Urais, Halima, Nassari na Kigoma

Status
Not open for further replies.
Siyo kweli....JK aliutaka saaaaaana na akaupata. Leo Lowassa na Zitto wanautaka saaaaaana na wataupata. Kumbuka
kuwa Tanzania na wananchi wake ni shamba la bibi....sijui tumelogwa!

No JK Hakuutaka sana, na kwa taarifa, baada ya lowasa kubaini ugumu wa yeye kutokuwa rais bila kuanzia kwenye uwaziri mkuu ili afute sumu za nyerere ndio alifanikisha Kikwete kuingia Ikulu.

Kikwete asingeweza kwa utashi na uwezo wake binafsi kupambana na fitna za Mkapa, Mangula na Sumaye, ndio maana kwa mara ya kwanza kwenye uchaguzi wa mwaka 2005 zilitumika pesa nyingi sana kwenye uchaguzi katika historia ya nchi yetu huku yeye Mwenyewe Jakaya akiwa hana thumni, pale lowasa alijua na kuamini kwamba unknowingly Watanzania walikuwa wamemchagua yeye kuwa rais, na oficially angeapishwa 2015, Ndio maana Jakaya hajawahi kubehave kama president ever toka ameingia ikulu, anang'amuang'amua macho tu, hajui afanye nini, aseme nini, amebakia kumshukuru Mwenyezi Mungu tu basi.

Zungumzia Lowasa, Lipumba, Mrema, Malecela, Mwandosya.

Amini nakuambia nchi hii, hawa hata na ZITTO hawatakuwa marais wa nchi hii, ila Naodha akawa; sijui kwanini naamini sana hii trend.
 
siku wako kigoma wakati halima anaongea huyu jamaa alitoa machozi!!! yalikuwa machozi ya nini ?
 
Mimi ina swali dogo tu ndugu Zitto, ni kweli ulitoa chozi kutokana na maneno ya Mdee?
 
Last edited by a moderator:
kwa hiyo unathibitisha pas na shaka kuwa halima na nassari walitamka maneo hayo?!!..wewe kama wewe unazungumziaje makanusho yao


Kwa mujibu wa maelezo ya Mh Zitto, Mh Halima na Mh Nassari waliyasema haya. Hapa Mh Zitto kaleta mkanganyiko mwingine! Kwamba katika CDM kuna viongozi huwa wanaongea hadi wanasahau wameongea nini!
Weka hiyo video yako kwenye jf pia ambako huu mjadala umekuwa mkali sana. Hofu wasijekuja na kusema umechakachua hiyo video.
 
Hongera sana sana Zitto kwa kuja hapa na kutolea swala hili ufafanuzi wale waliokuwa wanataka kupandikiza migogoro ndani ya chama kwa habari hii naamini mmepata majibu chadema hakina wala akifikirii urais kwa sasa na tabia ya kusema flani anatengwa ama atendewi haki sasa ife.

Hongera tena mh. Zitto naibu katibu wangu kwa kulijibu swala hili kiufasaha zaidi.M4C daima
 
Last edited by a moderator:
Unacheza na maneno wewe Zitto! lazima una hila nyuma yako! kumbuka wakati wa uchaguzi mdogo wa arumeru mashariki uliibuka na maneno yako haya tata kama mchawi!! kwamba unautaka urais!! yani watu tuko biz tunahangaika kuhakikisha Joshua anapita katika AM, wewe ukaibuka ki vile, tafsi ya wengi wetu ilikuwa wewe ni kuadi unatumika tu na wa upande wa pili! ili kutunyongesha kulichukua jimbo hilo au we unafikiri logic hasa ilikuwa nini katika uchaguzi ule we kuibuka na kaule kama ile?

Haya hata hayo ya upuuzi wk hayajakauka leo linazuka hili!
Zitto wewe ni mtata sana, tena mnafiki mkubwa!
Hila mbaya kama hizi za kuuendea uongozi mkuu wa nchi yetu leo zinamtokea JK puani! hata kama kajilimbikizia mali kiasi cha kutisha hana heshima tena! atabakia kuwa kiongozi wa ovyo aliyeshindwa kuliongoza taifa lake na watu wake!

Haya we endelea tu! lakini kumbuka siku zote mwisho wa ubaya ni aibu!
JK sasa anaaibika! Tafakari!

Mkojo, asante kwa kukumbushia kauli ya Zitto kuhusu kuutaka urais wakati watu wanahangaika Arumeru kumpigania kamanda Nassari.
Hii ilitushangaza wengi wakati ule. Haikuwa timing nzuri. Au ilikuwa ndiyo 'timing' nzuri? (distraction)?
 
Ninachokiona hapa Zitto anawajibia Mwananchi.Ukisoma taarifa yote ya Nassari na Mdee hakuna mahali popote wanamtaja Zitto bali wanakanusha habari ya gazeti kuwalisha maneno.Sasa ningemshauri Zitto awaachie Mwananchi wathibitishe au wakanushe madhali kasema hakualika waandishi.Hiki anachokifanya Zitto nadhani ni kuanzisha vita isiyo na maana yoyote kati yake na wabunge hao wa chama chake.Huo ni ushauri wangu kwake.


Well said mkuu. Halima na Nasari wamelalamikia Mwananchi, siyo Zitto! Sasa inakuwaje Mh awajibie mwananchi? Au na yeye ni sehemu ya Mwananchi? Maana hata katika utetezi wake kaipromoti sana mwananchi.
 
UNASEMA MGOMBEA URAIS BADO HAJATANGAZWA WKT UNAJUA DR SLAA NDO MGOMBEA. HII YOTE INAONESHA JINSI ULIVYO KOSA STAHA DR. NA CDM KWA UJUMLA.

KWA KUKOMALIA URAIS HATA KIPINDI TUPO ARUMERU KWNY UCHAGUZI MDOGO.

Sijui wengine wanakuonaje ila mi nakuona ni kijana mnafiki na hatari kwa CHADEMA na TZ na uwepo wako ni faida kwa CCM.
 
reputation ya Zitto inapungua kila siku na yeye andhani hii Tanzania ni ya wanafiki na wajinga kama wa enzi zile, walikuwepo wa kina Kikwete na walikuja na mbwembwe zote ili wapendwe lakini leo wako wapi? na Kikwete ndio kiongozi anayechukiwa hapa Tanzania sasa na huyu Zitto ameanza kuvimba kichwa kwa kujiona yeye anajua kila kitu ipo siku atakua kama barafu kwenye jua...
 
Miezi ya nyuma nilileta hii mada hapa jukwaani lakini kwa bahati mbaya MODs waliinyofoa dakika 20 baada ya kuiweka. Sina budi kurudisha hii mada baada ya sakata la Zitto Kabwe, Nassari, Alima Mdee pamoja na gazeti la Mwananchi. Kwa muda wa miaka kadhaa sasa, nimekuwa katika tasnia ya habari na lazima nikiri kwamba mengine yanayofanyika katika hii tasnia ni ya kukatiza moyo hasa kazi za wanahabari zinapoingiliwa na wanasiasa. Kwetu sisi wanawake inakuwa ni vigumu sana kukataa kutii haya maagizo ambayo mengine unaona kabisa ni za vitisho

Zitto Kabwe, January Makamba, Bernard Membe na hata Ngeleja kwa siku za nyuma alishiriki sana katika kuingilia kazi za waandishi. Kinara wao akiwa Zitto January na Membe. Hawa viongozi hasa Zitto wamezoea sana kujiandikia makala na hata habari kisha kumlazimisha mwandishi kuzichapisha ukurasa wa mbele kwa gharama yoyote ile. Wanatoa hela nyingi sana kwa waandishi na wahariri. Mbaya zaidi ni kwamba hawa viongozi wanajitengenezea kashfa au kutoka ndani ya vyama vyao.

Matokeo yake kesho wanaitisha waandishi tena kukanusha (kashfa) zao za kujipikia wakati ni wao ndio chanzo cha hizo habari. Lengo lao kubwa ni kutafuta huruma kutoka kwa umma wa kitanzania kwa vitu ambavyo havipo.

Kinachonishangaza ni kwa nini mtu ajichafue kwa kujitengenezea kashfa maadui feki ndani ya chama chake heti ndio wanaomchafua kumbe ni yeye mwenyewe alafu kesho yake akane hizo taarifa? Nadhani tunaelekea kubaya hawa watu wakiendelea nah ii tabia. Moja ya habari hizi ni zile zinazomlaumu Mbowe kam mtazikumbuka..

nawakilisha


Funguka funguka Mama Muke Ya Muzungu
 
Last edited by a moderator:
@Zitto kama kweli una dhamiri nzuri kwa watanzania, kwa nini unakimbilia IKULU?

...Kinyume chake ni sahihi, kama una dhamira nzuri kwa Watanzania na hauridhiki na hali iliyopo sasa then Ikulu ndio sehemu nzuri zaidi ya kuifanyia makubwa nchi na wananchi wake..

...Kwa wanasiasa waliopo sasa, Zitto yupo vizuri sana kuliko wengi waliopo, na sioni kwanini iwe tatizo kwa Mwanasiasa Makini kama Zitto kuwaza kuwa Rais,go Zitto...
 
Hachaneni na siasa nyie.Kila mtu anatafuta maslai pitia siasa hii.Ndo maana watu wengi hawapigi kura make siasa inachosha mno.
 
Dah.....i used to thought wewe ndo tumaini la watanzania and the big reason because ulikuwa mwanasiasa bora chadema ambako wengi ni wanaharakati....ivi did it ever occur to your mind ukute wenzako nassari and halima wamekana kutoyasema ayo kukitunza chama????.....as u said siasa za urais hazijaanza ya nini kutoa video inayokusifia wewe na kukivuruga chama?????...Grow up your future is bright moto wa nin??? utaunguza vinavyokusaidia......
 
...Kama akina Halima na Nassari wameyakana waliyoyatamka wamedhihirisha kuwa ni wanasiasa wasiojua wanachokiamini, na wanaoweza kuongea wasiyoyaamini, hii ni aibu kwao na kwa wananchi waliowachagua...

...Mara nyingine tena inajidhihirisha jinsi tulivyo na kundi kubwa la wanasiasa makondoo wasioweza kujisimamia wenyewe,wapo kwenye vyama vyote, lakini atleast tuna wanasiasa wachache wanaojua thamani ya maneno yao, hongera Deo Filikunjombe kwa kusimama kwenye maneno yako...
 
Muheshimiwa Zitto lakini nakumbuka pia katika speech yako ya kuzindua hili kundi uliloliita Kigoma all Stars uliwaambia unataka kuwajengea uwezo ikiwa ni pamoja na kuwakatia NSSF ili baadae waje wakusidie katika kampeni zako za Urais, sasa nikijumlisha na haya yaliyoandikwa na Mwananchi nakuwa sina shaka na nia yako juu ya nafais ya Urais!
 
I fail to understand why people always panic whenever Zitto Kabwe is associated with the presidency. Tatizo ni nini hasa? Zitto amesaliti vipi chama chake kwa kuutaka urais? Na kuna ubaya gani Zitto akigombea uRais au akiwa Rais? In my opinion more than any other politician Zitto has proved that he has the skills, capability,vision, knowledge and experience to lead this country. Yes he is outspoken and he will not hesitate to speak his mind. Through his character we have been able to understand and know him better than any other politician. Tunaelewa na kujua msimamo wake. After all he has done for this country, we instead choose to smear him with slander and call him all sorts of names...eti msaliti? Msaliti? Amemsaliti nani na kivipi? Nyinyi mnaomutia majina, what have you done for your country? Yaani with all the issues confronting this country, we choose instead to focus on who said what about Zitto and the presidency. Hivi tumekuwa watu wa aina gani? Yaani mna sakama mtu just because gazeti lime quote matamshi ya wabunge wenzake? Bro Zitto wewe endelea na mapambano!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom