Upungufu wa Dawa za malaria nchini je, Usimamizi mbovu au Uzembe? Hii nchi nani katuloga?

mzee wa njaa

JF-Expert Member
Jun 16, 2011
1,366
223
Upungufu wa Dawa za malaria nchini je, Usimamizi mbovu au Uzembe? Moyo unasononeka sana pindi nilipopata taarifa hii huko nchini Tanzania yaani usambazaji wa dawa za Malaria umekuwa duni hali iliyopelekea nchi kuingia katika matatizo wagonjwa wengi wanakufa pasipo kupata Dawa za Malaria.

Tunaelekea wapi hivi sasa!!!! Inauma sana tena sana wakati mwingine mtu unaweza kujuta kuzaliwa Mtaznania kwa mambo ya kipuuzi kama haya. Je, wakulaumiwa ni Health Focus wanaohusika na kusambaza dawa, Wizara ya Afya au MSD? Mi nadhani kuna sehemu kumekosa uwajibikaji kwa kweli. Kwa karne hii ya leo tunajiuliza hivi ni kweli Wananchi wa Tanzania wanatendewa haki na serikali yao? Inauma sana kusikia hiki kichefu chefu.

Lazima wahusika wawajibike, kwa hili nchi hii nani aliyetuloga jamani? Nalo hili tunahitaji muwekezaji katika usambazaji?

Kwa taarifa ya Msd serikali inaagiza dawa za malaria 40% na Kampuni binafsi 60%, je hii inatupa picha gani? Wizara husika imeshindwa kazi au? Huu ni uonevu wa wazi kabisa.

Usimamizi ni mbovu na tena ningeuita usimamizi ulio oza tena sana. Je, Waziri sijui na yeye kama atakuwa na pa kutokea au ingekuwa vyema WAZIRI HUSIKA NA WATENDAJI WAKUU WA WIZARA PAMOJA NA MSD WAWAJIBIKE.

Nawasilisha hoja ingawa roho inauma sana.
 
...Serikali yote hii ni ya kufukuza kazi. Unadhani wenyewe wanajali na hali hii!? Wakiugua hata mafua tu wanaenda SA au India kwa matibabu hivyo hili la kutokuwepo kwa madawa ya malaria haliwahusu kabisa....halafu bado wanatamka hadharani kwamba watatawala Tanzania milele!!!! Sijui kwa lipi walilolifanya hadi wastahili kutawala milele
 
point noted.
 
Back
Top Bottom