Napata taabu sana kuelewa statement hapo juu. Ninahisi akina Mdee na Nassari waliongea yale maneno. Zitto (na wahariri wa Mwananchi) walizipitia tape kwa umakini mkubwa sana na wana uhakika wapo sahihi. No wonder habari imechukua siku 6 kutoka. Ninahisi mtafaruku mkubwa ndani ya chama utafuata...
Very likely. Video itasaidia kujua kama kweli waliyasema, basi walisema katika mazingira gani? waliuzwa swali (leading question) na mwandishi wa habari au ilikuwaje? tusubiri.
Hata hivyo hii saga yote imekujaje? Kwanini hili tukio limetokea, na limetokea sasa? Nassari ana nguvu sana kwa vijana, je, hii saga inamwacha wapi? Na aliingiaje kwenye hii issue yote? Maswali ni mengi mengi sana, nimejikuta naanza hata kujiuliza bajeti na zile 0.