongozi mzuri.??Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ulimteua Kilango kuwa mmojawapo kati ya washiriki waliowania Tuzo ya Kimataifa ya Mwanamke Jasiri ya Mwaka 2009, kutokana na ujasiri aliouonyesha katika kukosoa na kuupa changamoto uongozi wa chama chake ili uweze kushughulikia kikamilifu suala la rushwa. ??Kwa kufanya hivyo alivunja utamaduni wa kisiasa uliokuwa umejengeka bila kujali vitisho kwa usalama wake binafsi. Bila kuchoka wala kutetereka, alishikilia azma yake ya kupiga vita rushwa na kuuliza maswali mazito yaliyoibua mijadala iliyochangia sana katika jitihada za kuongeza uwazi na utawala bora ndani ya chama tawala.


Hatua ya Rais Kikwete kumpongeza Kilango ni pigo kubwa kwa kundi la wana CCM wanaodaiwa kujihusisha na vitendo vya ufisadi na imekuja wakati chama hicho kimegawanyika katika makundi mawili, lile linalotuhumiwa kwa ufisadi na lile la wanaoongoza mapambano dhidi yao, akiwamo mbunge huyo wa Same Mashariki.


Rais Kikwete aliielezea tuzo hiyo kama ni tunda linalotokana na Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005 kuhusu vita dhidi ya rushwa.


"…CCM na serikali yake, vimetoa fursa pana zaidi kwa wananchi, wanahabari na viongozi, wakiwemo waheshimiwa wabunge, kushiriki kikamilifu zaidi," alisema Rais Kikwete kupitia taarifa hiyo na kuongeza:


"Kutunukiwa kwa tuzo hiyo ni ishara ya kutambua na kuthaminiwa kwa mchango wako katika mapambano dhidi ya rushwa."


Kilango ambaye ni mke wa mwanasiasa mkongwe, John Malecela, alikuwa miongoni mwa wabunge waliosimama kidete bungeni Februari mwaka jana kuhakikisha kuwa viongozi waliohusika katika mkataba tata wa Kampuni ya Richmond na serikali wanaadhibiwa.


Kashfa ya Richmond ilisababisha Waziri Mkuu, Edward Lowassa kujiuzulu na mawaziri wawili, Nazir Karamagi aliyekuwa akishikilia Wizara ya Nishati na Madini na Dk Ibrahim Msabaha aliyekuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
 
JK anaposema: "…CCM na serikali yake, vimetoa fursa pana zaidi kwa wananchi, wanahabari na viongozi, wakiwemo waheshimiwa wabunge, kushiriki kikamilifu zaidi," anamanisha serikali ipi? au ni ile iliyolifungia gazeti la mwanahalisi? au inayopata kigugumizi juu ya kuwapeleka Fisadis Kisutu, e.g EL et al wa Richmond+Dowans, Kagoda n.k, au sijamwelewa vizuri? Au nikujiweka katika kundi la washindi na kuanza kushabikia kuondoa aibu ya kufungwa?
 
- Mods hii iunganishwe na ile nyingine tupate flow nzuri ya kum-celebrate mpiganaji Mama Super K, saafi sana mcheza kwako hutunzwa jamani.

FMES!
 
Back
Top Bottom