nyumba kubwa
JF-Expert Member
- Oct 8, 2010
- 10,309
- 8,370
Ila nikimsikiliza huyu mama ...(unless awe anasema uongo) kuna possibility ya kuwa innocent...
Na hii incidence nadhani iwa alert waheshimiwa wasipende sana kuvamia maofisi wakiwa na wana habari...wataja umbuka siku moja wakikutana na mtendaji hamnazo...
Prof ametajwa na kila mtu ametafsiri kutajwa kwake anavyotaka yeye...
Bila ma camera aibu hii isingetokea...
Na hii incidence nadhani iwa alert waheshimiwa wasipende sana kuvamia maofisi wakiwa na wana habari...wataja umbuka siku moja wakikutana na mtendaji hamnazo...
Prof ametajwa na kila mtu ametafsiri kutajwa kwake anavyotaka yeye...
Bila ma camera aibu hii isingetokea...
Jipu hili ni la muda mrefu! Lakini kwa vile tulikuwa na Raisi Mtalii-majipu yaliendelea kukua na yako mengi.
Ripoti ya Jumla ya Mashirika ya Umma 2013/2014
PAU-SWAHILI.pdf
Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
Ripoti ya Mashirika ya Umma 2013/2014
3.6 Mapendekezo ambayo hayajatekelezwa kwa mwaka 2012/2013
3.6.2
Mita za Kupima Mafuta Zilizotelekezwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania Mamlaka ya Bandari Tanzania ilinunua mita nane kwa ajili ya kudhibiti upimaji wa shehena za mafuta yanayoingia nchini. Mita hizo ziliwekwa tayari kwa matumizi kwenye bandari za Tanga na Dar es Salaam kwa ajili ya kusaidia kudhibiti mapato yanayopotea kutokana na kutokuwa na vifaa vizuri vya kupimia shehena za mafuta zinazoingia nchini.
Vifaa hivyo vilinunuliwa na kuwekwa kwenye bandari hizo baada ya serikali kuagiza ununuzi wake kwa ajili ya kupata vipimo sahihi na hatimaye kutoza viwango sahihi vya kodi. Hata hivyo, mita hizo zimetelekezwa kwa miaka kadhaa sasa. Sababu iliyotolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa vipimo ni kwamba vifaa hivyo havikidhi viwango vinavyotakiwa. Baada ya matatizo hayo kushindikana, Mamlaka ikaamua kuendelea kutumia njia zisizo za kielektroniki (“deep stick”)fimbo ya kutumbukiza kwenye matangi ya mafuta) kwenye kupima shehena za mafuta yanayoingia nchini.