Upinzani unakufa kila kona ya Tanzania - NAPE

Alikuwa anamaanisha upinzani unakua kwa kasi kila kona ya nchi hii. Ni bahati mbaya kwamba mdomo wake hauna mawasiliano mazuri na ubongo wake. Anachowaza sio anachokisema. Anayo matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa kwa hiyo isengekuwa rahisi aseme hivyo. Hayuko sawa kichwani!
Kuna watu mpo jf kuongeza siku ZA watu,
Kiukweli umenifurahisha!!
Hamna akili mle!!
 
Niliwahi kuwakuta vijana wa bavicha siku moja wakijadili jambo kuhusu wewe, na baadhi yao wakasema kuwa wewe ni jembe lao katika kujenga hoja jf na hivyo unafaa kuwa kiongozi wao mkubwa ndani ya bavicha..

Samahani kidogo ndugu yangu..,hizo hapo juu ndio hoja zenyewe ambazo ndizo zilikuwa mtaji wako wa kisiasa wakati wa uchaguzi...??

Mchalo wako sio mtamu ndio maana umenyimwa ukuu wa wilaya. Namba utaisoma tu.
 
Hivi maccm mnasubiri nini kumtoa Nape kwenye nafasi aliyopo!?

Huu ni zaidi ya ujuha aise.Yaani useme Upinzani unakufa wakati TAMISEMI mmeburuzwa mpaka basi.
Bado maccm yanashangilia huu upuuzi,ama kweli sikio la kufa.........
Nadhani akili yako bado haijawa sawa, Serikali za mitaa CCM imeshinda nchi nzima kwa asilimia 85 na bado mnasema mmetuburuza...,kweli ukichaa sio lazima uokote makopo.
 
Mchalo wako sio mtamu ndio maana umenyimwa ukuu wa wilaya. Namba utaisoma tu.

Kila nikiwatazama vijana wa chadema naiona hofu kubwa katika mioyo yao, lakini baya zaidi nauona umbumbumbu mkubwa vichwani mwao ambao unawaongoza kutukana katika kila jambo.
 
That's politics , whatever you say is right but whatever is said by the opposite side is always lies. Tanzanians are alert and know what should be their choice. May the best man win in October
Umeongea vyema sana ila bahati mbaya umetumia lugha ngeni hawa vilaza wa CDM hawawezi kukuelewa kirahisi...sio mbaya nitawatafsiria.
 
Niliwahi kuwakuta vijana wa bavicha siku moja wakijadili jambo kuhusu wewe, na baadhi yao wakasema kuwa wewe ni jembe lao katika kujenga hoja jf na hivyo unafaa kuwa kiongozi wao mkubwa ndani ya bavicha..

Samahani kidogo ndugu yangu..,hizo hapo juu ndio hoja zenyewe ambazo ndizo zilikuwa mtaji wako wa kisiasa wakati wa uchaguzi...??

mi nakushangaa siasa zimekushinda sasa unaonekana umejaza tu wivu moyoni mwako unapowaona wenzako kina ben na yeriko wakichapa kazi ya kikamanda uliokua unaipenda na ikakufanya ujulikane nchi nzima.du pole sana dada july vipande 34 vya fedha vilikufanya uisaliti safari yako ya matumaini sitosahau siku ulonambia kuwa moyo na damu yako vyote viko chadema ccm ziko nguo zako tu
 
Nadhani akili yako bado haijawa sawa, Serikali za mitaa CCM imeshinda nchi nzima kwa asilimia 85 na bado mnasema mmetuburuza...,kweli ukichaa sio lazima uokote makopo.

kokotoa hesabu zako hapa tujue hiyo asilimia85 umeipataje maana hesabu sio siasa
 
Hivi huyu juliana ambae nafsi zenu zinawauma kila likitajwa jina lake amewafanya nini..?

Hivi kwa mfano, unapotaka kuzungumzia mafanikio ya kisiasa kati ya Ben, Yericko na July nani unamtaja kuwa ni mwenye mafanikio kisiasa..?

Ben ni nani Chadema, ni miongoni mwa rejected.,Yericko ndo kabisa, hana nafasi wala nyadhifa ni mchumia tumbo tu hajulikani hata kwenye kata anayoishi.,Ben na Yericko wanajulikana JF na Facebook, July sio level yao kabisa...

kaulizie hata kwa mtoto wa miaka 7 wa Namanyere anamjua.
 
Inawezekana Nape anasema hivyo kwa vile hajapata matokeo ya Sumbawanga, mwenye matokeo ampatie ili apunguze kubwabwaja.
Thubutu , hataki kabisa kusikia wala kuambia habari Sumbawanga. Mimi nilijaribu kumtonya tulipokutana sehemusehemu akanambia "achia hapo tumedhachukua hatua hukusikia, CHADEMA ni washenzi sana wanachezea sharubu za simba kwa kumdhalilisha Waziri mkuu na mgombea urais wa CCM 2015"
 
Matokeo ya Sumbawanga ameshayapata?. Au vijana wake wa huko wamegoma kumtumia?. Napeeee The VUVUZERA.
 
kokotoa hesabu zako hapa tujue hiyo asilimia85 umeipataje maana hesabu sio siasa

CCM wanajua kwamba UKAWA wamepata more 39.78% ...sasa pale mwanzoni ccm walijaribu kupika data kwa kusema ukawa wameshinda kwa 16%... Wakaona single haiuzi....wakasema 25% wakaona haiuzi...tamisemi ghafla wakageuka wakawa mabubu

Kwa maana ya kulisaidia jukwaa hili tutaweka hapa matokeo ya kila Mkoa ...nini UKAWA wamepata na nini ccm wamepata

Fikirieni tuu mfano mdogo...Dar ambapo upinzani hawakufanya vizuri...lakini wamepata 25.8% mpaka sasa...

Nenda kanda ya ziwa magharibi...mikoa ya Mara...Simiyu....Shinyanga....nenda mikoa ya ziwa Mashariki...Mikoa ya mwanza ..Kagera...Geita.., nenda kanda ya nyanda za juu kusini...Mbeya...Iringa...Rukwa nadhani ni juzijuzi tuu mmesikia ccm wakilia...wakijikataaa

Sasa nenda Kanda ya kaskazini...Manyara...Arusha...Kilimanjaro sasa nisiongee sana marafiki zangu...

Ila la mwisho nawahasa vijana wote wenye uwezo wa kuwa viongozi rudini kule vijijini mkagombee nafasi za kiserikali ...(Udiwani na Ubunge) twendeni tukawashike

Tumefanya vizuri serikali za mitaa kwa kuwa vijana wasomi mmeamua kujitolea maisha yenu...sasa hii ni LALA SALAMA... Kusubiri tena miaka mitano ccm iendelee kuwa madarakani ni janga

Mlioko mijini endeleeni kutoa elimu kwa ndugu zenu walioko vijijini(shangazi..mama zetu...baba...babu na dada zetu) ni kwa kufanya hivyo tuu Ccm itaondoka madarakani

Imebaki miezi 5 sasa hatutaki kusikia eti ccm imeiba kura..twendeni tukaamshe amushe TULIPOZALIWA
 
Nadhani akili yako bado haijawa sawa, Serikali za mitaa CCM imeshinda nchi nzima kwa asilimia 85 na bado mnasema mmetuburuza...,kweli ukichaa sio lazima uokote makopo.

Wewe uko nchi gani? Asilimia 85 za kuambiwa na Nape, futilia matokeo yaliyotolewa na mkurugenzi wa TAMISEMI hivi karibuni. Ukiondoa mapingamizi hata 50% inaweza isifike.
 
"NIMEPATA BAHATI YA KUZINGUKA PAMOJA NA KATIBU MKUU NDUGU ABDULRAHMAN KINANA NCHI NZIMA, NIMESHUHUDIA KWA MACHO YANGU KUWA UPINZANI UNAKUFA KILA KONA YA TANZANIA" - NAPE MOSES NNAUYE, uwanja wa Barafu, Dodoma.

Maneno hayo ni nukuu ya katibu wa halmashauri Kuu, Itikadi na Uenezi wa Chama bora Tanzania CCM alipokuwa akizungumza na maelfu ya wananchi waliojitokeza katika mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana katika Viwanja vya barafu vilivyopo Dodoma mjini, pembezoni mwa uwanja wa mpira wa Jamhuri.

Nape ametoa ushuhuda huo akiwaasa baadhi ya vijana na wananchi wa Dodoma ambao bado wanadanganyika na maneno ya uzushi na uongo wa upinzani ambao wanautunga kila asubuhi, Nape amesema kutunga uongo dhidi ya CCM na Serikali yake ni kutapatapa kwa upinzani ukiwa unakata roho.

Nae Katibu Mkuu katika Mkutano huo wa hadhara, amesema wajibu wa CCM ni kuhakikisha kuwa wananchi wanapata maisha bora, asema miaka ya hivi karibuni watanzania wameshuhudia maendeleo makubwa na kupiga hatua kubwa katika elimu, miundombinu ya barabara, madaraja, teknolojia na nishati.

Kinana amesema ni kazi ngumu kutenda rahisi kubeza, kazi ya CCM kutenda kazi ya upinzani ni kusema. Asema tumefanikiwa katika shule za UPE ambazo zimetoa mabalozi, mawaziri na wakurugenzi wakubwa ingawa wakati zinaanzishwa zilibezwa kama zinavyobezwa shule za Kata lakini zinatoa vijana wanaojiunga na vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini na tutapata wataalamu na wazalendo wa kweli kutoka shule za kata ingawa wapinzani wanazibeza.

Nape na Kinana siku hizi wanatembea na fisi angalau kuwavutia watoto waende kwenye vikao vilivyosusiwa na watanzania waliojitambua
 
Hivi huyu juliana ambae nafsi zenu zinawauma kila likitajwa jina lake amewafanya nini..?

Hivi kwa mfano, unapotaka kuzungumzia mafanikio ya kisiasa kati ya Ben, Yericko na July nani unamtaja kuwa ni mwenye mafanikio kisiasa..?

Ben ni nani Chadema, ni miongoni mwa rejected.,Yericko ndo kabisa, hana nafasi wala nyadhifa ni mchumia tumbo tu hajulikani hata kwenye kata anayoishi.,Ben na Yericko wanajulikana JF na Facebook, July sio level yao kabisa...

kaulizie hata kwa mtoto wa miaka 7 wa Namanyere anamjua.

huyo July ndiyo nani maana nasikia ccm maana nimepitia uzi mwanzo mpaka mwisho sijaona cha maana alichoandika
 
Upinzani unakufa???? Hivi lina akili kweli hili punguani?? Uchaguzi wa serikali za mitaa ilikuwa ni kipimo! Sasa kama anatumia zile miwani zake ambazo nafikiri kwa mtu mmoja yeye zinamuonyesha watu 15, basi atakuwa sahihi.
 
"..MKUBWA.." ndio neno ulilolitumia kumu address Ben..Duh

Wewe ulikuwa miongoni mwa wale makampeni meneja wake ambao mlikuwa mnampamba huyo bwana "MKUBWA"..?

Shonza pole sana dada yetu kwa yaliyo kukuta huko uliko kimbilia kwa ahadi ya kupewa ukuu wa wiliya,leo hii wamekutumia watakavyo na hatimaye wamekutupa kama ganda la miwa.Na ujue hapo bado utarudi kwa kutumia magoti kuja kuwaomba cdm wakusamehe
 
Nadhani akili yako bado haijawa sawa, Serikali za mitaa CCM imeshinda nchi nzima kwa asilimia 85 na bado mnasema mmetuburuza...,kweli ukichaa sio lazima uokote makopo.

hizo takwimu za Redet za kupika ili jamii iwaone mko sawa tumezizoea ,nenda field ndo uone ukweli.tuache propogada za kulipwa vijisent ili kuropoka ,hizo takwimu za 85% si sahihi,ni za kupika upinzani umekuwa.maana hizi takwimu zimekuwa kila mccm akibuka kuzungumzia ushindi wa uchanguzi wa serikalinza mitaa ,anakuwa na takwimu zake.
tujiulize oama ushindi ulikuwa wa haki na sahihi mbona tumeshuhudia watu wanpelekwa kuapishwa huku hawana vyeti vya ushindi na kuishia kupigwa ,mfano mzuri wilaya ya kinondoni.
acha blabla upijzani umekua.na haya makero ya Escrow,kiburi cha hao walioiba ,wakuu wa wilaya wajinga kama Dc wa kahama,ndo ccm inajichibia kaburi kabisa.
 
Back
Top Bottom