I believe Zitto is a controversial politician.
Mh.Zitto wakati wa kampeni za 2010 watu wengi wapenda mabadiliko yenye maslahi kwa taifa tukiwa busy kumnadi Dr.slaa kuwa Rais,nilikuona kupitia taarifa ya habari ukisema 2015 utagombea urais kwangu hiyo ilikuwa ishara ya kutokuwa pamoja na wengine kwenye chama,wakati wa kampeni za arumeru watu wako busy kumnadi Joshua wewe unaongea habhari za urais....kwa kifupi haya yananisababisha nisikuelewe kabisa kama kiongozi wa CDM LABDA KAMA UTAFAFANUA LABDA NAWEZA KUKUELEWA ila kinyume na hapo kama CDM wakikupitisha kama mgombea wao 2015 ntamchagua mgombea yeyote wa CCM NA KADI YANGU YA CDM NITAIRUDISHA HADHARANI.Sina chuki yeyote na wewe lakini mambo unayoyaibua katika wakati ambao kwangu unaonekana sio muafaka yananisababisha niondoke kwenye hiyo list ya wanaokuunga mkono.Nilikuwepo uwanjani pale lake Tanganyika Kigoma, kilichoandikwa ndicho nilichosikia pia. Videos zitawekwa hapa na zitathibitisha.
Siwezi kuwaandikia mwananchi kwani mimi silalamiki kuhusu habari hiyo. Wenye kuilalamikia habari wameandika.
Mimi ninaamini gazeti la Mwananchi ndio gazeti pekee huru la kiswahili hapa nchini. Ndio gazeti pekee ambalo umiliki wake hauna maslahi na waandishi na wahariri wake ni mahiri, hawana njaa na hawapindishwi. Ndio maana huandika ukweli muda wote na wanapokosea hawasiti kurekebisha. Ndio maana ni gazeti linasomwa kwa wingi kuliko magazeti yote nchini. Hakuna gazeti linalofikia hata nusu ya mwananchi kwa kusomwa. Hivyo Mwananchi linaaminika na umma.
Najua kuna watu wana chuki binafsi na mwananchi kama gazeti na wahariri wa mwananchi kama binaadamu. Hayo wayamalize wenyewe huko walikochukiana.
Subirini video ndio tutajua habari ile imepikwa au ni ya kweli. Kwa tuliokuwepo uwanjani tunajua nani alisema nini.
Mwanzoni kuna video iliwekwa huko kunakodaiwa lakini baada ya sakata hili kuchukua sura mpya, video yenyewe pamoja na jitihada zangu ilikataa kucheza hata kwenye mtambo wangu ninaouamini. Wasi wasi wangu ni moja tu, je kuna mtu aliistukia na sasa marekebisho madogo madogo inabidi yafanyike kwanza? Hata hivyo tuwe na subira....hiyo ''fideo'' bado tu
Mimi binafsi kati ya vitu vinavyonipa shida sana kufahamu ni msimamo wa Zitto Kabwe kuhusu mwelekeo wa nchi yetu hasa kuhusiana na jinsi anavyokinzana na mambo mengi sana ndani ya chama chake.
Zitto wewe ni economist, hivyo unapaswa kukaa chini na kuanalyse mwenendo wako na misimamo yako na kufanya maamuzi. Mimi nashawishika kuamini kwamba wewe uko sehemu siyo stahili yako kulingana na tabia ambayo umekuwa nayo siku zote. Zitto nashawishika kuamini kwamba CHADEMA siyo mahali panapokufaa, kwasababu unatofautiana nao kwa mambo mengi sana. Hivyo mimi nakushauri fanya maamuzi na ujiunge CCM labda huko utatimiza ndoto zako. Nasema hivyo kwasababu naamini hata Viongozi wenzako ndani ya CDM huna imani nao, ndiyo maana historia yako imejaa mambo mengi sana kinyume na mwelekeo wa chama chenu.
Zitto, kati ya vitu ambavyo siamini kama hata wewe unaamini ni wewe kuwa na uwezo wa kuongoza nchi kama TZ kwasasa na changamoto nyingi tulizonazo. Kwa nafasi yako na uwezo wako, bado huna uwezo wa kuwa Amiri Jeshi Mkuu mwaka 2015 lkn unaweza kuwa sehemu ya timu itakayowaletea watanzania mabadiliko ya kiuchumi na kijamii kutokana na uwezo wako. Lkn ukishakuwa ndani ya timu ya utendaji, hapo 2020 na kuendelea sasa unaweza ukawa na akili na uwezo wa kutimiza ndoto yako.
Zitto, tanzania ya sasa ilipofikia inahitaji mtu mwenye msimamo na asiyeyumbayumba kama ulivyo na rangi nyingi katika utendaji (rejea yanayoendea PPF na wewe kama mwenyekiti wa kamati husika lkn umewekwa mfukoni na Urio kwasababu tu anakupa support ya pesa wkt pale kuna uozo mkubwa sana).
Zitto, kuna watu wanakupoteza na kukudanganya kwa mwamvuli wa UDINI, UKANDA NA UKABILA na wewe unaykumbatia. Hii siyo ajabu kwani propaganda ya CCM siku zote ndiyo hizo lkn wewe pia nikichunguza kwa makini nagundua kwamba unakubaliana na hizi hoja hafifu hata kama kuna kitu kikitokea, basi watu wasiseme kisa UDINI na wewe huyu mdudu mbaya wa UDINI haujawahi kuukemea kabisa kwa kuwafafanunulia watu. Na kwa mantiki hiyo tunashawishika kuamini kwamba wewe unatumia hii dhana ya udini kama mtaji kwako kwa mambo ya kipuuzi ili upate sympathy ya wale wasiotaka kushugulisha akili zao.
Pole sana kwa kutotaka kutoka ndani ya Box bila kujua gharama ya kuwa na rangi nyingi katika dunia ya leo.
TELO.
huyu jamaa hana video anataka kutuaminisha tu kwa porojo zakehiyo ''fideo'' bado tu
huyu jamaa hana video anataka kutuaminisha tu kwa porojo zake
Ukiangalia blog yake kaweka video za tamasha tar 19/07/2012,kaupload video za wasanii wakiwa jukwaani,kama hi video anayozungumzia ipo kwanini hajaupload mpaka leoyuko twittere huko bize na kusambaza taarifa za kifo cha rais wa ghana.
...Hotuba za Wabunge wote zilirekodiwa kwenye video neno kwa neno na video hizo zitawekwa ........kama mwandishi kaandika ambayo wabunge hawa hawakuyasema basi itaonekana kwenye videos hizo. Wabunge wenyewe wanajua kwenye nafsi zao nini walisema Kigoma na kipi kiliwasukuma kusema walioyasema Kigoma...
Niliwaonya CDM kuwa lazima chama kisimame kama taasisi inayoongozwa na sheria, kanuni na maadili. Hapa ndipo CDM ilipo leo!
Ukiangalia blog yake kaweka video za tamasha tar 19/07/2012,kaupload video za wasanii wakiwa jukwaani,kama hi video anayozungumzia ipo kwanini hajaupload mpaka leo