Upotoshaji huu wa Mwigulu Nchemba ni kwa faida ya nani?

critical

Member
Apr 4, 2012
17
11
Leo asubuhi nimefuatilia mahojiano yaliyorushwa na TBC 1 ukiwashirikisha Mwigulu Nchemba na Zitto Kabwe. Mpango wa maendeleo wa taifa uliopitisha mwaka jana na bunge na kusainiwa na raisi unaanisha wazi kwamba kwa kila bajeti serikali itatenga 35% ya mapato ya ndani kwa ajili ya mipango ya maendeleo. Zitto anaanisha wazi kwamba mwaka huu fedha iliyotengwa kutoka mapato ya ndani ni 0% kinyume na mpango huu hivyo kukiuka azimio la bunge.

Kwa upotoshaji mkubwa Nchemba anasoma mpango wa kiingereza anapotosha kuwa si 35% ya mapato ya ndani bali ni 35% ya bajeti. Ila Zitto anasoma mpango wa kiswahili ambao unaonyesha wazi ni 35% ya mapato ya ndani. Pia bado kwenye hiyo bajeti hiyo 35% ya bajeti kwenye mipango ya maendeleo haionekani. Nchemba anakusanya hadi bajeti yote ya elimu kuongezea walau apate hiyo 35% bado haifiki licha ya kuwa hela nyingi kwenye elimu si maendeleo bali matumizi ya kawaida.

Swali langu hapa je upotoshaji huu wa Nchemba ni kwa faida ya nini? Ni kwa ajili ya kutaka bajeti ipite hata kama haina uhalisia na hata kama inakiuka maazimio ambayo yamepitishwa na bunge?

Nadhani Nchemba anasahau kuwa wananchi wa sasa hivi sio wale wa kuburuzwa tu kwa faida ya chama tawala.
 
Hivi huyu Nchembi ndiye anashikilia kitengo cha propaganda ndani ya ccm kwa sasa? kama sio hiyo degree ya uchumi anayotambia inamweka ktk kundi la wachumi ama wasomi kweli?
 
Hivi na nyie mna muda gani kuzungumza mambo ya huyu mzinzi. Myakuwa kama yeye shauri yenu.
 
Huyu jamaa ninawasiwasi sana na shule yake. hata mtu mwenye degree ya PASS hawezi kuwa na mtizamo wa huyu jamaa. Nimeshapata jibu, kwanini alikimbia BOT na kujiunga na kitengo cha Propaganda kwenye siasa. Inaelekea hata hiyo 1ST CLASS yake ni propaganda tu (Desa.com)
 
Jana na Juzi alikuwa anasimama na kuomba kutoa "TAARIFA" na kudiriki kuwadharau Mh. Tundu Lissu (juzi) na Mh. Mughwai (jana)! Inasikitisha saaana kwa mtaalamu huyu kutoona kuwa bajeti haitekelezeki. Mimi nadhani kujifaragua kwake bungeni anataka apewe uwaziri. CCM ni zaidi ya tuijuavyo!
 
Nchamaba amejidhalilisha na amewadhalilisha hata waliomchagua na baya zaidi amewadanganya watanzania na kuwapotosha, sikutegemea Nchemba kuwa angeongopa hata ktk mambo ya msingi kabisa ktk nchi yetu. Niliwasikia asb na tbc na upendeleo wa dhahili kwa nchemba awaongopee watanzania Shame to Nchemba , shame to tbc
 
acheni upuuzi wenu ata kama tunahitaji mabadiliko lakini kilichotokea kambi ya upinzani ime fail ku adress bajeti mbadala inayo kidhi mahitaji au ambayo inaweza kuwa bora zaidi ya CCM.na kwa hili limetuonyesha ikitokea tukawapa madaraka CHADEMA nchi hii itaharibika na kusambaratikia mballi maana izo takwimu wanazozitumia kutengeneza baieti hazina uhalisia yani ni ku copy na ku paste kwenye twiter na jamiiforum hawafany critical reserch hwaumizi kichwa wanaweza kutupeleka sehemu mbaya zaidi ya hapa tulipokua na CCM.
MFANO MMOJA ETI KIMA CHA CHINI NI 310,000.EBU CHUKUA WALIMU+MADACTARI+HALMASHAURI=< TRILIONI 15?
 
Uzinzi... uzinzi ali/ame zini na nani? uli/mli mshikia mguu au ni dada yako?
 
Mimi nashindwa kuelewa hawa wachumi wetu hasa wanaojitapa kuwa wamepata first class walipotunukiwa shahada zao mpaka hapa tulipo wamelisaidia nini taifa hili na hzo first class degrees zao au ndo wamezidi kuitumbukiza nchi kusikoeleweka naongelea baadhi sio wote lakini,ukiangalia scandles zilizo Centre bank unaweza kulia na ndio hao vipanga wetu wanangoza idara mbalimbali pale mimi nadhani ni kwasasa watanzania tuache kulalamika kila mtu afanye kinachostahili kufanywa hawa wanasiasa uchwara watashindwa hata jinsi ya kutuongopea.Haiwezekani kila mwanasiasa akawa ni mchumia tumbo kwa nafasi aliyonayo badala ya kuangalia maslahi ya wengi.
 
Zitto alimban kisawasawa hadi akajaribu kudai kuwa fedha za barabara ziko katika matumizi ya kawaida. Kama fedha za barabara ziko katika matumizi ya kawaida fedha zilizo katika wizara ya Ujenzi ni zipi? Ni vyema kila mtanzania tukajifunza kusoma hizi bajeti ili wapuuzi kama Mwinguku wasiweze kuudanganya umma. Hii ndio faida ya upinzani.
 
acheni upuuzi wenu ata kama tunahitaji mabadiliko lakini kilichotokea kambi ya upinzani ime fail ku adress bajeti mbadala inayo kidhi mahitaji au ambayo inaweza kuwa bora zaidi ya CCM.na kwa hili limetuonyesha ikitokea tukawapa madaraka CHADEMA nchi hii itaharibika na kusambaratikia mballi maana izo takwimu wanazozitumia kutengeneza baieti hazina uhalisia yani ni ku copy na ku paste kwenye twiter na jamiiforum hawafany critical reserch hwaumizi kichwa wanaweza kutupeleka sehemu mbaya zaidi ya hapa tulipokua na CCM.
MFANO MMOJA ETI KIMA CHA CHINI NI 310,000.EBU CHUKUA WALIMU+MADACTARI+HALMASHAURI=< TRILIONI 15?

Tatizo liko wapi kulipa kima cha chini Shs 310,000/= kwa mwezi. Si ndio hizo hizo wanazolipana posho na safari kwa trilioni 2.7
 
Leo asubuhi nimefuatilia mahojiano yaliyorushwa na TBC 1 ukiwashirikisha Mwigulu Nchemba na Zitto Kabwe. Mpango wa maendeleo wa taifa uliopitisha mwaka jana na bunge na kusainiwa na raisi unaanisha wazi kwamba kwa kila bajeti serikali itatenga 35% ya mapato ya ndani kwa ajili ya mipango ya maendeleo. Zitto anaanisha wazi kwamba mwaka huu fedha iliyotengwa kutoka mapato ya ndani ni 0% kinyume na mpango huu hivyo kukiuka azimio la bunge.

Kwa upotoshaji mkubwa Nchemba anasoma mpango wa kiingereza anapotosha kuwa si 35% ya mapato ya ndani bali ni 35% ya bajeti. Ila Zitto anasoma mpango wa kiswahili ambao unaonyesha wazi ni 35% ya mapato ya ndani. Pia bado kwenye hiyo bajeti hiyo 35% ya bajeti kwenye mipango ya maendeleo haionekani. Nchemba anakusanya hadi bajeti yote ya elimu kuongezea walau apate hiyo 35% bado haifiki licha ya kuwa hela nyingi kwenye elimu si maendeleo bali matumizi ya kawaida.

Swali langu hapa je upotoshaji huu wa Nchemba ni kwa faida ya nini? Ni kwa ajili ya kutaka bajeti ipite hata kama haina uhalisia na hata kama inakiuka maazimio ambayo yamepitishwa na bunge?

Nadhani Nchemba anasahau kuwa wananchi wa sasa hivi sio wale wa kuburuzwa tu kwa faida ya chama tawala.

we unadhani CCM kuna mtu mwenye akili timamu? wote 0 kbs kusoma huyo mchemba sijui chemba alikuwa anakremisha mpaka leo anakremisha
 
Back
Top Bottom