Naendelea sasa na nitaendelea tena kesho kuupinga Uraia wa Nchi mbili . Wazungu ndiyo model yetu ya maendeleo nadhani kila mara we must site them as an example hadi kufika hapo hawakuhitaji uraia wa Nchi 2. Wamefika hapo kwa kuuthamini uraia wao na kuachana na mawazo ya kifisadi na matendo ya kifisadi. Unaweza kupeleka pesa Tanzania hata sasa na watu wamekuwa wakipeleka pesa TZ kabla ya hata wazo la uraia wa Nchi 2.
Hapa Membe anaongeza speed mtaona sasa watakavyo kuja watoto wao kuchukua madaraka na kueneleza utawala waoa kwa manufaa yao . Uraia wa Nchi 2 hivi itakuwaje kwa ajira za polisi, usalama wa Taifa , jeshini nk ?Mnaongelea Waghana kupeleka pesa hizo kwao wakati hata sisi watanzania tunapeleka na baadaye wazungu wanapeleka mabilioni lakini bado tuko hata kadi za kupiga kura ughaibuni wala access ya kuchagua ukiwa ughaibuni haipo . We are not serious na dual is never an answer.
Lunyungu,
Jibu hoja ya Waziri, je ungelikuwa wewe, utamnyima uraia huyo Mtanzania ambaye kaamua kuchukua uraia wa Canada ili watoto wake wagonjwa watibiwe?
Mifano ya namna hiyo iko mingi sana na ndio inawafanya watu wachukue uraia wa pili.
Watu hapa kila wakiambiwa wapeleke bank stament wanakuta overdraft kila mwezi zimetumika, kama ni kwenye visa jibu ni NO. Watu kama hao ndio inafika mahali wanaona ya nini shida?
Utasema watu kama hao ni watoto wa vigogo? Mtoto wa fisadi amejaza pesa bank unafikiri anahaja hata ya kuhangaika na uraia wa nchi mbili?
Mimi Watanzania ambao najua wana magamba ya hapa UK, kwa asilimia 90 ni watoto wa watu wa kawaida tu Tanzania ambao kwa sehemu kubwa hawa vijana ndio wanawasaidia hata wazazi wao kuishi kule nyumbani.