Idimi
JF-Expert Member
- Mar 18, 2007
- 14,963
- 10,457
Kwa Tanzania sidhani kama tunaihitaji teknolojia ya nyuklia kwa sasa, na niliwashangaa sana wabunge wetu walipopitisha sheria hii miaka kadhaa iliyopita. Sijajua walikuwa wanafikiria nini hasa. Nasema hivyo nikiwa na misimamo ifuatayo:
1. Usalama
Kwa jinsi hali ya usalama ilivyo tete kwa nchi masikini kama Tanzania, utunzaji wa masalia ya nyuklia kutoka katika vinu vyake hatutauweza kwa sasa, kwa sababu bado hatujaonyesha uwezo huo kwa teknolojia nyingine tulizo nazo. Mfano tumeshindwa kutunza treni zetu, ambazo teknolojia zake ni rahisi, itakuwaje kwa teknolojia tata ama hii ya vinu vya nyuklia? Tumeshindwa kutunza viwanda vinavyotumia teknolojia rahisi alivyotuachia Mwalimu Nyerere, itakuwaje kwa teknolojia tata kama hii? Tumeshindwa kutunza jenereta za dizeli tulizo nazo, nyuklia tutaiweza? Naogopa yasije yakatukuta kama yale yaliyotokea katika mji wa Chernobil nchini Urusi mwaka 1986, ambapo kutokana na uzembe wa baadhi ya watu, kinu kilivuja na kusababisha hasara na maafa ambayo bado yanadumu mpaka leo.
2. Mahitaji ya Nishati
Kwa Tanzania, bado hatujavuna nishati za maji, jua na upepo kwa matumizi ya nishati kiasi cha kulazimika kutumia nyuklia kwa kuzalisha nishati. Nasema hivi kwa sababu bado sirikali inasuasua mpaka sasa kuendeleza miradi ya nishati za nguzu ya maji kama vile mradi wa Rumakali uliopo wilayani Makete (222 Megawatt), mradi wa Stiegler's Gorge (358 Megawatt) na mwingine ulipo wilayani Njombe (100 Mgawatt). Sasa basi, iwapo tungekuwa tumeendeleza miradi yote hii mikubwa ya umeme na bado kukawa na mahitaji, basi tungekuwa na sababu mwafaka ya kufikiria teknolojia nyingine kama nyuklia, lakini kwa sasa mie naona bado sana.
3. Nguvu ya Kiuchumi Uchumi
Kwa Tanzania masikini kama hii ninayoifahamu mimi, ambayo asilimia arobaini ya bajeti yake inategemea hisani ya wafadhili kutoka nje, itakuwa ni kicheksho na mzaha kufikiria teknolojia ya nyuklia, kitu ambacho huwa kinagharimu pesa nyingi sana kukiendesha. Kama hatuwezi kujenga mitambo ya nguvu za maji ambayo ni bei rahisi, kama nilivyodokeza hapo juu, itakuwaje kwa teknolojia ya nyuklia ambayo huhitaji pesa nyingi? Huu ni mzaha, tena wawazi kabisa.
4. Nishati Mbadala
Kama nilivyodokeza hapo juu, tuna vyanzo mbadala vingi sana vya nishati kama vile nishati ya jua, upepo na mkondo wa bahari, kwa hiyo basi hakuna ulazima wowote wa kuikimbilia teknolojia ya nyuklia kwa ajili ya uzalishaji wa nishati. Itakuwa ni matumizi mabaya ya kile tulichonacho.
5. Kipaumbele
Kwa wakati huu, kuwa na mitambo ya nyuklia isiwe kipaumbele, nadhani hii pesa ambayo tunapanga kuendelezea teknolojia hii ingepelekwa katika upatikanaji wa huduma za afya, miundombinu na elimu ambavyo ndio tunavihitaji sana kwa sasa kuliko hio nyuklia.
Hitimisho
Siungi mkono kabisa Tanzania kuwa na teknolojia ya nyuklia kwa sasa. Najua huenda wanasiasa wasiyasome maoni haya na kuyapa umuhimu, lakini nashukuru kwamba nimetumia haki yangu kama Mtanzania kufikisha kwa jamii kile ninachoona kinafaa kwa taifa kwa sasa, kuliko kung'ang'ania sifa na ujiko.
Nawasilisha.