Uozo Ndani ya Polisi: Wanachi wamechoka; Jisomee huu Mkasa

hapa mungu peke yake hatoshi. Cha msingi polisi wajirekebishe vyenginevyo....!

zaidi ya mungu ni nguvu gani tena uhitaji? Mbona waongea bila kufikiria? Kuna kitu unamaanisha kwa msemo wako huo, bila mkono wa mungu unadhani utafanikiwa?
 
Hii hali ndio halisi ambayo serikali ya sisi imeilea na imekua na sasa kuimaliza ni ngumu mpaka ccm yenyewe ife
 
Ukisikia uonevu wa polisi Tanzania basi hii hapa ni ya mwaka! Chama cha CCM inabidi ijipange kuhususiana na watendakazi wake. Raia hawatawavumilia tena. Kesi za uonevu na unyanyasaji zimezidi! . Kuna mshikaji wangu mmoja anaishi huko majuu marekani. Alikuja likizo kumuona mkewe. Wife akawa anaendesha gari maeneo ya Ubungo, ghafla polisi akawasimamisha na kumuomba leseni. Baada ya huyo mama kumpa leseni, huyo polisi hapo hapo akasimamisha madereva wengine watatu. Ghafla alifika dada mwingine, matokeo yake akamsimamisha, na kuingia kwenye gari lake na kuongozona naye akidai wanakwenda kituoni. Hapa ana leseni ya watu wanne. Hao wengine wote wakaambiwa wamfuate kkwenda Ubungo Bus Terminal Police. Walipofika hapo kituoni, polisi mwenyewe hakawa hayupo kumbe lile gari alilopanda alimalizana na dereva wake njiani. Basi wote waliokuwa wakidai leseni zao wakaondoka.

Baada ya kurudi kesho yake, huyo traffic akawa hayupo tena, jamaa na mkewe wakaondoka. Baada ya wiki tena, huyo mama akarudi mtu mzima akarudi kutafuta leseni yake, bahati nzuri akamkuta yule polisi sasa. Akaambiwa atoe laki tatu ili asamehewe Tsh. 300,000. Mama akashtuka aksema hana hela, basi wakamuomba laki na nusu. Mama akakataa, basi hapo hapo. Wale polisi wakaamua kumbambia kesi ya kutanua na kumuingiza mama wa watu Sero na waalifu wengine vibaka, majambazi nk... (hii ni wiki moja baadae, na mama kaja mwenyewe kutafuta leseni yake). Huyu mama alikuwa na $1,900 taslimu siku hiyo alizoachiwa na mumewe kwa ajili ya shuguli zao a kimaendeleo. Basi wakati wa kuzikabidhi hizo hela, akaomba kumjua jina anayekabidhiwa. Kosa kuuliza, akabambikiziwa kesi nyingine ya kashfa dhidi ya polisi na tayari hapa walishagawana hizo $1,900. Mama wa watu, mtu mzima akakaa sero kwa siku nzima bila kosa akiambiwa kesho anapelekwa mahakamani, mtu aliyeondoka nyumbani kwake kuja kuchukua leseni yake aliompa polisi kwenye routine check ya kwaida, matokeo yake kuswekwa ndani.

Bahati yake ikawa kuomba simu yake kuwataarifu ndugu zake kuhusu mkasa uliomkuta. Baada ya kumpigia mumewe, bahati nzuri mume ana ukaribu na Kamanda Kova. Mume akampigia Kova, naye Kova kampigia mkuu wa trafiki wa mkoa haraka haraka kuzima hii kashfa. Sasa kumbe shemeji yake huyu dada ni mtu mkubwa sana TAKUKURU. Shemeji mtu wa TAKUKURU akaenda moja kwa moja hadi Ubungo Terminal Police Station. Polisi wakawa hawajui nani kaja pale wakaanza kumchimba mkwara, kumbe wanachimbia bosi mkubwa sana wa taukururu. huyu bosi wa TAKUKURU na ile tabia ya kulindana na wakuu wa polisi, naye pia kazima hii skendo kutokana na ombi la mkuu wa trafiki..... Mimi niliposimuliwa nikabaki mdomo wazi. Ikiwa watu wakubwa wanafanyiwa hivi watu wa kawaida je? Mimi na wewe tukikamatwa itakuwaje? kwa maana hawa polisi walipoona mambo yamekuwa magumu, wakaanza kumfukuza huyo mama aondoke hapo kituoni haraka sana.... yaani basi tu. Ila najiuliza maswali machache

-Mtu anakuja kudai haki yake, anakamatwa na kuwekwa sero na wahalifu sugu kama majambazi na wauaji?
-Rushwa inakuwa ya kulazimisha, wakuu wanataarifiwa lakini hawachukui hatua, nchi inaelekea wapi?
-Wakuu wao wanataarifiwa kuhusu uhuni kama huu alafu wanazima skendo, bila ya kuwawajibisha hawa polisi wasio na nidhamu? Kova kaletewa kesi kama hii, Polisi wa Ubungo Terminal kufanya uchafu kama huu, alichukua hatua gani dhidi ya hawa vibaka ndani ya jeshi lake, au kuuzima kwa kumuachia huyo mama ndio mambo kwisha, na hela zake je??

C.C.M inafanya nini dhidi ya hawa watendaji wake, has apolisi wasio na nidhamu? Kamanda Lema kayazungumzia haya majuzi Bungeni lakini tunaona wanamagmba hawasikii. Hatutakubali uonevu kama huu, mrudishieni huyu mama hela zake. $1,900 ni nyingi sana kumnyang'angya mtu

IGP Mwema,
Cmdr. Kova,
Fuatilieni huu mkasa na kuwawajibisha hawa polisi wa Ubungo Terminal kabla haujaingia kwenye media. Hii ni skendo kubwa

Mkuu, hili si suala la kusubiria kupeleka kwenye media. Lipelekwe haraka sana. Naona ushahidi wote uko kamili! Hawa watu WAMEIBA, ni WAHALIFU! Kwa nini wanavumiliwa? Iko siku tutaanza kutembea na mapanga, wakitusimamisha, tukiona tunaonewa tunachomoa na tunawakata mikono yao! Tamaa zao zisitusababishie maumivu na hasara zisizo na msingi! Namwonea huruma huyo mama. Inakuwaje hao nduguze wa TAKUKURU na kwingineko wakashindwa kumsaidia kupata pesa zake?
 
He! Mkasa huo mbona cha mtoto,c bora huyo mama anakaa mjini,watu kama kova na huyo bw wa takukuru wanapata hata taarifa...chukua huu mkasa nilioukuta mkoani morogoro,wilaya ya ulanga,tarafa ya malinyi,kijiji cha biro...kuna bw m1,msukuma kwa kabila,alifiwa na mtoto wake wa umri wa miaka 2, (niseme tu kwanza hawa wasukuma wanaogopa polisi kuliko simba) kwa mujibu wa mtoa habari wangu kifo cha mtoto huyo kilisababishwa na ugonjwa wa kuharisha na kutapika. Na ukichukulia hawa mabwana wanaishi mbali mashambani. Kuna polisi m1 akasikia jamaa kafiwa akaenda kwa yule mfiwa na kumtetemesha kwa kumwambia yeye ndo kasababisha kifo cha yuke mtoto kwa uzembe wa kutompeleka mwanae haspitali,...basi,akamtaka jamaa ampatie Tsh milioni 2 la sivyo atamfungulia kesi ya mauaji. Msukuma wa watu akapiga hesabu akaomba apewe wiki 1,akauza mazao yake na ng'ombe akampatia polisi yule mshenzi tsh 2ml akatokomea zake. Mtoa habari wangu anadai hata OSS hajui hiyo deal. Imagine ndo wewe mwanao amekufa wanakuja wahuni wanakuchukulia na pesa ...matukio ni mengi!
...Huyo Pollisi alishaona huyo msukuma ni mbwiga ndio maana akamtoa 2ml kwa kifo cha mtoto wake. Hawezi kufanya hivy hata siku moja kwa wajanja atakapewa kata funuwa apotee!!!
 
Kwa upande wangu naweza kusema police tanzania (PT) Ni sawa na waasi kama vile LRA, PARE PAREPE UTU na N.K wanafanya uhalifu wa kivita wanapiga watu,wanaua watu ,wanadhulumu,wanapora mali za wananchi na hakuna wakukutetea kuna jamaa yangu alikamatwa na kupelekwa mabatini kjnyama kituoni pale wale askari walimpora dola mia 5 alizo kuwa nazo kwenye walet ,wakamuweka celo siku 4, dhamana alikataliwa na mawasiliano yali zuiliwa mkuu wa kituo alipo ambiwa akawabana hao askari na kugawana pamoja hizo hela za wizi kutoka kwa mtu ambaye baadae ilionekana hana hatia na huo ndio ulikuwa msaada kutoka kwa kiongozi wa kituo mhaya, huu ni muendelezo wa machungu ya topic hii na ni mifano michache tu ya uozo ndani ya geshi la police,namkumbuka hayati chacha wangwe ambaye alikwisha wahi ku7ema kuwa gesh la police na mgambo wa jiji kuwa ni majambazi walio pelekwa mafunzo na selikari na kupewa sheria halali na silaha ili kuuwa wananchi na kupora mali zao na hivyo basi kupendekeza kuwa mageshi haya ya polce na mgambo wa jiji yafutwe kwani yamekuwa keroo....Ovaa
 
Yaani nimesoma baadhi ya post hadi machozi yananidondoka, kiukweli polisi ni washenzi sana. Ni kama chuoni kwao wanafundishwa unyanganyi badala ya usalama wa raia. Kuna siku nilikuwa natoka Arusha naelekea Tanga, kabla hatujafika Mombo nikaona polisi wamenipiga mkono. Kwa kuwa nilikuwa kasi sana ilibidi nikasimame mbali kidogo, yaani kufumba na kufumbua nilivamiwa na jopo la maafande na kuombwa leseni. Nikatoa class C, nikaulizwa unajua makosa nikawaambi sijui. Nikaambiwa mwendo kasi. Nami nikawaambia ninaharaka. Nikaulizwa, yaani eneo hili tu ndiyo litakuchelewesha. Nami nikawajibu kuendelea kunihoji ni kunipotezea muda. Wakaniambia unajiamini nini wewe, sina zaidi ya ukweli wangu. Baada ya malumbano makali wakaniuliza unafanya kazi wapi, sifanyi kazi yoyote. Kulikuwa na mkuu wao mmoja pale akasema hebu mwache aende zake maana mijitu kama hii haieleweki. Wito, polisi wa nchi hii ni very corrupt hivyo inabidi kujizatiti sana pindi inapohojiana nao. Huwa wana tendency ya kuogopa watu wenye asili ya kujua mambo.
 
Niliwahi kusema hapa jamvini, jeshi la sasa la Polisi lahitaji kuvunjwa na liundwe upyaa bila kuchukua tena mijipolisi ya sasa.
Kulivunja Jeshi la Polisi lote na kuliunda upya ni mchakato na gharama, mimi nina hakika kuwa ENDAPO POLISI WANAOFANYA MAKOSA WANGEKUWA WANAADHIBIWA KWA MUJIBU WA SHERIA ZA JESHI LAO, nadhani tabia hii ya uonevu ingepungua. Hata ukisoma post ya mtoa mada Kova kapata taarifa lakini hajachukua hatua zaidi ya kumtoa mhusika na kumuacha polisi aliyemuonea bila adhabu yoyote. Hii inonyesha kuna mtandao ndani ya Jeshi la Polisi ambao hata wakubwa wanajua na ndiyo maana wanashindwa kuchukua hatua madhubuti.
 
Nakuja na tz sasa ,coz in nigeria when someone talk about Boko haram ,those who call themselves police officer, they know how it sound.owke
 
Hiyo ishu ya huyo mama kama ni kweli inasikitisha sana.
Jambo la kwanza ambalo ningependa kujua huyo mama alipoenda polisi alisindikizwa na mtu yoyote?manake mimi nawaelezaga watu sana wanaosema wanaenda polisi kufuatilia issue yoyote lazima at least asindikizwe na mtu,hii itasaidia angalao kuweza kupata ushaidi,manake kama alikuwa mwenyewe ni ngumu sana kuproof kama kweli alikua na hizo hela na akanyanganywa.
Suala la pili huyo mama aliweza angalao kuchukua namba ya huyo askari?au kama anaweza kumkumbuka sura,hii itasaidia katika kumuidentify.
Sasa swala ambalo naliona hapa kama huyu mama anaweza kuproof kwa hayo ambayo nimeyanena hapo juu,nashauri aende akaonane na wanasheria na kufungua kesi mahakamani moja kwa moja ya unyanganyi na unyanyasaji atapata nafasi ya kuidentify wezi waliomwibia na jibu litapatikana.Halafu siku hizi kunavyama vingi vya kuwatetea wakina mama na watoto mawazo ya kisheria na vingine vinatoa msaada wa moja kwa moja,jaribu kwenda huko pia watakupa mawazo Badala ya kukimbilia wakubwa mbalimbali wa nchi na ndugu wenye title kubwa.Huo ni ushauri wangu.
 
Hiyo ishu ya huyo mama kama ni kweli inasikitisha sana.
Jambo la kwanza ambalo ningependa kujua huyo mama alipoenda polisi alisindikizwa na mtu yoyote?manake mimi nawaelezaga watu sana wanaosema wanaenda polisi kufuatilia issue yoyote lazima at least asindikizwe na mtu,hii itasaidia angalao kuweza kupata ushaidi,manake kama alikuwa mwenyewe ni ngumu sana kuproof kama kweli alikua na hizo hela na akanyanganywa.
Suala la pili huyo mama aliweza angalao kuchukua namba ya huyo askari?au kama anaweza kumkumbuka sura,hii itasaidia katika kumuidentify.
Sasa swala ambalo naliona hapa kama huyu mama anaweza kuproof kwa hayo ambayo nimeyanena hapo juu,nashauri aende akaonane na wanasheria na kufungua kesi mahakamani moja kwa moja ya unyanganyi na unyanyasaji atapata nafasi ya kuidentify wezi waliomwibia na jibu litapatikana.Halafu siku hizi kunavyama vingi vya kuwatetea wakina mama na watoto mawazo ya kisheria na vingine vinatoa msaada wa moja kwa moja,jaribu kwenda huko pia watakupa mawazo Badala ya kukimbilia wakubwa mbalimbali wa nchi na ndugu wenye title kubwa.Huo ni ushauri wangu.

haya ndo yale ya Arusha. Hawa watu itabidi wakimbie nchi
 
Nampa mama pole: kituo cha ubungo kimezidi uchafu ila kinahitaji watu majasiri ili kulimaliza tatizo hili ngoja dawa inachemka.

Ukienda kituo cha police ostabei utaona askari wanakaa nje ya kituo wanasubiri watu ukitokea tu wanaanza kukuzonga kama wapigadebe kila mtu anataka umwambie shida yako ili akusaidie. Ukimweleza anakupa gharama:
1:kufungua kesi ikae vizuri 20000
2:kumfuata muhalifu 30000
3: kuongea na mkubwa badala yako ili mshitakiwa afutiwe dhamana 60000
4: kumuweka mtu ndani zaidi ya siku tatu 150000.
5: Ukiwa umenatafutwa na police ukitaka wasikukamate 500000

Sasa kweli nani ataweza kupata haki?

Viongozi wa police mpo humu mimisikumoja ubungo waling'oa number plate za gari alfajiri nilikuwa nasafiri. Wakadai niwape 50000 ili wanirudishie plate no zangu kosa nimepaki vibaya sasa kama nimepaki vibaya mbona gari moja tu ndio mchukue no katikati ya magari mengi yaliyopaki??

Wanyonge wa tanzania hawana haki kabisa tena wanyonge ninamaanisha masikini.

Enyi sisi em hamlioni hili.

Kifupi swala la polisi halihitaji siasa ni maamuzi au jeshi lifutwe kama bunge lilivyopambana na mahita enzi zile za posho ya wabunge????
 
Kulalamika kwenye mtandao haitawasaidia walioathirika wala wanaosababisha madhara mnayoyachangia. Jeshi la polisi halijaharibika kiasi hicho, bt ni kweli baadhi ya askari wanaliharibu jeshi. Ushauri,

1. Mwenye ushahidi apeleke malalamiko kwenye kitengo maalum cha kushughulikia malalamiko pale makao makuu ya polisi. Or

2. Peleka malalamiko yako kwenye kurugenzi maalum ya kupokea malalaniko pale wizara ya mambo ya ndani ya nchi inayoongozwa na Mkurugenzi wake Mr. Shiyo. Or

3. Peleka malalamiko moja kwa moja kwa Mkurugenzi wa Upelelezi makao makuu ya polisi.

Sitegemei kwamba options zote hizo zitakalia malalamiko yako provided utataoa ushirikiano utakaohitajika. If you are serious hatua utaona zinachukuliwa but iwapo tuhuma mnazotoa ni za kufurahisha baraza then they will remain that way.

Mweny
 
Mkuu, this is true, ukiwa maeneo ya ubungo lock gari yako, wana tabia ya kukusimamisha kwenye foleni na kufungua mlango na kuingia kwenye gari, walinifanyia hivyo hawakujua mimi kichwa ngumu. Akanambia twende ubungo terminal, mi nikamuuliza ameingiaje kwenye gari yangu??' foleni ikaachia mi nikaingia sam nujoma kuelekea mwenge, ananiambia niweke gari pembeni, nikamwambia nimetoka home sikua na abiria, wewe umetoka wapi kwenye gari yangu??
Mwanaume nikapiga gia hadi mlimabi city, nikaingia survey, then chuo, then utawala, nikakamata njia ya changanyikeni.....akanambia ninamteka na kwamba ninaenda maporini kumuua, nikamwambia kama vile shehe yahaya, umejuaje??
Akataka kuruka kwenye gari pale kituo cha polisi utawala, akaogopa, nikafika mbele nikamwambia shuka, akashuka.....mimi nikapiga gia nikatambaaa zangu!

Nikaenda mwenye ubungo kesho yake, nikaongea na mkuu wa kituo... Wana njaaa sana hawa. Akabambia imeripotiwa lakini nimpe laki tano aimalize, nikamwambia nikikupa laki tano utakuwa huna kazi tena, fanya nikupe fifty tuachane kiungwana, na huyo mbwa wako asinifuate tena nitampeleka pande!!

tena mjihadhari kweli na traffic wa ubungo, ukikataa kuwapa pesa na wakiogopa personality yako wanakupa kesi. Mazingira ya mtoa mada yanafanana kabisa na yaliyonikuta walinipa kesi ya kumteka askari na wanakuweka celo ndio mchezo wao.
Tukichukua nchi 2015 ni kulibomoa lote na kuwapa kazi wajeda, simu lazima wakuzuie wakikuogopa.
 
polisi wa tanzania si wazalendo wamejaa njaa na ukosefu wa maadili ya kazi zao, hawa ndio wanasababisha hata kuongezeka kwa ajali barabarani kwa sababu baada ya kufanya kazi yao kwa ufanisi huachia maovu chungu nzima kwa kutaka pesa.

mambo haya ya uonevu wa polisi hutokea sana karibu kila siku. nafikiri ifike wakati wananchi tutafute njia ya kuukomesha udhalimu huu na uonevu tukifanyiwa mambo kama haya ni kuripoti katika vituo vya haki za binadamu na asasi za kiraia kwa sababu ukiripoti kwa afisa mkuu wa polisi hamna anachofanya ukiripoti takukuru nao njaa tu. poleni sana wote mliokumbwa na mikasa hii
 
polisi wa tanzania si wazalendo wamejaa njaa na ukosefu wa maadili ya kazi zao, hawa ndio wanasababisha hata kuongezeka kwa ajali barabarani kwa sababu baada ya kufanya kazi yao kwa ufanisi huachia maovu chungu nzima kwa kutaka pesa.

mambo haya ya uonevu wa polisi hutokea sana karibu kila siku. nafikiri ifike wakati wananchi tutafute njia ya kuukomesha udhalimu huu na uonevu tukifanyiwa mambo kama haya ni kuripoti katika vituo vya haki za binadamu na asasi za kiraia kwa sababu ukiripoti kwa afisa mkuu wa polisi hamna anachofanya ukiripoti takukuru nao njaa tu. poleni sana wote mliokumbwa na mikasa hii

uliyonena yanaweza kuwa na element ya ukweli bt busara haikutumika ktk kufikisha ujumbe, problem ya watz ni kulalamika tuuuuu nadhani ndio mana Ben Nkapa aliwaita wavivu wa kufikiri.

Tusiendeshwe na hisia na ku-generalize mambo, i believe % police ukiwapa ushirikiano kuanzia kutoa taarifa na kwenda kutoa ushahidi unapotakiwa kufanya hivyo, hatua muafaka wanazichukua. Haiwezekani viongozi wote wa polisi na wizara kwa ujumla wanalinda maovu yanayofanywa na baadhi ya polisi.

Acheni blaa blaa, peleka hoja yako makao makuu ya polisi au wizarani uone hatua zinachukuliwa au la.
 
uliyonena yanaweza kuwa na element ya ukweli bt busara haikutumika ktk kufikisha ujumbe, problem ya watz ni kulalamika tuuuuu nadhani ndio mana Ben Nkapa aliwaita wavivu wa kufikiri.

Tusiendeshwe na hisia na ku-generalize mambo, i believe % police ukiwapa ushirikiano kuanzia kutoa taarifa na kwenda kutoa ushahidi unapotakiwa kufanya hivyo, hatua muafaka wanazichukua. Haiwezekani viongozi wote wa polisi na wizara kwa ujumla wanalinda maovu yanayofanywa na baadhi ya polisi.

Acheni blaa blaa, peleka hoja yako makao makuu ya polisi au wizarani uone hatua zinachukuliwa au la.

ndugu yangu labda kosa lenyewe liwe ni la kawaida sana lakini likiwa na kuwaumbua watu hata huko wizarani watanyanyua simu na kuwasiliana na kukujibu kuwa watafwatilia na yataishia juuu kwa juu. wapo wachache sana wanaofanya kazi kwa ufanisi lakini system ya kipolisi imekaa kulindana sana.haya nisemayo tunayashuhudia sana yakitokea.
 
ndugu yangu labda kosa lenyewe liwe ni la kawaida sana lakini likiwa na kuwaumbua watu hata huko wizarani watanyanyua simu na kuwasiliana na kukujibu kuwa watafwatilia na yataishia juuu kwa juu. wapo wachache sana wanaofanya kazi kwa ufanisi lakini system ya kipolisi imekaa kulindana sana.haya nisemayo tunayashuhudia sana yakitokea.

Sikubaliani na hoja yako Iron Lady, take it from me kama Jeshi la Polisi lingekuwa linatoa takwimu ya askari wanaofukuzwa kwa utovu wa nidhamu bac jamii ingeshangaa coz ni wengi.

Sio kweli kwamba system ya Polisi imekaa kulindana lindana, nenda kasome PGO utaona jinsi ilivyoya kikandamizaji kwa polisi na ndiyo inayotumika kuwaathibu polisi wanapokwenda kinyume na maadili.

Nasema tatizo mnaona vitendo hivyo vitakomeshwa kwa kuandika kwenye mitandao ya kijamii badala ya kuwasilisha hard evidence kwenye mamlaka husika, kutoa ushirikiano na kufuatilia kujua matokeo yake.

Realistically, watz tunapenda kushabikia mambo na kupaka matope kwa hisia za mtu fulani, tunafuata mkumbo
 
Back
Top Bottom