Upotevu wa Mafuta bandarini: Mtendaji Mkuu WMA, Meneja Vipimo wasimamishwa kupisha uchunguzi

Muhongo anahusikaje hapo!!??? Wewe unajua Wakala wa Vipimo Nchini iko chini ya Wizara gani!!??? Au unakurupuka tu, naona MUHONGO amewakalia pabaya sana.

Hapa siyo sehemu ya kampeni za uchaguzi wala UKAWA vs CCM. Kama kweli Muhongo ndiye aliyepeleka SMS kama huyo mkuu wa vipimo alivyosema, basi anastahili kuachana na serikali. Hana maana, hana ethics, hana jipya la kutueleza.

Ifikie wakati tukubali kwamba hata baba yako akiwa mpuuzi, unaweza ukasimulia upuuzi wake.
 
Hebu kasome gazeti la Jamhuri lililofichua hilo suala uone kuwa agizo la kutokutumia mita lilitoka mwaka 2011 na Muhongo aliteuliwa kuwa Waziri mwaka 2012. Na aliliona hilo suala ikiwemo la mazingaombwe ya TIPER, akaanzisha mchakato wa kununua hisa 50% za TIPER ili imilikiwe na Serikali kwa 100%. Walipoanza mchakato wa kuandaa mkataba wa makabidhiano, agizo likatoka "ngazi ya juu" kuwa suala hilo liachwe kama lilivyo. Google Gazeti la Jamhuri usome, taarifa nzima.

Kwa upande wangu muhimu siyo historia ya mita. Tatizo ni hiyo juzi. Kwa nini alipeleka sms kwa mkuu wa vipimo afungulie mita? Kwa nini ktk miaka yote ya uwaziri wake hakuwahi kutoa msg kama hiyo?

Yes, tatizo alilikuta lakini naamini kwa kiasi fulani alilibeba, likawa ni sehemu ya maisha yake. Manufaa yaliyoanzishwa na wengine yakawa ni manufaa yake pia. Hata kama niya yake na TIPER ilikuwa nzuri, kwa hali hii ya juzi inaonyesha wazi kwamba alifahamu wizi na hakuuzuia kwa manufaa yake.
 
Well said mkuu, Prof anapigwa vita kila sehemu - sijui kwa nini baadhi ya members hawapo makini ku analyse mambo - hivi mtu mweledi kama Prof.Muhongo anaweza kweli kumtumia njia za kihuni kufikisha ujumbe wa kiofisi? Si hilo tu anawezaje kutoa amri kwa mtu ambaye hayupo chini ya Wizara yake!!!

Sijui kwa nini watu hawakumsikiliza kwa umakini Waziri mkuu, alimwambia CEO wa VIPIMO kwamba anawezaje kufanyia kazi amri aliyo pata kupitia msg, in other words mtu yeyote mwenye ujuzi wa kutosha katika masuala ya masasiliano anaweza kufanya lolote lenye lengo la kumdhalilisha Prof, who knows labda ni mwendelezo wa vita vya vitalu vya gesi vimehamia Idara ya Vipimo kwa CEO Chuwa.

Mh.Majaliwa ni binadamu makini sana na hakurupuki katika utekelezaji wa wajibu wake, sijawahi kushudia akivamia sehemu akatoka kapa - anafanya homework ya nguvu kabla ya kutekeleza jambo, jamaa huyu namkubali sana upelelezi wake siwa kawaida hata kidogo - atafanikiwa sana.

This is another nonsense! Kwani huyo mama ni mara ya kwanza kuwasiliana na Muhongo? simu ya Muhongo anaifahamu. Technicalities za msg bandia au la hilo ni jambo jingine ambalo kwa sasa hatulihitaji. Linapoteza muda. Muhongo siyo golden goose!
 
Baada ya suala kufika chini ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali na kuagiza waje wataalamu kupima mita hizo, walifika na wakazifanyia tathmini na wakasema mita zinafanya vzr. Lkn huyo mama akadai kuwa hicho bado si kigezo cha kuruhusu mafuta yapite kwenye mita. Kuna nini hapo nyuma ya pazia!! Watu wanajadili hili kwa mihemko tu, wengi wapo less informed hata taarifa toka kwenye gazeti lililofichua hayo hawajasoma.

Mkuu tatizo hapa baadhi yetu tunatanguliza ushabeki wa itikadi za vyama tunasahau kabisa Uzalendo!!

Kitu cha kujiuliza kwanza, huyu Chuwa jeuri ya kukataa kutekeleza mapendekezo ya wataalamu wa tume ya Bunge - jeuri hiyo alikuwa anaitoa wapi?

Mimi kinacho nisikitisha zaidi ni kwamba Chuwa aligharimiwa na Serikali yetu kusomea masuala ya vipimo, ni mtaalamu hivyo anafahamu sana umuhimu wa flowmeter kufungwa pale ili zibaini kiwango/ujazo sahihi wa mafuta yanayo pita kwenye mabomba kwenda kwenye matanki ya kuhifadhia bidhaa hizo, anajua vile vile umuhimu kufanyia flowmeters calibration ya mara kwa mara ili zisiwapunje au kuzidisha kiwango, mambo hayo yote Chuwa kayasomea, leo hii anazuga Serikali eti flowmeters zilikuwa hazisomi vizuri kiwango cha mafuta yanayo pita kwenye mabomba ndio maana alihamua kuzi-bypass, hii inaingia akili kweli - mtu msomi anaturudisha tena kwenye karne ya stone age ya kutumia dipstick kama laypeople!! Swali ni:Je hii ilikuwa ni bahati mbaya au it was a well calculated move ukiwekea maanani Serikali kukataliwa kumiliki TIPER by 100% at the sane time.
 
How do you n


How do you mean "TCRA Officer"? Messaging technology may sound Greek 2 you, lakini kwa watu weledi ni plain sailing - don't U 4get that.

Nimekuhoji swali dogo na hapa narudia: We kwa mawazo yako unafikiri kwa nini Waziri Mkuu Mh.Majaliwa hakuwekea maanani madai ya CEO wa vipimo? Anajua ni rahisi sana ku manipulate teknolojia ya kigitali inayo tegemea zaidi message switching katika kusafirisha ujumbe na mara nyingi hausafirishwi in a real time unlike circuit switching inayo tumika kwenye voice.
Wewe ndo unasema PM hajawekea maanani,wewe na yeye hajasema hajawekea maanani mdau,yule mama why amtaje huyio na si mwingine???
 
Mkuu mimi sijui ujuzi wako ni wa kiwango gani katika masuala ya kiufundi unaohusu nyaja za mawasiliano (voice na sms).

We unafikiri kwa nini Waziri Mkuu hakuwekea maanani madai ya CEO kuhusu SMS anayo dai alitumiwa na Waziri ambaye Wizara yake haipo chini yake.
Yaani PM Amemuuliza serikal inafanya kaz kwa meseji?ww unasema hakuwekea maanani?na mtu amemtaja unasema hakuwekea maanani,labda ulitaka afanyeje ujue anamaanisha?
 
Si
Mkuu, kwani Muhongo alikuwepo bandarini kwa miaka yote 5 wakati hujuma zinafanyika?

Labda useme Mwakyembe ambae alianza kushughulikia hili la mabomba na sifahamu aliishia wapi.
Umesahau kuwa alikimbizwa mara moja kwenda wizara ya ushirikiano wa afrika mashariki kwa sababu ya kuhatarisha maslahi ya mkwere?
 
This is another nonsense! Kwani huyo mama ni mara ya kwanza kuwasiliana na Muhongo? simu ya Muhongo anaifahamu. Technicalities za msg bandia au la hilo ni jambo jingine ambalo kwa sasa hatulihitaji. Linapoteza muda. Muhongo siyo golden goose!

Mkuu nimefafanua ilivyo rahisi ku manipulate sms kama ana ujuzi wa kutosha na sehemu conducive ya kutekeleza njama hizo - sasa mambo ya kusema Muhongo sio golden goose ua goose anaye totoa golden egg yanaingia ingiaje hapa. Kama una issues na Muhongo as a person - we sema.
 
Yaani PM Amemuuliza serikal inafanya kaz kwa meseji?ww unasema hakuwekea maanani?na mtu amemtaja unasema hakuwekea maanani,labda ulitaka afanyeje ujue anamaanisha?

Mimi nimezungumzia kiufundi zaidi, Mh.Majaliwa ni mtu makini sana wala husijidanganye kwamba kwa mbinu zake za kipelelezi hukujua in advance kuhusu SMS mnayo komalia hapa, hivyo so rahisi Waziri mkuu kuwa swayed na SMS zinazo weza kuchezewa na wataalamu.
 
Hii sijaelewa
SMS imetoa order machine zifunguliwe ASAP

Meseji ilikuwa hivi na taasisi zote zilizotajwa kwenye hiyo meseji walitumiana kuweka msisitizo.
wa kutekeleza agizo.


"ACTING MD TPA - MATUMIZI YA FLOW METER: Wizi wa mafuta umekidhiri huku matumizi ya flow meter hayapo hapo Bandarini. Ipo flow meter ya zamani nashauri ianze kutumika kuanzia kesho, Jumatano, 10 Feb 2016. TPA ndiye Mhusika Mkuu kwenye hili suala. TRA na Weights and Measures watoe ushirikiano mzuri. PBPA (Wizara ya Nishati na Madini) ifuatilie kwa makini. KASI INAHITAJIKA KUEPUKA WIZI WA MAFUTA.
S. Muhongo"
 
Mkuu nimefafanua ilivyo rahisi ku manipulate sms kama ana ujuzi wa kutosha na sehemu conducive ya kutekeleza njama hizo - sasa mambo ya kusema Muhongo sio golden goose ua goose anaye totoa golden egg yanaingia ingiaje hapa. Kama una issues na Muhongo as a person - we sema.

Mkubwa, Tusihangaike kumtetea mtu ambaye hatujui wema wake. Kwa wakati huu ambao ametajwa na afisa mwenzake wa serikali, mbele ya PM tuamini alihusika. PM alimuomba aweke maelezo yote hayo ktk maandishi na amtaje huyo mtu above, aliyempa sms. Sasa kwa nini tuseme hakuhusika?

Muhongo alikuwa waziri tangu kipindi cha bwana kicheko.com. Alilifahamu hili. Kama aliongopa nguvu ya kifisadi ya awamu iliyopita, kwa nini tangu apewe tena uwaziri alishindwa kuliondoa hadi asubiri ziara ya PM?
 
Hii sijaelewa


Meseji ilikuwa hivi na taasisi zote zilizotajwa kwenye hiyo meseji walitumiana kuweka msisitizo.
wa kutekeleza agizo.


"ACTING MD TPA - MATUMIZI YA FLOW METER: Wizi wa mafuta umekidhiri huku matumizi ya flow meter hayapo hapo Bandarini. Ipo flow meter ya zamani nashauri ianze kutumika kuanzia kesho, Jumatano, 10 Feb 2016. TPA ndiye Mhusika Mkuu kwenye hili suala. TRA na Weights and Measures watoe ushirikiano mzuri. PBPA (Wizara ya Nishati na Madini) ifuatilie kwa makini. KASI INAHITAJIKA KUEPUKA WIZI WA MAFUTA.
S. Muhongo"

Mkuu VunjaMfupa ule uzi wako ulioweka mawasiliano kati ya maafisa wa Bandari na TRA , upo wangu ? Nautafuta .
 
Uliyosema ni sahihi kabisa lakini wahusika wa moja kwa moja ni Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na agency yao ya WMA. Hawa WMA ni watalaamu wa masuala ya vipimo na ndio maana wapo pale na wapo kila pahala panapohusika na upimaji! Ni hawa WMA ndio walitoa agizo kwa TPA kuacha kutumia flow-meters. Swali linalofuata ni ikiwa agizo hilo lilikuwa ni kwa maslahi ya umma au hapana!

Sioni connection ya wizara ya nishati katika hili! Leo hii WMA wanaweza kutoa agizo na kutekelezwa kwamba vipimo vinavyotumika kwenye mabucha havipo sahihi kwahiyo kuanzia sasa vitatumika Vipimo X. Baadae ikionekana Vipimo X hivi vina walakini sidhani kama itakuwa ni suala la Wizara ya Mifugo!! Wizara ya Mifugo sio watalaamu wa vipimo bali WMA ambayo ni taasisi ya serikali ndio wenye wajibu huo! Baadhi ya maagizo haya kama sio yote yanakuwa approved na Waziri wa Viwanda na Biashara!

Kama isingekuwa mita zenyewe nazo ni magumashi basi nadhani hata TPA wasingekuwa na hatia manake nao pia sio wataalamu wa vipimo! Wakiambiwa vipimo vyenu fake and alternatively tumieni option X nao watafuata manake agizo linatoka kwenye taasisi ya serikali ambao ndio hasa wataalamu wa masuala ya vipimo. Hata hivyo, TPA hawawezi kukwepa kwavile chanzo cha yote haya ni wao wenyewe ambao walinunua mita magumashi. Hii habari back then ili-trend sana na ilionekana kwamba, si tu kwamba mita zilikuwa magumashi (zilifanya kazi chini ya mwaka mmoja kabla hazijaanza magumashi) lakini hata taratibu za manunuzi zilikiukwa!
Baada ya uchunguzi hili ndio litakuwa JIBU. Kama Serikali ya Mh. Maghufuli inazingatia Haki. Na imani yangu Rais ni mkweli.TUSUBIRI.
 
Waziri mkuu kakubaliana na alichoaagiza Muhongo kwenye SMS.Muhongo aliagiza kuwa hizo mita zianze kufanya kazi ndani ya masaa 24.Waziri mkuu kaseme ziendelee hizo hizo mita kufanya kazi.Unataka aadhibiwe kwa lipi kwa kuagiza mita zifanye kazi au nini.

Katika sakata zima issue kubwa ilikuwa mita zifanye kazi.Siyo agizo la mita zifanye kazi limetolewaje.Kama limetolewa kwa SMS likaleta matokeo mazuri tatizo liko wapi.

UKAWA mlipenda waziri mkuu afike pale halafu museme magazeti yaliandika na Muhongo hakufanya chochote.Tunawajua UKAWA toka mchemke wakati ule WA issue ya LOWASA uwezo wenu wa kuaminika na kusikilizika haupo tena.
Hembu achana na siasa hem tuambie huyo muhongo kwann alikishe ishu kwa mama huku akijua kesho yake PM anatia timu pale... Najua we ni mnazi wa kutete utumbo ila hem jibadili ufikiri kwa kichwa ukiwa na akili timamu then utaelewa ninachosema hapa.
 
Labda nikuulize na wewe mwenye dhamana ya diesel,petrol na kerosine ni nani?Aliyeandika meseji ya kuorder hizo machine zifunguliwe nani??Na kwanini amuanidkie SMS badala ya kwenda mwenyewe au kuandika proper official letter??

Hivi hauoni kuna kitu kimefichwa mahali??Penda kujiuliza,Sipendi kuamini kila kitu kinachofanywa na wanasiasa.

Watendaji wetu wamekuwa wapuuzi kweli kweli,Wanasiasa wakikohoa wanashindwa kuwaambia ukweli.Wasomi wetu hawana tofauti na asiyeend ashule kabisa
Hapana mkuu naona unachambua mambo vizuri ila kwa kusema wasomi wetu ni wabovu unakosea sana.
Sijui unafanya kazi wap ila ukweli ni kuwa tz tuna mfumo mbovu sana wa kusimamia mambo, kinachosababisha yote haya ni pale tulipoacha azimio la Arusha na sasa tunaongozwa kimzimumzim hali inayofanya watu kupiga pesa mnoo..
Sasa labda nikwambie kwann watendaji sio wa kulaumiwa.. Kiutaratibu serikalini kazi huwa zinafanywa kwa maagizo top to bottom.. Ni vigumu sana kutekeleza jambo bottom Up
Hivyo ni wazi kabisa hawa watendaji hubaaki kuambiwa fanya hv na usifanye hivi na ukijidai kupingana na maagizo hayo jua utawekwa pembeni na kuambulia kushushwa cheo au kupelekwa kantalamba kabsa upotelee huko..
WANACHOKIFANYA HAWA WATENDAJI NI KUTII AMRI ZA WAKUBWA WAO ZIWE NI MBAYA AU NZURI HAWANA JINSI MAANA NDIO WANAPOPATIA MKATE WA KILA SIKU.. hata ingekuwa ni wewe Tetty ktk mfumo huu ambao kila mtu ni mpigaji na hakuna kuchukuliwa hatua kwa ufisafi... usipopiga unaambulia kufa njaa wakati wenzako wanachanua kirahisi..
Kwa ufupi hakuna uwajibishwaji katika mfumo wa serikalink kwa kipindi kirefu.
Sasa kama huo mfumo wa uwajibishwaji umeeanza basi asiangaliwe mtendaji wala mwanasiasa aliyeteuliwa wote washtakiwe na sio kuwaonea watendaji tu.
 
Inategemea na unavyoiona.Kwa Tanzania yangu ni bora uwe hujaenda shule kuliko hawa walioenda mpaka wakamaliza madarasa yote.Wasomi wetu ndiyo wanaoliumiza TAIFA letu.
Inaonekana una ufahamu mdogo sana kuhusu hii nchi.. Na hasa utaratibu wa kazi serikalini.
Kama hujui tatizo sio watendaji bali wanasiasa ndo wanaiharibu hii nchi..
 
Jipu hili ni la muda mrefu! Lakini kwa vile tulikuwa na Raisi Mtalii-majipu yaliendelea kukua na yako mengi.



Ripoti ya Jumla ya Mashirika ya Umma 2013/2014
PAU-SWAHILI.pdf


Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali

Ripoti ya Mashirika ya Umma 2013/2014



3.6 Mapendekezo ambayo hayajatekelezwa kwa mwaka 2012/2013



3.6.2

Mita za Kupima Mafuta Zilizotelekezwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania Mamlaka ya Bandari Tanzania ilinunua mita nane kwa ajili ya kudhibiti upimaji wa shehena za mafuta yanayoingia nchini. Mita hizo ziliwekwa tayari kwa matumizi kwenye bandari za Tanga na Dar es Salaam kwa ajili ya kusaidia kudhibiti mapato yanayopotea kutokana na kutokuwa na vifaa vizuri vya kupimia shehena za mafuta zinazoingia nchini.

Vifaa hivyo vilinunuliwa na kuwekwa kwenye bandari hizo baada ya serikali kuagiza ununuzi wake kwa ajili ya kupata vipimo sahihi na hatimaye kutoza viwango sahihi vya kodi. Hata hivyo, mita hizo zimetelekezwa kwa miaka kadhaa sasa. Sababu iliyotolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa vipimo ni kwamba vifaa hivyo havikidhi viwango vinavyotakiwa. Baada ya matatizo hayo kushindikana, Mamlaka ikaamua kuendelea kutumia njia zisizo za kielektroniki (“deep stick”)fimbo ya kutumbukiza kwenye matangi ya mafuta) kwenye kupima shehena za mafuta yanayoingia nchini.
 
Back
Top Bottom