Urgent-joto kali

Tricker

Member
Nov 26, 2010
95
25
Wataaalam nina mtoto mdogo wa mwaka mmoja na nusu anajoto kali sna yani ukimshika hivi mpaka anaunguza.nimempeleka hospitali wamemcheki hana maleria wala mkojo wake hana shida sasa anakunywa panadol lakini joto halishuki.pia tunamuogesha maji ya vuguvugu lakini wapi je nini kinaweza kua tatizo?am desperately waiting for your answers wakuu
 
Mkuu kwanza pole sana najuwa mzazi yeyeto huwa anakuwa na raha na amani pale anapoona familia inafuraha vinginevyo full kuhangaika
nakushauli nilikuwa na mwanangu alikuwa na tatizo hilo,mpeleke kwa PROF Masawe huwa anapatikana Hindumadal hospital laikini kwa appointment neda Hindumandal omba appointment na Prof unafanikiwa
Pole sana
Jitu78
 
Nashukuru Jitu78 kwa ushauri

Magonjwa kama degedege, polio na typhoid nayo huleta joto kali. Joto likizidi linaweza kuleta madhara mabaya sana kwa mtoto mdogo ikiwemo brain damage na kupooza. Unapaswa kuwahi sana kwa daktari mahiri hasa wa magonjwa ya watoto. Kila la heri.
 
Naomba nishauri jina la hospitali au jina la dokta ili nimtafute.manake hata huyo nilieenda kwake mara ya mwisho ni specialist lakini hakumcheki typhoid

Magonjwa kama degedege, polio na typhoid nayo huleta joto kali. Joto likizidi linaweza kuleta madhara mabaya sana kwa mtoto mdogo ikiwemo brain damage na kupooza. Unapaswa kuwahi sana kwa daktari mahiri hasa wa magonjwa ya watoto. Kila la heri.
 
Mpeleke mtoto kwa daktari wa watoto na kusiwe na limit ya uchunguzi atakaofanyiwa!

Sio kila kiu inasababishwa na upungufu wa maji kwahiyo ongea na daktari apanue uchunguzi wake.Na ikiwezekana google matatizo yote yanayoweza kusababisha joto kwa mtoto uende na list yako just incase dr akihitaji kufundishwa sijui kukumbushwa kazi yake kidogo ufanye hivyo!!

Poleni pamoja na mtoto ... kila la kheri!
 
je, wewe huna ugomvi na majirani/wafanyakazi wenzako? tangu mtoto azaliwe ulishampeleka kwa wazee? au ulishawahi kumtambulisha mwanao baada ya kuzaliwa kwa wazee wa mtaani?
 
Wataaalam nina mtoto mdogo wa mwaka mmoja na nusu anajoto kali sna yani ukimshika hivi mpaka anaunguza.nimempeleka hospitali wamemcheki hana maleria wala mkojo wake hana shida sasa anakunywa panadol lakini joto halishuki.pia tunamuogesha maji ya vuguvugu lakini wapi je nini kinaweza kua tatizo?am desperately waiting for your answers wakuu

Mkuu kuwa mwangalifu sana na watoto..na madawa.. Kama umeenda kwa Dkt na kuona hakuna kitu..jaribu kusubiri kwa siku moja au mbili zaidi..Sometime watoto wanapata infection ambazo zinaisha zenyewe.. Kumlimbikiza mtoto madawa kunaua uwezo wa mtoto kujitengenezea kinga zake mwenyewe..

ushauri...Tulia ..ila uwe 24 hrs alert.. mkipokezana kulala wewe na mkeo kupunguza joto ..ingawa ujasema ni nyuzi joto ngapi...Usimshauri dkt akupe dawa au kubadili hosptali ili tu kupata dawa...utamjaza sumu mtoto wako..
 
Alikua na 39.3 degrees,thanx kwa ushauri jamani saivi joto limepungua lakini ni baada ya kumpeleka tena kwa docta.Thanx again for ur concern

Mkuu kuwa mwangalifu sana na watoto..na madawa.. Kama umeenda kwa Dkt na kuona hakuna kitu..jaribu kusubiri kwa siku moja au mbili zaidi..Sometime watoto wanapata infection ambazo zinaisha zenyewe.. Kumlimbikiza mtoto madawa kunaua uwezo wa mtoto kujitengenezea kinga zake mwenyewe..

ushauri...Tulia ..ila uwe 24 hrs alert.. mkipokezana kulala wewe na mkeo kupunguza joto ..ingawa ujasema ni nyuzi joto ngapi...Usimshauri dkt akupe dawa au kubadili hosptali ili tu kupata dawa...utamjaza sumu mtoto wako..
 
Narubongo sina hakika kama unatania au upo serious mbona huu ushauri umekaa ki-CCM sana en very close to uchawi

je, wewe huna ugomvi na majirani/wafanyakazi wenzako? tangu mtoto azaliwe ulishampeleka kwa wazee? au ulishawahi kumtambulisha mwanao baada ya kuzaliwa kwa wazee wa mtaani?
 
Thnx Lizzy kwa ushauri,thnx God mtto anaendelea vizuri baada ya kurudi tena kwa dokta

Mpeleke mtoto kwa daktari wa watoto na kusiwe na limit ya uchunguzi atakaofanyiwa!
Sio kila kiu inasababishwa na upungufu wa maji kwahiyo ongea na daktari apanue uchunguzi wake.Na ikiwezekana google matatizo yote yanayoweza kusababisha joto kwa mtoto uende na list yako just incase dr akihitaji kufundishwa sijui kukumbushwa kazi yake kidogo ufanye hivyo!!

Poleni pamoja na mtoto ... kila la kheri!
 
pole sana. Kama uchunguzi haujaonesha kuwa na any infection in this case bacterial then rest in peace kwani atapona. But most importantly mchunguze mwanao vizuri ATAKUWA ANAOTA MENO. In that case anachohitaji mtoto ni paracetamol na maji kwa wingi! But all in all mshauriane vema na daktari wako! Pole na mtoto
 
ndg,hiyo hali huwa inatokea kwa watoto,hata miimi imeshawahi kunitokea kwa mwanangu nikampeleka kwa GP,baada ya vipimo akaonekana hana tatizo,ila si vizuri kumkanda na maji ya baridi 'eti' kushusha joto,hii ni mbaya na inaweza kumletea degedege..maadam ulishampeleka hosp basi kuwa na subira,na unapompeleka kwa dokta mwingine basi kuwa muwazi kwa dawa alizotumia au ikibidi nenda nazo ili usije kumzidishia mtoto dose bila kujua.pole na kuuguza
 
Pia inaweza kuwa ni tonsiz, la sivyo be aware pia na huyo yaya wake, jaribu kuomba ruhusa even a week ukae naye wewe mwenyewe tena utaona.
 
Nadhani mtoto wako atakuwa amepata nafuu ya kutosha sasa. Nilikuwa nje ya mtandao kwa muda.
Mimi si daktari, lakini nakushauri yafuatayo:
Kwanza hakikisha mtoto ananyonya kadri inavyowezekana au mpe juice ya matunda (passion fruits)usiichanganye na sukari. Haya mawili ni kuhakikisha joto lile halisababishi upungufu wa maji mwilini kwani yakipungua sana ataanza kutapika.
Daktari acheki tena malaria, typhoid, na kama uko sehemu zenye kawaida ya homa ya uti wa mgongo, basi nayo waiangalie.
Daktari pia acheck kiwango cha damu.
kama ulivyoshauriwa na wengi, usibadilibadili hospitali mara kwa mara, hadi docta mhusika akuruhusu.
Paracemol ni dawa nzuri ya kumpa wakati unampeleka hospitali; usiitumie kama tiba.
Pole sana ndugu yangu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom