Updates kutoka Uwanja wa Mashujaa Mtwara: Mkutano wa Kampeni za mgombea Urais CCM

Muda huu star tv wanarusha mkutano live. Watu wamejaa na nguo zao za ccm halisi na wapiga kura. Twende pamoja..anaongea sasa Lukuvi.
 
Mi nawashangaa wanamuita fisad

Je ufisad uliowah kutokea TANZANIA NI RICHMOND PEKE YAKE?
 
Akitoka hapo atasema yeye mlemavu na kwamba anaomba vurugu zisitokee kwakuwa walemavu wataathirika zaidi huku anachochea vurugu majukwaani. Nadhani angetoka kwenye hichi chma kama kiongozi abaki mwanachama tu ili aendelee na njaa zake.
 
Haina shida....yan watukane matusi yooote yaishe....sisi tupo pale pale....kwa hiyo CCM wameona wamchukue huyo AMON aokoe jahazi? duuuuuuuu!
 
Hizi siasa za kuchafuana zishapitwa na wakati,matusi hayatusaidii sisi wapiga kura,hamjui mnatupa hasira sana,
 
Kampeni za Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dr John Pombe Magufuli zinaendelea katika Mkoa wa Mtwara ambapo ni Mkoa wa Sita tangu alipoanza Kampeni hizo katika Mkoa wa Katavi.

Mkutano huo wa hadhara unaofanyika katika uwanja wa Mashujaa Mtwara unarushwa live na vituo kadhaa vya runinga ikiwemo star TV pamoja na vituo vya redio vya kitaifa na vya mikoani.

Hivi sasa Dr Magufuli anazungumza na hii hapa chini ni update ya hotuba yake...

- Dr Magufuli anawashukuru wanamtwara kwa kujitokeza kwa wingi na kuwaambia kuwa hiyo ni ishara kuwa wanataka mabadiliko na ameomba nafasi ya Urais kwa kuwa na yeye anataka Mabadiliko.

- Nimekuwa Serikalini kwa miaka 20, najua kwenye Serikali wapi pana lega lega na wapi panaihitaji kuangaliwa kwa umakini...naijua Serikali na namna ya uendeshaji wake na ndio maana nimeomba kuiongoza ili niisimamie.

- Anasema anajua matatizo yaliyowakabili watu wa Mtwara wakiwa wanasafiri kwa miezi sita kufika Dar, tatizo hilo amelimaliza na kuwaahidi kuwajengea barabara nyingine ya kwenda Newala mpaka Masasi.

- Ameahidi kuboresha bandari na kupanua uwezo wa bandari hiyo kupakua mizigo ili itoe ajira kwa vijana wa Mtwara na iboreshe maisha ya wanamtwara.

- Anasema Serikali ya awamu ya nne imefanya mambo makubwa katika maandalizi ya kurina gesi...imejenga kiwanda cha Dangote.,Dr Magufuli ameahidi kujenga na kusambaza Viwanda Mtwara yote..

- Anaahidi kuwa ataongeza makusanyo ya Serikali na fedha hiyo itatumika kuwaboreshea maisha Watanzania...amesema Serikali ya Awamu ya nne imeongeza mapato kutoka 300 kufikia bilioni 900, ameahidi kuongeza makusanyo.

- Dr Magufuli anasema atajenga reli kutoka Mtwara mpanga Mbaba Bay Ruvuma kupitia mchuchuma.

- Anazungumzia suala la pembejeo za kilimo na soko la kudumu la zao pa korosho. Anasema lazima wakulima walipwe fedha zao kwa wakati na yawe malipo yenye tija.

- Anawataka wanachama wa upinzani kumuunga mkono kwani ndie Mtu anayeweza kuwaletea maendeleo katika awamu ya tano.

- Kila Mkoa utakuwa na hospitali ya rufaa na kwamba vifaa vya huduma za Afya pamoja na Dawa zitapatikana kwa wingi na kujitosheleza katika sekta ya Afya.
 
Back
Top Bottom